Molemo nduguPoor Mtanzania.
Wimbo wao wa Ugaidi umechuja.Pia ule wa Dr Slaa kumuua Zitto nao umechuja.Sasa wameibuka na Baregu.
Hili gazeti ni sawa na Toilet Paper
Kama Bwana wako hana njaa mbona kakupa tenda ya kuweka mfumo wa kompyuta bila kufuata taratibu? mnajipopesha mapesa ya kujengea nyumba nje ya utaratibu hii sio tu njaa bali ni ufisadi ulio kubuhu.
Iweje chama kilipe mpaka posho wa house girl wenu mkienda kutembea Arusha?
Nakubaliana na wewe akili yake ukichanganya na ya kwako mnakwapua mahela ya ruzuku kama mchwa anavyo kula gogo.
Josephine wewe ndie janga la taifa umemuacha mume wako wa ndoa kufuata fedha kwa Padri unajidhalilisha
Rafiki,
Dr Slaa hana njaa.
Utajiri na hazina kubwa ya Elimu ni utajiri tosha anaojivunia.
kama ni pesa,Akili yake inauwezo wa kumuingizia mamilioni.
Watanzania yawapasa kufikia sehemu mruhusu ubongo ufanye kazi.watu kama wewe ni janga Taifa.
Wapo Wapumbavu watakaoshambulia Gazeti badala ya kujadili hoja. Chadema wabadilike waruhusu watu wenye mawazo mbadala ndio maana ya Demokarsia
Rafiki,
Dr Slaa hana njaa.
Utajiri na hazina kubwa ya Elimu ni utajiri tosha anaojivunia.
kama ni pesa,Akili yake inauwezo wa kumuingizia mamilioni.
Watanzania yawapasa kufikia sehemu mruhusu ubongo ufanye kazi.watu kama wewe ni janga Taifa.
Hii ni moja ya sifa ya Profesa...huwa sio mtu wa kupelekeshwa bali ni mtu anayeamini katika kile anachokiona....au kile ambacho kulingana na tafiti au factors nyingine ameshapima na kuona advantages outweigh disadvantages!
kama katiba ingekuwa ya nchi, ccm ingejaza wanachama wake wote kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya? Ccm wamebaka mchakato mzima wa katiba, kana kwamba katiba ni ya ccm pekee!Nchi kwanza...........Chama baadae.
Tatizo la Babu Slaa na DJ Mbowe wanataka wanachokisema wao basi iwe ndio tu na wamesahau kuwa KATIBA NI YA NCHI wala si ya Vyama vya Siasa!
hakuna chochote mkuu, ni mlungula wa kikwete kwa wajumbe wa katiba, mabilioni. Chezea ccm wewe!Siku zote mkifanya Chama kama mali ya watu fulani fulani ndio madhara yake haya!
Hivi kuna wasomi wangapi nchi hii ambao hawakupata fursa ya kutoa utaalam wao katika CCM wanataka kutoa mchango wao kwa taifa kupitia katika vyama vingine, lakini wakiangalia mfumo wa hivyo vyama vingine unawanyima fursa ya kuwa huru.
Kama hili swala linavyokomaliwa na Dr. bingwa wa magonjwa ya kinamama
Profesa Baregu anaweza kuwa chachu ya wasomi wengi kuingia katika vyama hvi pinzani, endapo tu ataachwa kuwa huru na kushirikiana na wajumbe wengine katika kutuletea katiba mpya.
Profesa Baregu komaa hapa ndio taifa litakapoweka history yako miaka 50 mbele, hii sio tume kama ya Waziri mkuu Pinda kumchagua Mbatia kisha kukataa uteuzi, na watu kumjaza misifa humu JF kumbe angaingia mle angejua mambo mengi ambayo yangemsaidia mbeleni.
kaka mlungula wa kikwete, prof anapewa mamilioni na gari full tank, hamna lolote!Unajua sisi Chadema ndio tunamvuruga Prof. Baregu.
Hasa Mgombea Urais wa 2015 Dk Slaa!
Nchi kwanza...........Chama baadae.
Tatizo la Babu Slaa na DJ Mbowe wanataka wanachokisema wao basi iwe ndio tu na wamesahau kuwa KATIBA NI YA NCHI wala si ya Vyama vya Siasa!
*Msimamo wake Katiba Mpya wakitikisa CHADEMA na Watanzania.
*Dk. Slaa asema atahukumiwa Kamati Kuu
MSIMAMO wa mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesigwa Baregu.
Hii hapo juu ni posti yako uliponijibu kule ule mjadala ukijidai hujui ama kufahamu nafasi ya Bagenda kwenye hiyo tume.Kama kuna huwezi,ni heri unyamaze,na kama huna knowledge kuhusu hiyo,pia ni bora usome tu maoni ya wengine.Ng'wamapalala said:Mkuu, Bagenda siyo mjumbe wa kamati. Labda sijakuelewa una maana gani unaposema ni mwakilishi wa CHADEMA.
Hii hapo juu ni posti yako uliponijibu kule ule mjadala ukijidai hujui ama kufahamu nafasi ya Bagenda kwenye hiyo tume.Kama kuna huwezi,ni heri unyamaze,na kama huna knowledge kuhusu hiyo,pia ni bora usome tu maoni ya wengine.
Sasa rudi kwenye ile thread kule uniambie kama umeelewa kuwa Bagenda ni mwakilishi wa chadema au bado.
Vichwa vingine bana!Ndo maana kuna wanaodai mnalipwa mkiposti.Maana saa nyingine huwa mnabandika tu.
MLENGWA WA MLIPUKO ALIKUWA BALOZI WA VATICAN?
(Naona mods wana watu wao wenye haki ya kuanzisha threads, sisi wengine haturuhusiwi)
Ndugu WanaJamvi;
Kwa muda sasa kumekuwa na hoja mbali mbali juu ya uhalali wa uwepo wa Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania. Katika hili kuna, kuna pande kuu mbili zinazokinzana - wanaopinga na wanaounga mkono kama ifuatavyo:-
(1) Wanaopinga: wanajenga hoja kwamba kwa kuwa Vatican ni nchi ya kidini (Kikatoliki) na kwa kuwa, kwa mujibu wa Katiba, Tanzania haina dini hivyo sio sahihi kwa "nchi" hiyo kuwa na ubalozi wake hapa nchini. Wengine wanaenda mbali zaidi kiasi kwamba hawataki kukubali Vatican ni nchi. Hata hivyo "wanalegeza" masharti kwamba kama Vatican ina ubalozi wake hapa basi ni halali kwa Tanzania kama nchi kuwa mwanachama wa taasisi za kidini kama OIC. La kushangaza hapa ni kwamba kwao uhalali wa Ubalozi wa Vatican utakuwepo endapo Tanzania itakuwa mwanachama wa hizo taasisi za kidini vinginevyo sio halali.
(2) Wanaounga mkono:hawa wanajenga hoja kwamba; kwanza Vatican ni nchi huru, yenye mamlaka kamili, na inayojitegemea kwa mujibu wa tafsiri sahihi ya neno "nchi" lilivyo na linavyotambulika kimataifa. Na wanaenda mbali zaidi kwamba sio tu kwamba Vatican ni nchi bali inatambulika hivyo rasmi na UN. Hivyo, kwa hoja hii, ni sahihi kabisa Vatican na Tanzania kuwa na mabalozi wanowakilisha nchi zao.
MLIPUKO WA LEO:
Kati ya viongozi wakuu wa Kanisa waliokuwepo kwenye shughuli ya leo kule Olasiti, Arusha, ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambaye pia ana hadhi ya Askofu Mkuu. Hivyo zimeanza kuzagaa habari pengine kutokana na ukinzani wa baadhi ya makundi kutotaka Vatican kuwa na ubalozi wake hapa nchini, kuna uwezekano pia mlengwa mkuu alikuwa Balozi husika. Mimi sijui, ila kama GT tudadavue na hili.
LAWAMA:
Lawama pia zimeanza kuelekezwa kwa serikali kwa kutochukua hatua madhubuti na kwa wakati pindi zinapotokea chochoko kama hizi katika jamii. Kwa mfano, hili la upotoshoji wa uhalali wa Ubalozi wa Vatican hapa nchini propaganda zake zimeenezwa kwa muda mrefu sana kwa njia mbalimbali kama mihadhara, ibada, na hata kwenye media mbalimbali. Badala ya serikali kutolea ufafanuzi wa uhalali wa huo ubalozi, imekuwa kimya bila kujali athari za baadaye za propaganda hizi chafu pengine kwa falsafa ya "ni upepo tu utapita". Je, ni kweli serikali inastahili lawama katika hili?
HITIMISHO:
Je, kama serikali ikitekeleza madai YOTE ya haya makundi, kuna uwezekano wa chokochoko hizi kukoma na hivyo nchi yetu kuwa ya amani na utulivu kama ilivyoachwa na waasisi wetu? Lakini je, walengwa wa haya matukio ni wakatoliki peke yao? Au ni pamoja na makundi mengine? Haya matukio yana uhusiano wowote na siasa za nchi yetu? Mimi sijui, nalileta kwenu wakuu.