Mzee wa SUP, mimi nipo na pia nakiri kuwa wengi wetu mnanijua kama pro EL, ni ukweli kabisa, ila ule upro EL wangu was only ment for great thinkers.Only those who can read in between the lines ndio walinielewa!.
Wakati wa Arumeru, niliside na Sioi kwa vile niliamini Watanzania ni wale wale juzi jana na leo, hivyo baada tuu ya kupitisha, nikasema kwa uhakika, uchaguzi umeisha kilichobakia ni kukamilisha tuu taratibu!.
Kilichotokea sote tumekiona, kumbe Watanzania wa sasa, sio wale wale wa juzi na jana, hawa wa leo wameamka, sio watu wa kupelekwa pelekwa tuu kwa t-shirt, kofia na shibe ya siku moja!. Watanzania wa sasa sio tena bendera fuata upepo!. Hivyo baada ya uchaguzi ule nilikuja na kukubali matokeo na nikasema bayana kumbe mabadiliko yanawezekana hata bila CCM kumsimamisha EL. The wind of change is sweeping accross Tanzania, hivyo 2015, hata CCM ikimsimamisha the best of the best, down the drain, it will go!.
Wakunielewa wamenielewa, msio elewa endeleeni kuelewa hivyo hivyo mnavyoielewa kwa kadri ya uelewa ambao kila mmoja wetu amejaliwa. Jf ni yetu sote, the great mind, the ordinary and the simple mind alike.
Asante.
Pasco