Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

Prof. Baregu: Zitto ni mzigo

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,462
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye.

Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.

"Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu."

Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.

Prof. Baregu aliwahi kuwa "mlezi wa Zitto" ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho "kusaidia kumlea."[/COLOR]

Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, "Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki."

Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto "katikakati ya migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum," anaeleza Baregu.

Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.

 
Last edited by a moderator:
"Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye." Na Hiki Ndicho Kitu Kibaya Sana kwa Mwanadamu. Kauli ya Prof. Baregu ni Sahihi Kabisa, Kwa Sababu Hata Mshirika Wake Mkuu Prof. Kitila Mkumbo alipata Kusema Kuwa Mweshimiwa Mbowe Kama Mwenyekiti wa CHADEMA ni too Local.

Ngoja tusubiri tuone Watakavyokijenga Chama Chao Cha ACT, ambacho kwa Mtizamo wao Wanaona Wamekianzisha Watu Wasomi.

Ni Kweli Zitto ni Mzigo ambao Hata Mnyamwezi Hawezi Kuubeba.
 
CHAMA cha Alliance for Change and Transparance (ACT-Tanzania) kimefanikiwa kuishawishi kwa hoja mahakama kuu ya Tanzania na kushinda katika maombi ya zuio la muda yaliyoombwa na wanachama wake Kadawi Limbu na wenzake ya kutaka mahakama Kuu itoe amri ya zuio la muda kwamba Samson Mwigamba, Peter Mwambuja na Mohamed Masaga wasijihusishe na shughuli yoyote ya Chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa

Kutokana na kutupwa kwa zuio hilo la muda kesi ya msingi namba 21/2015 imepangwa kusikilizwa April 15 mwaka huu, huku Limbu na wenzake wakitakiwa kulipa theluthi moja ya gharama za kesi hiyo

Kabla ya Limbu na wenzake kuomba zuio la muda la kutaka Mwigamba na wenzake wasijishughulishe na kazi za Chama kwa nafasi ya Katibu Mkuu,Naibu katibu Mkuu na mhasibu,walifungua kesi ya msingi iliyokuwa na maombi manne

1 Mahakama kuu ya Tanzania Itamke kuwa Chama cha ACT-Tanzania haina kamati kuu na Halmashauri kuu

2 Mahakama kuu ya Tanzania itamke kuwa kikao halali cha viongozi wa ACT-Tanzania ni kile cha kamati kuu iliyokutana Disemba 31 mwaka jana

3 Mahakama kuu itamke kuwa washitakiwa watatu Mwigamba,Masaga na Mwambuja siyo wanachama halali wa ACT-Tanzania

4 Mahakama kuu iwatake washitakiwa kulipa gharama zote za kesi

Kwa upande wake wake Mwigamba na wenzake waliweka pingamizi la kusikilizwa kwa maombi ya zuio la muda ya Limbu na wenzake kwa hoja zifuatazo

1 Walalamikaji Limbu na wenzke hawakuonyesha ni kanuni gani ya kisheria waliyotumia kuiomba mahakama itoe zuio la awali

2 Kwenye hati ya mlalamikaji katika kesi ya msingi mlalamikaji namba moja ni Kadawi Lucas Limbu,lakini Kwenye hati ya kiapo ya maomb ya zuio la muda mla kiapo namba moja amejitambulisha kuwa ni ACT-Tz

3 Maombi hayo yangeweza kuombwa katika mahakama ya chini badala ya mahakama kuu

Kufuatia hoja hizo tatu za mawakili wanaowawakilisha kina Mwigamba, wakili wa Limbu na wenzake alikiri upungufu katika hati yao ya maombi hivyo mahakama kuu chini ya Jaji J.Mwandambo ikatupilia mbali maombi ya zuio la muda na kumtaka Mlalamikaji Kulipa gharama za kesi.
 
Prof Baregu anamshauri Zitto mchana, wakati yeye Zitto anashauriwa na wataalam wake usiku (Hii ni kazi mbaya kama ya kuosha nguruwe- anajigalagaza kwenye maji hayo hayo machafu uliomwoshea.
Waste of time!
 
Baregu naye ni miongoni mwa wazee mizigo kabisa akili zake zimenyonyoka kama nywele zake.
 
CHAMA cha Alliance for Change and Transparance (ACT-Tanzania) kimefanikiwa kuishawishi kwa

Kufuatia hoja hizo tatu za mawakili wanaowawakilisha kina Mwigamba, wakili wa Limbu na wenzake alikiri upungufu katika hati yao ya maombi hivyo mahakama kuu chini ya Jaji J.Mwandambo ikatupilia mbali maombi ya zuio la muda na kumtaka Mlalamikaji Kulipa gharama za kesi.
acha umbumbumbu wa kuleta habari zisizo fanana na mada
 
Hapa nadhani Baregu kaamua kutua mzigo maana kwa alivyokuwa anamtetea zitto, Sasa ameuona rangi zote za huyu dogo.

NENDA ZITTO MAJIVUNO NA UBINAFSI VIMEKUPONZA.
 
Prof Baregu anamshauri Zitto mchana, wakati yeye Zitto anashauriwa na wataalam wake usiku (Hii ni kazi mbaya kama ya kuosha nguruwe- anajigalagaza kwenye maji hayo hayo machafu uliomwoshea.
Waste of time!

Watalaamu wake wenyewe wakina Kitila.
Kwa hili la Zitto, Kitila ni wa kulaumiwa.
 
Zitto ni mzito sanaa elimu yake inamsaidia kwendea choon. Hana family Hana mama nan amshauri? Mzito sana huyu kinyongaaa
 
Back
Top Bottom