Prof. Ali Mazrui mwalimu wangu wa masafa marefu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
Leo alfajir nimeikuta video ya Mwalimu wangu wa masafa marefu Prof. Ali Mazrui.bImenikumbusha mbali.

Nina umri wa miaka 15/16 namsoma Ali Mazrui katika Sunday Nation kutoka Kenya.

Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."

Sikusita nikakinunua.
Nikimpenda Mazrui sana.

Katika umri ule nilikuwa namsoma Kwame Nkrumah, "Challenge of the Congo."
Namsoma Nkrumah anavyochambua matatizo na fitna ya kampuni kubwa ya Wabelgiji - Union Miniere kwa Patrice Lumumba.

Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.

Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.

Hela zangu zilikuwa zinakwenda kwanza kwenye comics, ice cream, records na mwisho tiketi za cinema kuangalia movies Jumamosi mchana na Jumapili asubuhi saa nne Empire Cinema.

Mara yangu kumuona Prof. Mazrui ilikuwa miaka ya mwishoni 1960s Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sikumbuki ilikuwa kwenye sherehe gani na Julius Nyerere alikuwapo.

Nilikuwa nimefuatana na kaka yangu na rafiki yangu pia Shaabani Muhunzi maarufu kwa jina la Mkorofi yeye alikuwa mwanafunzi pale chuoni na nikimuusudu sana kwa hilo.

Shaaban alinitia hamu ya mimi kufika alipofika yeye.

Chumbani kwangu nilikuwa na ubao na ubao huu alinipa Abdallah Tambaza.

Hivi sasa Abdallah ni mwandishi nguli wa historia ya Dar es Salaam.

Shaaban akija chumbani kwangu mwisho wa juma akitokea Chuo Kikuu anakuta kwenye ubao juu kabisa nimeandika, "English Literature."

Chini yake patafuatia ''passages'' za William Shakespeare tene nikiziandika kutoka kichwani.

Yeye atafuta ataandika, "Literature in English," kunisahihisha bwana mdogo wake.

Akiondoka nitafuta na nitaandika kama nilivyoandika mwanzo.

Juma linalofuatia itakuwa mchezo ni ule ule.

Atanisahihisha mwanafunzi mkaidi na mwalimu wangu akiondoka nitafuta.

Sasa nimekuwa kijana wa kati Mazrui akatengeneza ile ''documentary'' maarufu sana, "Africans: A Triple Heritage."

Hapa ndiyo alinimaliza kabisa.

Nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Said Baamumin tukikaa jirani yeye akifanyakazi UNDP.

Siku moja akaniambia angependa kunipeleka kwao Mtondia Mombasa nikamuone mama yake.

Said Bamumin akanifahamisha kuwa wao wamejenga na wana mashamba katika ardhi ya ukoo wa Mazrui.

Tulipofika Mtondia akanipeleka Takaungu kuona msikiti wa Mazrui ambao una umri kiasi ya miaka 400 na kisima cha asili kipo hapo na bado kinatoa maji.

Ardhi hii ya ukoo wa Mazrui ina historia ndefu katika historia ya Kenya na Mombasa.

Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilimpelekea nakala mwalimu wangu na niliandika ''Kwa Mwalimu wangu wa Masafa Marefu Prof. Ali Mazrui.''

Hapa pana kisa kidogo.

Balozi Ramadhani Dau rafiki na ndugu yangu yeye alikuwa akifahamiana na Prof. Mazrui na wakiandikiana.

Nadhani labda kwa kujua mapenzi niliyokuwanayo kwa Prof. siku hiyo akaniambia kuwa yeye anakwenda New York na itakuwa vyema kama nitampa kitabu changu ampelekee Prof. Mazrui.

Hivi ndivyo nilivyofahamiana na Prof. Mazrui na tukawa tunaandikiana.

Nakumbuka baada ya kupata kile kitabu Prof. aliniandikia kunishukuru na akaniambia, ''Nimefurahi jinsi ulivyowaandika Waswahili.''

Miaka ikaenda.

Huyu huyu Balozi Dau akanikutanisha na Dr. Harith Ghassany.

Nilikuwa nakwenda Mascut Balozi Dau akanipa kitabu changu mwenyewe cha Abdul Sykes akaniambia nimfikishie rafiki yake Dr. Harith Ghassany Muscat.

Hivi ndivyo nilivyokuja kufahamiana na Dr. Ghassany tukawa marafiki ndugu.

Harith Ghassany ndiye yeye aliyenijulisha tena kwa Prof. Mazrui kwa staili nyingine kabisa.

Nilikuwa nimealikwa mkutano Kampala na Prof. Mazrui alikuwa na yeye amealikwa pia.
Nilipomfahamisha Harith akanipa salamu nimfikishie Prof. Mazrui.

Harith alisomeshwa na Prof. Mazrui University of Michigan.

Sote tulikuwa tunakaa Hilton Hotel.

Nilikuwa nimesimama kwenye ''lobby'' ya hotel kwa mbali nikamuona Prof. Mazrui anakuja upande wangu.

Aliponikaribia nikapiga hatua nikamtolea salamu.

Akaniitikia na alipoona ile tabasamu yangu hakupita akaniuliza, ''Tunafahamiana?''

Nikamtaja Balozi Dau na nikamwambia pia nina salamu zake kutoka kwa Dr. Ghassany.

Nilikuwa nimemtajia Prof. Mazrui watu wake basi akaniambia tukae kitako tuzungumze.

Nilimstaajabisha sana nilipomwambia kuwa nimefika hadi kwao Takaungu na tulizungumza mengi na haukupita muda jamaa wengi wakaja pale tukakaa na Prof. Mazrui na kuzungumzanae.

Mazrui ni mtu asiye na makuu mwepesi wa kuingilika.

Alizungumza na sisi kama vile ni watu tunajuana miaka.

Siku anaondoka kurudi Marekani kanikuta pale ''reception,'' kaja ku-''check out,'' na mimi nina ''check out,'' tukaagana.

Nakumbuka ''typical Mazrui trend,'' alimwambia Manager on Duty pale Hilton, ''Tengenezeni hizi lift kwani zinagoma sana na ikija Mmarekani kanasa kwenye hizi lift zenu atawapelekeni mahakamani.''

Sijui kama wenzangu waliokuwa pale walielewa lakini kwangu mimi ujumbe ulikuwa umefika sawia.

Nikamkumbuka katika ''The Africans: A Triple Heritage,'' anaonekana anafungua bomba la maji katika hoteli moja ya Nyota Tano katika mji mmoja mkubwa Afrika bomba linakohoa halitoi maji.

Mimi kwa tahadhari ile Prof. akawa kanikumbusha hoteli moja Lagos ndiyo nimefika nataka kukoga, nimefungua bomba la maji kwanza bomba likakohoa kisha maji yakaanza kutoka lakini rangi yake ilikuwa ya udongo, rangi ya kahawia.
 
Navutiwa sana na historia unazo tupatia.
Mimi pia hua ananikosha na kuniliwaza sana huyu Maalim Mohamed Said, ni mtu mmoja anaenisababishia kuchelewa sana kulala usiku hasa weekend (Last weekend amenilaza alfajiri kwa kusoma makala zake).

Binafsi ni mpenzi sana wa kusoma vitabu, ni ugonjwa wangu mkuu, na katika usomaji wa vitabu nimeweka matabaka mawili ya waandishi, yaani kuna waandishi aina mbili, waandishi walisoma kwa waandishi (Waandishi wa zamani) na waandishi waliosoma shule (Waandishi wa sasa hivi).

Waandishi waliosoma kwa waandishi makala zao huwa ni fikirishi na zinakutoa katika ulimwengu uliopo kihalisia na kukupeleka katika zama zinazoelezewa katika hio makala (Yaani unajihisi kama na wewe ulikuwepo na muandishi katika hayo matukio).

Waandishi waliosoma shule, ni wale ambao anaandika ili kufundisha au kuelewa, makala haikuchukui kisaikolojia.

This man is gifted in writting. He has an amazing capabilities to turn his views/past/reality in to words/text that time travels your mind.
 
Mzee wangu uko na kumbukumbu nzuri sana vijana sasa hivi hawajielewi vitu vizuri hawataki kusoma wao ni upuuzi tu sasa hazina kama hizi ndio za kushikilia hata siku wakiondoka ndo tayari tushayakwaa maarifa yao
 
Asante kwa bandiko

Hivi profesa Mazrui ana ujamaa na Ahmed Mazrui yule aliyetajwa kwenye kitabu cha Dr. Harith Gasanny cha 'Kwaheri ukoloni kwa heri uhuru'?

Mazrui wa katika kitabu hiko alikuwa akimiliki kampuni ya ujenzi ambayo John Okelo alikuwa kibarua katika kampuni hiyo.
Mimi pia hua ananikosha na kuniliwaza sana huyu Maalim Mohamed Said, ni mtu mmoja anaenisababishia kuchelewa sana kulala usiku hasa weekend (Last weekend amenilaza alfajiri kwa kusoma makala zake).

Binafsi ni mpenzi sana wa kusoma vitabu, ni ugonjwa wangu mkuu, na katika usomaji wa vitabu nimeweka matabaka mawili ya waandishi, yaani kuna waandishi aina mbili, waandishi walisoma kwa waandishi (Waandishi wa zamani) na waandishi waliosoma shule (Waandishi wa sasa hivi).

Waandishi waliosoma kwa waandishi makala zao huwa ni fikirishi na zinakutoa katika ulimwengu uliopo kihalisia na kukupeleka katika zama zinazoelezewa katika hio makala (Yaani unajihisi kama na wewe ulikuwepo na muandishi katika hayo matukio).

Waandishi waliosoma shule, ni wale ambao anaandika ili kufundisha au kuelewa, makala haikuchukui kisaikolojia.

This man is gifted in writting. He has an amazing capabilities to turn his views/past/reality in to words/text that time travels your mind.
 
Leo alfajir nimeikuta video ya Mwalimu wangu wa masafa marefu Prof. Ali Mazrui.
Imenikumbusha mbali.

Nina umri wa miaka 15/16 namsoma Ali Mazrui katika Sunday Nation kutoka Kenya.

Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."

Sikusita nikakinunua.
Nikimpenda Mazrui sana.

Katika umri ule nilikuwa namsoma Kwame Nkrumah, "Challenge of the Congo."

Namsoma Nkrumah anavyochambua matatizo na fitna ya kampuni kubwa ya Wabelgiji - Union Miniere kwa Patrice Lumumba.

Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.

Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.

Hela zangu zilikuwa zinakwenda kwanza kwenye comics, ice cream, records na mwisho tiketi za cinema kuangalia movies Jumamosi mchana na Jumapili asubuhi saa nne Empire Cinema.

Mara yangu kumuona Prof. Mazrui ilikuwa miaka ya mwishoni 1960s Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sikumbuki ilikuwa kwenye sherehe gani na Julius Nyerere alikuwapo.

Nilikuwa nimefuatana na kaka yangu na rafiki yangu pia Shaabani Muhunzi maarufu kwa jina la Mkorofi yeye alikuwa mwanafunzi pale chuoni na nikimuusudu sana kwa hilo.

Shaaban alinitia hamu ya mimi kufika alipofika yeye.

Chumbani kwangu nilikuwa na ubao na ubao huu alinipa Abdallah Tambaza.

Hivi sasa Abdallah ni mwandishi nguli wa historia ya Dar es Salaam.

Shaaban akija chumbani kwangu mwisho wa juma akitokea Chuo Kikuu anakuta kwenye ubao juu kabisa nimeandika, "English Literature."

Chini yake patafuatia ''passages'' za William Shakespeare tene nikiziandika kutoka kichwani.

Yeye atafuta ataandika, "Literature in English," kunisahihisha bwana mdogo wake.

Akiondoka nitafuta na nitaandika kama nilivyoandika mwanzo.

Juma linalofuatia itakuwa mchezo ni ule ule.

Atanisahihisha mwanafunzi mkaidi na mwalimu wangu akiondoka nitafuta.

Sasa nimekuwa kijana wa kati Mazrui akatengeneza ile ''documentary'' maarufu sana, "Africans: A Triple Heritage."

Hapa ndiyo alinimaliza kabisa.

Nilikuwa na rafiki yangu kipenzi Said Baamumin tukikaa jirani yeye akifanyakazi UNDP.

Siku moja akaniambia angependa kunipeleka kwao Mtondia Mombasa nikamuone mama yake.

Said Bamumin akanifahamisha kuwa wao wamejenga na wana mashamba katika ardhi ya ukoo wa Mazrui.

Tulipofika Mtondia akanipeleka Takaungu kuona msikiti wa Mazrui ambao una umri kiasi ya miaka 400 na kisima cha asili kipo hapo na bado kinatoa maji.

Ardhi hii ya ukoo wa Mazrui ina historia ndefu katika historia ya Kenya na Mombasa.

Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes nilimpelekea nakala mwalimu wangu na niliandika ''Kwa Mwalimu wangu wa Masafa Marefu Prof. Ali Mazrui.''

Hapa pana kisa kidogo.

Balozi Ramadhani Dau rafiki na ndugu yangu yeye alikuwa akifahamiana na Prof. Mazrui na wakiandikiana.

Nadhani labda kwa kujua mapenzi niliyokuwanayo kwa Prof. siku hiyo akaniambia kuwa yeye anakwenda New York na itakuwa vyema kama nitampa kitabu changu ampelekee Prof. Mazrui.

Hivi ndivyo nilivyofahamiana na Prof. Mazrui na tukawa tunaandikiana.

Nakumbuka baada ya kupata kile kitabu Prof. aliniandikia kunishukuru na akaniambia, ''Nimefurahi jinsi ulivyowaandika Waswahili.''

Miaka ikaenda.

Huyu huyu Balozi Dau akanikutanisha na Dr. Harith Ghassany.

Nilikuwa nakwenda Mascut Balozi Dau akanipa kitabu changu mwenyewe cha Abdul Sykes akaniambia nimfikishie rafiki yake Dr. Harith Ghassany Muscat.

Hivi ndivyo nilivyokuja kufahamiana na Dr. Ghassany tukawa marafiki ndugu.

Harith Ghassany ndiye yeye aliyenijulisha tena kwa Prof. Mazrui kwa staili nyingine kabisa.

Nilikuwa nimealikwa mkutano Kampala na Prof. Mazrui alikuwa na yeye amealikwa pia.
Nilipomfahamisha Harith akanipa salamu nimfikishie Prof. Mazrui.

Harith alisomeshwa na Prof. Mazrui University of Michigan.

Sote tulikuwa tunakaa Hilton Hotel.

Nilikuwa nimesimama kwenye ''lobby'' ya hotel kwa mbali nikamuona Prof. Mazrui anakuja upande wangu.

Aliponikaribia nikapiga hatua nikamtolea salamu.

Akaniitikia na alipoona ile tabasamu yangu hakupita akaniuliza, ''Tunafahamiana?''

Nikamtaja Balozi Dau na nikamwambia pia nina salamu zake kutoka kwa Dr. Ghassany.

Nilikuwa nimemtajia Prof. Mazrui watu wake basi akaniambia tukae kitako tuzungumze.

Nilimstaajabisha sana nilipomwambia kuwa nimefika hadi kwao Takaungu na tulizungumza mengi na haukupita muda jamaa wengi wakaja pale tukakaa na Prof. Mazrui na kuzungumzanae.

Mazrui ni mtu asiye na makuu mwepesi wa kuingilika.

Alizungumza na sisi kama vile ni watu tunajuana miaka.

Siku anaondoka kurudi Marekani kanikuta pale ''reception,'' kaja ku-''check out,'' na mimi nina ''check out,'' tukaagana.

Nakumbuka ''typical Mazrui trend,'' alimwambia Manager on Duty pale Hilton, ''Tengenezeni hizi lift kwani zinagoma sana na ikija Mmarekani kanasa kwenye hizi lift zenu atawapelekeni mahakamani.''

Sijui kama wenzangu waliokuwa pale walielewa lakini kwangu mimi ujumbe ulikuwa umefika sawia.

Nikamkumbuka katika ''The Africans: A Triple Heritage,'' anaonekana anafungua bomba la maji katika hoteli moja ya Nyota Tano katika mji mmoja mkubwa Afrika bomba linakohoa halitoi maji.

Mimi kwa tahadhari ile Prof. akawa kanikumbusha hoteli moja Lagos ndiyo nimefika nataka kukoga, nimefungua bomba la maji kwanza bomba likakohoa kisha maji yakaanza kutoka lakini rangi yake ilikuwa ya udongo, rangi ya kahawia.
Picha
IMG-20201203-WA0103.jpg
Screenshot_20201203-084515.jpg
 
MZEE KUMBE UMESOMESHWA NA WAKATOLIKI?

UNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU NA KUMTUKUZA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI KWA BARAKA ZAKE ZILIZOKUPATIA ELIMU

"Siku moja napita Kanti Bookshop duka la vitabu karibu na shule yangu St. Joseph's Convent nikakiona kitabu chake, "On Heroes and Uhuru Worship."
 
Uzalendo...
Darasa la kwanza nimesoma Lutheran Primary School, Moshi.

Sekondari ndiyo nikasoma St. Joseph's Convent School.

Hakika nina kila sababu ya kulishukuru kanisa kwa elimu niliyopata.

Umemtaja Yesu nami napenda nikufahamishe kuwa Uislam hauna tatizo lolote na Bwana Yesu mjumbe wa Allah.

Katika Qur'an Mwenyezi Mungu amemtaja kwa jina la Isa bin Maryam na kaeleza kuzaliwa kwake kwa miujiza bila baba na akampa miujiza ya kufufua na kuponya kwa idhini yake Mungu.

Allah anaeleza jinsi alivyomnyanyua mbinguni pale Wayahudi walipomzingira ili wamuue.

Si haya tu Allah akaweka sura nzima katika Qur'an "Surat Maryam," anatueleza habari za mama yake Yesu.

Hii ndiyo heshima ya Yesu kwetu sisi Waislam na wala hatubagui baina ya Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Haya ndiyo mafunzo yetu.
 
Ufafanuzi mzuri uliojaa hekima

Hata hivyo kuna nyongeza kama ifuatavyo:

Yesu Kristi alikufa kwa kutundikwa Msalabani na alifufuka siku ya tatu.

Kifo chake kilileta Ukombozi kwa Wanadamu wote.

Yesu Kristo alipaa mbinguni siku 40 baada ya kufufuka na sasa ameketi karibu na Kiti cha Baba Yake

Yesu Kristo atarudi siku ya kiama ili kutoa hukumu kwa wote akiwemo " Mtume" Muhamadi

Aksante

Uzalendo...
Darasa la kwanza nimesoma Lutheran Primary School, Moshi.

Sekondari ndiyo nikasoma St. Joseph's Convent School.

Hakika nina kila sababu ya kulishukuru kanisa kwa elimu niliyopata.

Umemtaja Yesu nami napenda nikufahamishe kuwa Uislam hauna tatizo tatizo lolote na Bwana Yesu mjumbe wa Allah.

Katika Qur'an Mwenyezi Mungu amemtaja kwa jina la Isa bin Maryam na kaeleza kuzaliwa kwake kwa miujiza bila baba na akampa miujiza ya kufufua na kuponya kwa idhini yake Mungu.

Allah anaeleza jinsi alivyomnyanyua mbinguni pale Wayahudi walipomzingira ili wamuue.

Si haya tu Allah akaweka sura nzima katika Qur'an "Surat Maryam," anatueleza habari za mama yake Yesu.

Hii ndiyo heshima ya Yesu kwetu sisi Waislam na wala hatubagui baina ya Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Haya ndiyo mafunzo yetu.
 
...

Nikiangalia nyuma leo hata sielewi nini kilikuwa kinanisukuma kuchukua mkondo ule wa usomaji vitabu.

Juu ya haya siachi kusikiliza muziki wa Elvis Presley, Beatles, Wilson Picket kwa kuwataja wachache.

...
Sheikh Mohamed na wewe unasikiliza mambo ya kikafir? Sikutegemea statement kama hiyo kutoka kwako Mzee wetu.
 
Back
Top Bottom