Prison Break 2005 Ni series ya kwanza kwa baadhi ya watazamaji wengi, kwa maneno rahisi ni series iliyowavunja u virgin wa kuangalia series hivyo itabaki kuwa pendwa kwa baadhi ya watu hata useme nini hawatakuelewa. Story line ni nzuri sana, uhusika umekaa mahala pake, licha ya kuwa kipindi kile hakukua na teknolojia kubwa kama sasa waliweza kuiweka vyema ikapendeza. . (BTW nairudia sasa kwa mara ya pili tangu niione mwaka 2006). Tukija Upande wa Lacasa De Papel,series imeundwa ikaundika, uhusika umekua mzuri, story line pia njema na tumeona teknolojia kubwa kidogo ukilinganisha na prison break seasons za mwanzo. Zote Mbili zime base katika mandhari moja kwa muda ambayo haichoshi kuitazama, Prison Break Gerezani sana na Lacasa De Papel in the royal mint.
NASIMAMA NA PRISON BREAK kwa sababu licha ya kuwa na teknolojia ndogo kwa wakati ule waliweza kutengeneza kitu bora ambacho unaweza kulinganisha na series zilizotengenezwa wakati huu.