Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,242
- 33,850
Mohamed Said, anasimulia:
"Nikiwa mtoto mdogo katika miaka ya katikati ya sitini, nilikuwa nikisikiliza muziki wa Sal Davis... nikiimba na mwingine nikipiga kwenye gitaa langu.
Siku moja baada ya karibu miaka 40, mimi hapa Dar es Salaam nakutana na Sal Davis kwenye baraza letu pale Lumumba usiku. Mimi nilishtuka pale, nikamwambia 'Wewe Sal Davis? Sal Davis ikawa ni mada kubwa mimi bwana, wewe ni mwanangu bwana.'
Basi nikamwambia 'Aah bwana, miaka mingi sijakuona.' Basi na yeye akawa amefurahi kuona kuwa kuna mtu amemtambua, wale watu walikuwa wamekaa naye pale hawakuweko wanamjua huyu ni nani. Nikawaambia 'Ninyi hammwelewimjui Sal Davis?'
Mimi nili fanya mzaha kidogo, nikawa nilipomwona nikazikumbuka zile nyimbo alizokuwa anaimba na mimi nilikuwa naimba nikiwa mdogo... 'Makini, makini...' mwenyewe anachukua: 'Makini ya kini...', ingine 'Mama, it is my system men...' mwenyewe anachukua: 'It's my system men, it's my... in the many system eyes, mama this menu is crazy...'
Wale watu wote pale walishangaa, 'Mwalimu na wewe unajua kuimba?' Nikasema mimi naimba huyu, sasa Sal Davis mwenyewe kaimba pale.
Sasa tulipoachana pale mimi nikasema, 'This is a big story.' Mimi nikaandika makala, nikaipeleka The EastAfrican.
Wale wakaoona mimi na mwadithia Sal Davis kupitia maisha yangu. Aliyejitokeza anaitwa James Odindo, akasema 'Mwalimu Ndowah, badilisha hii makala. Wewe utapata publicity kuhusu sisi, free publicity. Tunataka utuandikie kuhusu Sal Davis.'
Kwa hiyo mimi nikaiandika tena ile makala na ikachapwa kwenye gazeti. Ilikuwa miaka ya 2006 ilikuwa.
Ile makala ilipotoka bwana, kwa sababu sasa wale waliokuwa nao udogoni sasa ndio ma-executive katika makampuni. Wana niandikia, 'Mwalimu, Sal Davis yuko wapi huyu?' Nikawaambia 'Sal Davis yuko Dar es Salaam hapa.'
Na mimi ni wapelekee picha za Sal Davis, basi EastAfrican ndio walikuwa wanaenda kwenye kumbukumbu zao, wakatoa picha zake wakaiweka kwenye makala.
Nikamwambia 'Sal Davis bwana, wewe ni mtu mkubwa bwana.' Nikamshawishi ndio nikaandika... tukaandika kitabu chake.
Laini katika nacho karibu miaka... kama 15 Sal Davis kwanza kuchapwa, unajua kwetu huku. Sasa siku moja nikamwonyesha publisher mmoja, akaniambia 'Mwalimu, hii bwana this is a gold mine bwana. Mimi nitachapa hii na nitachapa na Amazon.'
Kwa hiyo tumemaliza ile kazi yote. Tulikusudia hii kitabu foreword aandike Ali Mazrui, kwa sababu Sal Davis alipelekwa akiwa na umri wa miaka 15 alipelekwa Uingereza Manchester akafanye 'A' Level akafanye sheria. Siku hiyo akaingia kwenye muziki. Na aliyempokea ni Professor Ali Mazrui ambaye ni katika familia moja.
Nikamwambia 'Sal, hiki kitabu Mazrui atuandikie foreword.' Na mimi Mazrui kwa bahati nzuri tunafahamiana. Bahati mbaya Mazrui amefariki... sasa ndio tukamtafuta rafiki yake mmoja amerejea bwawani kuwa BBC, ndiye aliyempokea Sal Davis alipompokea Mazrui BBC pale.
Anyway, sasa ndio tunasubiri foreword ichapwe, nadhani inaweza kuchukua mwezi hivi utakiona mtandaoni... Sal Davis!"