Miki123
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 289
- 505
Kama unataka kumiliki simu nzuri na yenye uwezo mkubwa basi jambo la kwanza la kuangalia ni processor kwenye ulimwengu wa simu hufahamika kama SoC (System on Chip).
SoC (system on chip) ni processor inayounganisha vitu vyote vinavyounda simu. Processor ya simu ni tofauti na kompyuta katika nyanja zifuatazo.
SoC inaweka RAM, ROM(storage ya mafaili), Modem kwa ajili ya ineternet (wifi, bluetooth nk), Graphic Processing unit (kwa ajili ya video, kuonyesha picha kwenye screen nk), ISP (kuchakata picha iliyopigwa na camera) na CPU yenyewe sehemu moja kwenye kakifaa kadog.
Tembelea hapa kwa ufahamu zaidi
en.wikipedia.org
Kwa mantiki hiyo ukiachagua SoC nzuri basi kwa asilimia kubwa utamiliki simu nzuri kiuwezo kuanzia inteaneti ya kasi, picha nzuri na video nzuri, ukaaji wa chaji wa muda mrefu na uwezo wa kufungua app kubwa kubwa bila kustack.
Hizi hapa ni SoC bora za simu kwa mwaka huu tangu 2021 .
Ubora wa SoC umeegemea kwenye uwezo wa core moja kwa sababu apps nyingi hazitumii core 8. Na tool iliyotumika ni geekbench
1. Apple Bionic A14
Hii ni processor iliyobuniwa na kampuni ya apple na kutengenezwa na kampuni ya TSMC ya Taiwan.
Imetumika kwenye simu za iphone 12, iphone 12 Mini, iphone 12 pro max na iphone 12 pro.
Apple Bionic A14 imezipita SoC nyingine kwa kuwa uwezo wake kwenye single core(yaani processor moja kati ya 6) ni mkubwa.
Kiwastani soc ya apple inaenda mpaka points 1593 kwenye tools ya Geekbench 5.1
Simu za iphone zenye A14 SoC mfano wa iphone 12 pro max bei inazidi TSH 2,300,000
2. Snapdragon 888
Snapdragon 888 ni ya pili. Ni SoC iliyobuniwa na kampuni ya QualComm ya marekani na kutengenezwa na SAMSUNG ELECTRONIC ya Korea Kusini.
SoC hii inazipa nguvu simu za android ambazo ni
i. Samsung galaxy S21 series USA
ii. Xiaomi mi 11
iii. Asus zenfone 8
iv. Vivo X60 Pro plus
v. Asus Rog Phone 5
vi. OnePLus 9
vii. Oppo find x3 pro
viii. Sony experia 1 III
Hii processor inatumika kwenye highend hivyo bei za simu zenye snapdragon 888 zimechangamka.
Xiaomi mi 11 kwa mfano ni Tsh 1,950,000/= hii inaweza kuwa ni nafuu kati ya simu zinginine za sd 888.
Sd 888 kwenye tool ya geekbench 5.1 inaenda mpaka point 1125.5 tofauti ya point 300 na Apple Bion A14.
3. Samsung exynos 2100 5G
Hii ni SoC iliyobuniwa na Samsung electroni na kutengenezwa na SAMSUNG Electronic ya korea kusini.
Kitu cha kushangaza ni kuwa samsung anatengeza processor za QualComm lakini ubora wa exynos upo nyuma ya Snapdragon.
Hii ni chip ambayo samsung wamejatahidi sana.
SoC hii utaikuta kwenye simu ya Samsung galaxy S21.
Ikumbukwe Samsung series zinazouzwa USA na China hutumia Chip iliyoshika nafasi ya pili SD 888 wakati sehemu zingine duniani hutumia Samsung exynos 2100 5G
Kwenye geekbench 5.1 uwezo wa exynos 2100 unaenda mpaka points 1100
Bei ya samsung s21 ultra yenye exynos 2100 ni karibu na TSH 2,015,000 ni sawa na ile yenye sd 888.
Utachagua ipi kati ya matoleo haya mawili?
4. Snapdragon 865
Snapdragon wanaingiza SoC ya pili kwenye list.
Snapdragon 865 imebuniwa na kampuni ya QualComm ya Marekani kama kawaida na kutengenezwa na TSMC ya Taiwan.
Simu zinazotumia sd 865 ni nyingi ila baadhi ya hizo ni Samsung galaxy s20 series USA, xiomi mi 10, realme x50, sony xperia 1 II, oppo find x2.
Unaweza zipata simu zingine za sd 865 hapa
Uwezo wa hii soc kwenye geekbench 5.1 unafikia point 910.
List ya simu ulizoziona bei zake zinahitaji uvumilivu kutokana na aina ya processor yenyewe.
Mfano oppo find x2 bei yake ni TSH 2,033,359.58
5. Snapdragon 870 5g
Snapdragon 870 imebuniwa na Qualcomm ya USA na kutengenezwa na TSMC ya Taiwan (Kuna haja ya kuizungumzia taiwan upande wa Semiconductor)
Ni simu ya tatu kwenye list kutoka mabingwa wa SoC Qualcomm.
Baadhi ya simu zinazotumia hii SoC ni xiomi mi 11x, iqoo 7, vivo x60 na OnePlus 9R
Kwa mujibu wa geekbench 5.1 uwezo sd 870 unafikia point 985
Simu zenye hii SoC pia bei yake ni kubwa kama ilivyo soc zilizotangulia.
Mfano oneplus 9r inauzwa zaidi ya TSH 1,249,693.06
6. Samsung exynos 990
Exynos 990 imebuniwa na Samsung na kutengezwa na SAMSUNG ELECTRONIC wenyewe.
Simu zinazotumia Samsung exynos ni Samsung galaxy S20 series zote za nje ya USA na China.
Score ya hii chip kwenye geekbench ni 940 point
Bai samsung s20 kipindi imetoka ni TSH 2,400,000
7. Hisilicon kilin 990 5g
Kilin 990 imebuniwa na kampuni ya Huawei ya China na kutengenezwa na TSMC ya Taiwan.
Chip hii inazipa nguvu simu za huawei mate 30 5g na huawei mate 30 5g pro.
Kwa mujibu wa geekbench 5.1 tool, Huawei kilin 990 kiuwezo inafikia point 772.5
Bei ya simu inayoumia kilin 990 5g ambayo ni Huawei mate 30 5g ni TSH 1,833,741.98
8. Hisilicon kilin 990
Hii ni kilin 990 toleo la mwanzo lenye 4g.
Imebuniwa na huawei ya china na kutengenezwa TSMC ya Taiwan
Simu zenye hisilicon 990 ni huawei mate 30 na huawei mate 30 pro
Kiuwezo, Kilin 990 haina tofauti sana na kilin 990 5g.
Kwani geekbench inaipa point 770 kilin 990.
9. Mediatek dimensity 1000+
Matoleo ya MediaTek dimensity SoC bora za mediatek tangu kuanzishwa.
Processor imebuniwa na kampuni ya Mediatek ya Taiwan na kutengenezwa na kampuni ya TSMC ya Taiwan pia.
Simu zinazotumia dimensity 1000+ ni nyingi ila baadhi ya hizo ni Realme x7 pro, Oppo reno5 pro, Vivo iqoo z1, xiaomi redmi k30.
Kwenye geekbench 5.1 dimensity 1000+ ina point 796
Kama ilivyo ya simu za mediatek bei zinavumilika.
Kwa mfano vivo iqoo z1 bei yake ni TSH 927,416
10. Qualcomm Snapdragon 860
Snapdragon 860 imebuniwa na Qualcomm ya USA na kutengenezwa na TSMC ya Taiwan
Baadhi ya simu zenye sd 860 ni Xiaomi poco x3 pro
Kiuwezo sd 860 kwenye geekbench 5.1 inafikia point 728
Na bei simu zenye hii processor zinavumilika kabisa, poco x3 pro kwa mfano ni TSH 507,760.26
Mambo ya msing.
Tool moja haitoshi kuweza kukuelezea ubora wa processor. Angalia tools zingine pia kama antutu, 3d mark nk.
Karibu processor zote bora zimetengenezwa Taiwan na kamapuni ya Taiwan Semiconductor Manufacturing Company (TSMC)
Kampuni nyingi kwa sasa wana-design tu utengenezaji unafanywa na kampuni nyingine.
Nchi za asia zimeteka kwenye hii sekta kwani 75% ya chip hufanyika huko huku TSMC ya taiwan ikitawala kwa 50%
Semiconductor inahitaji high tech na ni gharama kuwa kiwanda cha chip.

System on a chip - Wikipedia