Producer Man Water apewe heshima aisee

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,848
2,000
Mimi sio mpenzi sana wa miziki ya Bongo Flava ya siku hizi kwa sababu beat zake asilimia 90 zimetengenezwa kwa kompyuta.

Kipindi nasoma Secondary School tulikuwa na music lessons. Tulifunzwa kusoma music notes na kucheza instruments kama recorder, guitar na keyboard.

Twende kwenye mada sasa. Leo mdogo wangu wa kike kacheza muziki wa Malkia Karen (mtoto wa Gardner Habash) uitwao “tutoke”. Beat ya hii nyimbo imenikosha sana aisee. Instruments zinasikika vizuri sana aisee. Hakuna kuchakachua. Nyimbo nimeicheza siku nzima kwenye gari yangu.

Producer Man Water Mungu akuweke!
 

Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
5,218
2,000
Very true ule wimbo man walter kapiga vizuri sana ala za muziki kila kitu kina sound live aisee ni mapinduzi ya muziki wetu watu waache kutumia fake melodies za computer.
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,116
2,000
Beat ya hii nyimbo imenikosha sana aisee. Instruments zinasikika vizuri sana aisee. Hakuna kuchakachua. Nyimbo nimeicheza siku nzima kwenye gari yangu.
Samahani mkuu rekebisha kidogo hapo kwenye wino mzito.
Sio hii nyimbo badala yake sema huu wimbo.
Sio nyimbo nimeicheza badala yake sema wimbo nimeucheza.

Ukisema nyimbo ipo ktk uwingi, wimbo ni mmoja.

Don't take it too personal.
 
Top Bottom