KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,117
- 5,321
Natamani sana waziri Mkuu awe mwanamke tena mwanamke chuma kweli ,mwanamke wa shoka mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji na hapa ndio naliona jina la Prof. Joyce Ndalichako anafaa kwenye nafasi hiyo.
Mhe. Rais ,tafadhali mteue Prof. Ndalichako kama waziri Mkuu kwenye Serikali yako ili akusaidie kwenye ujenzi wa Tanzania imara na yenye nguvu na itakayovuka malengo ya ilani ya CCM ya uchaguzi Mkuu uliyoinadi nchi nzima kwa jasho na damu.
Kwa nini Prof.Joyce Ndalichako?
1. Uzoefu mkubwa :
Prof. Joyce Ndalichako ana uzoefu mkubwa mno kwenye utendaji Serikalini na anafahamu mifumo inavyofanya KAZI
2. Utendaji mzuri: katika watu wenye wasifu mzuri wa uchapakazi na utendaji mzuri , Prof. Ndalichako namuweka kwenye kundi hilo.
3. Misimamo isiyotumba: misimamo yake isiyotumba ndio inafanya nimuweke kwenye kundi la wanawake wa shoka na misimamo isiyotumba katika nchi hii. Hivyo ninaamini atafaa kwenye uwaziri Mkuu
4. Msomi mahiri: elimu yake itasaidia kufanya utambuzi na utatuzi wa haraka wa changamoto na kero za wananchi na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa Baraza lako.
5. Anajiamini sana : Prof. Ndalichako anajiamini na sio mtu wa kuyumbishwa katika maamuzi yake. Ninaamini kwa sifa hii atafaa kuwa waziri Mkuu.
6. Hana skendo ya ufisadi wala rushwa: Prof.Ndalichako hajawahi kupata kashfa ya ufisadi au rushwa katika kipindi chote Cha utumishi wake na atakuwa msaada katika kuwajibisha wezi na mafisadi wa mali za umma .
Ninaamini kwa sifa hizo na nyingine alizonazo Prof . Ndalichako anabaki kuwa mtu sahihi kwenye uwaziri Mkuu