Production costs za viwanda Tanzania...! tujadili

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,702
2,000
Je, Production costs katika viwanda hapa Tanzania zinatoa ushindani katika soko Africa Mashariki?

Je, bidhaa za Tanzania zinauzika Kenya au Uganda?

Mfano, Mafuta ya kupikia ya Sunola ya Singida Lita 3 Tanzania ni 13000 na Fresh Palm Oil ya Kenya ni 13500.

Tanzania kuelekea nchi ya viwanda inawezekana kwa gharama za Umeme hizi na utitiri wa Kodi?
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,965
2,000
Ni rahisi sana kufanya Biashara ya kuleta bidhaa kutoka nje kuliko kuanzisha kiwanda hapa Tanzania.
Tatizo kubwa ni Gharama za uendeshaji wa viwanda hapa Tanzania kuwa KUBWA, KUYUMBAYUMBA KWA SOKO, KODI, USUMBUFU, NISHATI ISIYOTABIRIKA na USHINDANI WA KIMAGUMASHI.

Biashara pekee ambayo ni rahisi kuanzishia kiwanda hapa Tanzania ni VINYWAJI.
 
Asante kwa kutoa maoni..

Nashangaa watanzania wengi wanafanya biashara kwa mitaji mikubwa sana....wanaleta bidhaa nyingi sana

najiuliza, mtu mwenye mtaji mkubwa kama huu, hawezi kujenga kiwanda japo cha Toothpick tu?

Viberiti tuna agiza - Indonesia

Hata vijiko na uma tunaagiza

Sufuria tunaagiza India

Mafuta ya kujipaka na Lotion - kuna bidhaa nyingi sana za Uganda na Congo

Tanzania Private Sector Foundation na TBNC wanasemaje kuhusu hili

Serikali inatakiwa kubadili sera haraka na kuwezesha viwanda vya ndani kupata umeme wa bei nafuu
 
Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
22,405
2,000
ila mafuta ya Alizeti pure ni 13500 kutoka kiwandani kwa Lita 5.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom