Pro kanumba naomba msaada wenu

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Baada ya Kifo cha huyu Kijana watu wengi huku wakipewa support kubwa na vyombo mbali mbali vya habari pamoja na Ndugu Jakaya Kikwete wameibuka na maelezo kwamba huyu Jamaa ameshiriki kwa kiwango kikubwa katika kuinua Tasnia ya Filamu nchini na maelezo mengine mengi sana kama kuitangaza Tanzania Kimataifa n.k

Mimi naomba msaada kwenye mambo yafuatayo.

1.Kwamba ameitangaza Tanzania, Je. Ni Kazi Gani ya Kanumba iliyobeba picha halisi ama ya Maisha kwa ujumla au mila na desturi za jamii yoyote ya kitanzania.

2. Kwamba ametoa mchango Mkubwa, Je. Ni Mchango gani ambao unabeba maudhui ya Kitaifa au Sekta ya Filamu?

3. Na ni kazi gani ya Kanumba ambayo imebeba ujumbe wenye msingi wa kujenga Jamii iliyostaharabika na kusimamia Misingi imara ya kifamilia,kijamii,kibiashara,kidini n.k

Ipi??

Asanteni.
 
Ngoja tuwasubiri, wapo wengi tu watatusaidia, inawezekana wengine hatujaziona movie zake halisi, nachojua mimi movie zake zimejamaa maisha ya kusadikika sadika sana kiasi ambacho huwezi hata kusema kwamba ni kioo cha Jamii, inawezekana sijaziona hizo zinazosemwa na wengi.
 
Baada ya Kifo cha huyu Kijana watu wengi huku wakipewa support kubwa na vyombo mbali mbali vya habari pamoja na Ndugu Jakaya Kikwete wameibuka na maelezo kwamba huyu Jamaa ameshiriki kwa kiwango kikubwa katika kuinua Tasnia ya Filamu nchini na maelezo mengine mengi sana kama kuitangaza Tanzania Kimataifa n.k

Mimi naomba msaada kwenye mambo yafuatayo.

1.Kwamba ameitangaza Tanzania, Je. Ni Kazi Gani ya Kanumba iliyobeba picha halisi ama ya Maisha kwa ujumla au mila na desturi za jamii yoyote ya kitanzania.

2. Kwamba ametoa mchango Mkubwa, Je. Ni Mchango gani ambao unabeba maudhui ya Kitaifa au Sekta ya Filamu?

3. Na ni kazi gani ya Kanumba ambayo imebeba ujumbe wenye msingi wa kujenga Jamii iliyostaharabika na kusimamia Misingi imara ya kifamilia,kijamii,kibiashara,kidini n.k
Ipi??

Asanteni.
Angalia sinema yake ya mwisho kabla ya kifo inayoitwa KIJIJI CHA TAMBUA HAKI utaona na kushuhudia Kanumba alivyoigiza kutoa mafunzo ya dhana ya kupinga uonevu katika jamii inayoakisi hali halisi ya sasa ya Kitanzania.
Katika filamu zote za huyu jamaa, hii ndiyo imekuwa na Utanzania zaidi, na huenda wako sahihi waliosema kuwa UKIONA UTAMU UNAZIDI UJUE UMEKARIBIA MWISHO!
 
Jamani au mmesahau kama huyu jamaa alikua muigizaji? maisha ya kusadikika ndio kuigiza kwenyewe.
 
Angalia sinema yake ya mwisho kabla ya kifo inayoitwa KIJIJI CHA TAMBUA HAKI utaona na kushuhudia Kanumba alivyoigiza kutoa mafunzo ya dhana ya kupinga uonevu katika jamii inayoakisi hali halisi ya sasa ya Kitanzania.
Katika filamu zote za huyu jamaa, hii ndiyo imekuwa na Utanzania zaidi, na huenda wako sahihi waliosema kuwa UKIONA UTAMU UNAZIDI UJUE UMEKARIBIA MWISHO!

Nitaitafuta, PK nitakuwa nimekosea kusema kwamba misifa yote wanayompa ni misifa ya uongo, sababu angalau Filamu yake hata moja ingekuwa imemuwezesha kupata internationally recongnized Filimu Awards tungeweza kusema nyota imezimika ghafla, ila kwa viwango vyake ninapata wasiwasi mkubwa sana na vyombo vyetu vya habari.
 
Serikali yoyote duniani ambayo haina pupularity kwa wananchi wake hutumia njia kama hizi kurudisha popularity .Mara nyingi huwa ni wrong move kwani hushauriwa na watu wasio na maono na kutokusoma alama za akati.

Tumeona maprofesa wanafariki hakuna publicity kama hii.

R. I. P Kanumba
 
tuache kukariri...umaarufu wa mtu ni kitu kinachokuja naturally, ima kutokana na kazi yake, madaraka au fani yake!..kwa vyovyote usemavyo Kanumba alikuwa mtu maarufu pengine kuliko wacheza sinema wote, wacheza mpira na baadhi ya wanasiasa wa nchi hii!..Kutokana na umaarufu huo Serikali lazima kwa namna yeyote iguswe na tukio hilo!..kwa sababu serikali zote Duniani zinaongozwa na wanadamu!..Sioni kwa nini tunalazimisha kuukata ukweli ilhali sebule zetu karibu raia wengi zimeja DVD,VCD na pengine VHS za Muigizaji huyu Nguli SCK!..Pumzika braza kazi uliyoifanya imeonekana na Mwenyezi Mungu ameona kuwa uliwapendeza Wanadamu wenzio.
 
Mchango wanaoutoa wasanii wa kibongo ni kuamasisha watoto kutoenda shule na kujishughuliza na uimbaji na uigizaji huku wakitelekeza masomo wakiwa na umri ndogo, baadaye baada ya popurality watumie mwanya huo kugombea nafasi mbali mbali kwa kutegemea mvuto walio nao, kwa maana hiyo tutazaliwa vilaza wengi kwani vilaza hao hawatatengeneza programm yoyote yenye maendeleo kwani shule hakuna, vilaza hawa hawawezi kwenda kwenye internation forum kujadili uchumi au kujifunza jinsi ya kundeleza nchi yao. Mchango mwingine ni kuhusudisha maisha ya starehe sana na ushawishi kwa vijana kuingia katika uaribifu huo, yaani miziki, u-cd, utovu wa nizamu kama vibinti kutoroka na kudhulia matamasha.
Mgano tumchukue dogo janja wa Arusha, unamkuta baa, zikirushwa chupa mamaye ataelezea nini kwa jamii, eti kisa usanii, jamani turudi shule usanii uwa unaisha kwa sekunde ukifilisika mawazo, lakini elimu uwa haifilisiki.
 
Ah wapi kanumba alikua maarufu kama mwigizaji tu. Hakua na jipya kwa Taifa hili. Yale matangazo uliyoyaona ni mediaa zetu hupenda habari za burebure wakatio BBC wanaripoti watoto lukuki wa mitaani na ajira kwa watoto wao wamekaa kusubiri habari zisizokua na tija kwa taifa hili! JF waliposema sana TBC wakafunga Tuamke
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom