Prof. Kabudi Kutumbuliwa Na Magufuli Baada Ya Barrick Kuondoka?

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Mh Rais Magufuli ana falsafa yake ya kipekee anayoiamini katika uongozi wake na hii ndo nguzo kuu inayomfanya atimize majukumu yake sahihi katika kipindi chake cha uongozi.

Falsafa hiyo ni ya KUTOPENDA KUSHINDWA PALE ANAPOAMINI KUNA USAHIHI.

Prof.kabudi alishawahi kuambiwa na Rais "Nitakushangaa kama na hizi sheria ndogondogo zitakushinda na huo uprofesor wako, nitakushangaa sana" ni maneno ya Rais magufuli.

Leo hii Rais amemuamini na kumpa Prof.Kabudi kuwa mwenyekiti wa kamati ya mazungumzo dhidi ya Barrick Gold, amemuani kwakuwa pia ni waziri aliyemteua katika wizara muhimu ya sheria,

Huu ni mtego Mkubwa sana kwa Prof. Kabudi pamoja na kamati yake, endapo mazungumzo yataisha na hakuna ambacho serikali imekipata kutoka Barrick Gold basi dhahiri Prof.Kabudi atatumbuliwa kuwa waziri wa sheria kwa kushindwa kazi aliyopewa.

Pili ataingia kwenye mikono ya taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa na hatimae atakuta na kesi ya kuihujumu nchi na kuishia jela maana Rais haitamuingia akilini zaidi ya Trilion 425 akose hata robo yake.

Kazi kwako Prof. Kabudi maana kila Mtanzania anasubiri matokeo ya mazungumzo
 
Mafia zao huwa wanawatafuta watu wa kamati wawawawekea fedha kwenye account kisha wanaanza kuwatisha huku wakiwalazimisha wakosee mahala wanapopataka hapo game is over ukikomaa waeza poteza vitu vingi maishani hao jamaa wapo radhi kupoteza hata ukoo mzima na huwa hawashindwi..
 
Back
Top Bottom