Prison Break kurejea kivingine

Prison Break kurejea kivingine

Series ya hovyo sana, yaani mkamatwe, mtoroke, then makamatwe tena na wote wale wale, huo ni ufala.
Prison huwezi fananisha na series yeyote... Angalia ukiwa umetulia vinginevyo unaweza kuangalia mwanzo mpaka mwisho lakini usijue nini. Kuna kitu kinaitwa Company kama hutakijua hiki ni nini au hawa ni wakina nani na wanataka nini, prison break kwako itakuwa ni mchezo wakuigiza
 
Hii taarifa sijui hao bongo5 wameitoa kwenye source gani ila hakuna PRISON BREAK nyingine itakuja kutoka maproducer walishagoma kabisa kuendelea na hiyo kitu
 
Prison Break kurudi bila Michael Scofield na Lincoln Burrows.

Kulingana na Radio Times, sio Dominic Purcell wala Wentworth Miller wanaotarajiwa kurejea.

Mfululizo huu unaripotiwa kuandikwa na kutayarishwa na Elgin James wa Mayans MC, huku mtayarishaji wa Prison Break Paul Scheuring akifanya kama mtayarishaji mkuu.

Ikumbukwe kuwa The Original Prison Break iliigizwa na Wentworth Miller kama Michael Scofield na Dominic Purcell kama kaka Michael Scofield na Lincoln Burrows, ambao walipanga mpango wa kumtoa Burrows gerezani baada ya kushtakiwa kimakosa kwa uhalifu uliomfanya ahukumiwe kunyongwa. Kipindi hicho kiliendeshwa kwa misimu minne kati ya 2005 na 2009, baadaye kikarudi kwa sinema ya TV ya 2009 Prison Break

Ingawa bado ipo katika maandalizi ya mwanzo, wakati wa kuzinduliowa bado haujawekwa wazi wakielezwa kutafuta namna ya kuifanya wakitafuta waigizaji wengine watakaovaa uhusika wa Michael Scofield na Lincoln Burrows.

Kufikia sasa, maelezo yoyote kuhusu yaliyomo kwenye onyesho jipya la Prison Break hayajatolewa na wenngi wanajiuliza kama itaendana na ile ya mwanzo au laah, Hata hivyo, inaonekana kuwa wanajaribu kutafuta muunganiko wa waigizaji wapya huku wakiepuka makosa ya kipindi kifupi cha Prison Break msimu wa 5 maana pia wakati wa nyuma ni tofauti na wakati wa sasa, lakini pia wengi wanaamini Bila Michael na Lincoln onyesho hilo litaonekana la tofauti na hunenda lisivutie watu wengi, ingawa pia bado linaweza kufanyika bila wao.

Unatamani Prison Break irudi bila Michael Scofield, Lincoln Burrows, Sarah Wayne, T-Bag na wengine?? na Je nani alikuwa anakuvutia zaidi?

Chanzo: Bongo5
Uzushi huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom