Prof. Baregu aivuruga CHADEMA

Prof. Baregu aivuruga CHADEMA

Mwita Maranya hii point yako ya neutrality is a symbol of weakness hata haina mashiko kwa siasa za Tanzania come 2015. Kwani hufahamu kama Tanzania ya 2015 itakuwa na Neutrality candidate ambao kwa lugha nyingine wataitwa Independent candidate. Sijui toka lini Independent candidate wakawa weakness.

Kitu kingine muhimu, Bible katika maandiko ya Matthew 6:1 yanasema, Be careful not to display your righteousness merely to be seen by people, otherwise you have no reward with your Father in heaven.

Kuna misukule wengi sana hapa JF kila kukicha wanapiga kelele na kudai wao ni wanaCHADEMA haswa wakati hata hawaifahamu Falsafa na Itikadi yake achilia mbali Katiba, Kanuni, Maadili na itifaki ya chama. Hawa kwangu ni kama makapi yanayosubiri kuwa RECYCLED na viongozi wa CHADEMA kwa jinsi wanavyopenda.

Maandiko yangu ndiyo VERITY AND IMPARTIALITY bila kujari kama yanaangaza upande fulani kisiasa.

mKUU Ng'wamapalala labda tujikite hapo kwa independent candidate vs neutral or (impartial candidate-kama nitakuwa sawa).

Ninaposema neutrality is a symbol of weakness ninamaanisha kuwa haiwezekani kabisa kwa mtu unayefuatilia masuala ya uendeshaji wa nchi yako; kisiasa, kijamii, kiuchumi n.k halafu useme kwamba uko neutral wakati kila unapoandika comments zako tunazisoma na kukuona una mapenzi na upande fulani wa siasa za Tanzania.

Kama kweli unataka kuwa impartial basi zingatia sana na kuuishi ushauri wa HT . Ikemee ccm sawa na unavyofanya kwa Chadema. Sio unapaza sauti kwa maswala ya Chadema lakini yakija ya ccm unaanza kunong'ona!! Jitathmini mwenyewe uone jinsi ulivyo na bidii ya kupost mambo yenye mtazamo hasi kwa Chadema huku ukiwa na bidii ya kupost mambo yenye mtazamo chanya kwa ccm. Hadi hapo utabaini kwamba rangi yako halisi umeshaibainisha kilichobaki ni kutoka hadharani na kuuikiri ukweli wa moyo wako...
 
Last edited by a moderator:
chadema ni chama imara sana cha upinzani Tanzania ilo halina ubishi. kimeibua maovu mengi sana yanayofanywa na utawala uliopo kwa sasa. ushauri kwa prof toa ushauri wako unaoitajika kwa tume lakini asiamini kuwa prof anakivuruga chama chetu cha kinachotetea watanzania walalahoi.chadema hoyeeeeeeeeeeeeee
 
Unapomkabidhi mtu NYUNDO usitegemee ataenda kuliweka bila kulifanyia kazi au hawezi kulitumia kukupigia kichwani pale unapomkosea.

A LITTLE CHADEMA boy has turned out to be a MONSTER.

CHADEMA kwa sasa kinaweweseka na jinsi ya kumkabili asije akaivuluga nyumba yao.

IS THIS A MISSION IMPOSSIBLE?.

Yetu ni macho na masikio.
Go on with your views you are a candidate for a BAN for false information

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/557865-sijajiuzulu-uongozi-chadema-prof-baregu.html

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Prof. Mwesiga Baregu amekanusha vikali taarifa za kujiuzulu nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA zilizozagaa kwenye mitandao, asema hana mpango wa kufanya hivyo.

Professa Baregu amesema uvumi huo unaenezwa na CCM na vibaraka wake na kuendelea kusisitiza kwamba Chadema itaendelea kuwa moja na Imara zaidi.

Source:Mwananchi Breaking News​
 
Profesa Baregu amgomea Slaa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni mhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbroad Slaa, alimwita msomi huyo ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe ndani ya Tume hiyo kwa sababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Baregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya Kiingereza, akisema: "If I told to choose between my country and my party (CHADEMA), I will choose my country," akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha CHADEMA, angechagua nchi yake kwanza.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake, Dk Slaa, pamoja na chama chake cha CHADEMA, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.

Itakumbukwa kwamba CHADEMA, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakati akiwasilisha hotuba mbadala ya kambi rasmi ya upinzani kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba, akitaja sababu kadhaa, zikiwamo za mchakato mzima huo kutekwa na CCM na lakini pia kwamba wajumbe wa Tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

"Ni kweli, niliitwa na Katibu Mkuu (Dk Slaa), akaniambia Kamati Kuu ya chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, na kwa hiyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili; kwanza kijitoe na pili, kikishakujitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo," anasema Profesa Baregu katika mahojiano maalum na Raia Mwema.

Anasema aliomba kujulishwa rasmi maamuzi hayo ya CC kwa maandishi, ili ajue atachukua uamuzi gani lakini hadi anafanya mahojiano na Raia Mwema hakuwa amepata majibu, huku akisema kwamba kwa maoni yake kama kweli yalikua ni mamuzi ya kikao, basi Kamati Kuu itakua ilifanya makosa kufikia uamuzi wa kujitoa bila kumshirikisha.

"Kwanini? Mimi tangu mwanzo kabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni suala la mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba CHADEMA ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya ya Katiba. Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010 na nilishiriki kuandika Ilani ya uchaguzi, na hili la kutaka Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu.

"Wakati ule wenzetu (CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na Katiba mpya, iliyopo inatosha, lakini baadaye Serikali ikaona ipo haja ya kuwa na Katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo. Muswada ukapelekwa bungeni, wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. CHADEMA tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yakakubaliwa.

"Muswada ukarudishwa bungeni upya, sheria ikafanyiwa marekebisho na kukubaliwa na wabunge wa kambi ya upinzani. Sasa leo hii, wabunge wale wale waliokubali, wanataka kukataa mchakato wa Katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe…kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato, yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo, nisingekuwamo humu, ningejitoa. Tunatengeneza Katiba ya Watanzania wote, si Katiba ya chama fulani.

"Lakini pia, CHADEMA tulipokutana na Rais (Jakaya Kikwete), alitushauri na tukakubaliana naye, twende hatua kwa hatua. Itungwe sheria yenyewe kwanza, halafu iundwe Tume, baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa... tangu wakati huo hadi sasa nadhani sisi kama Tume tunafanya vizuri ikilinganishwa na wenzetu huko nje walioandika upya Katiba yao.

"Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa Bunge Maalumu la Katiba, hatua hii nayo wananchi wametakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ya muundo wa Bunge hilo. Ushauri wangu kwa CHADEMA, naomba chama chetu kikae mkao wa kujenga nchi yetu, na si mkao wa kuibomoa. Kama chama tukae na Watanzania kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yetu hii kwa sababu fursa hii haitakuja tena karibuni labda baada ya miaka 50 ijayo…kuzira, kujitoa, nasema Watanzania hawatatuelewa."

Akifafanua msimamo wake alioutoa kwa Dk Slaa kwamba kama angeambiwa achague kati ya nchi yake na chama chake, angechagua nchi kwanza, Profesa Barugu anasema: "Ndiyo, chama kinaundwa na kinapita, lakini Tanzania kama nchi itaendelea kuwepo daima. Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba kwa kuwa sisi tulishajiweka katika kusimamia mchakato huu wa kuwa na Katiba mpya, tusijiharibie kwa kuvuruga mchakato huu."

Chanzo:
Raia Mwema

Toleo la 292
1 May 2013
 
Back
Top Bottom