mbweni nunueni wenyewe, lakini sisi tunaofanyakazi katikati ya jiji tunahitaji viwanja maeneo ya magomeni, kinondoni, ilala at least mpaka mwenge hivi na ubungo.
Sababu iko wazi wakuu, khali ya foleni hapa mjini ni mbaya sana, toka mbweni mpaka city centre ni 30 km combine with road traffic lazima uwe kichaa. Jamaa wanaokaa huko wananiambia kwamba ili ufike job (city centre) mapema inabidi uchomoke saa 11 kamili asubuhi. Jioni inabidi uzugezuge ofisini au bar ili foleni ipungue na uondoke hapa city centre saa 3 usiku na kufika home (mbweni/bunju) saa 4:30 usiku.
Sasa wadu hamuoni kwamba kama una familia, utaishia kukutana nao jumapili tu!! Achilia mbali kubenjuka na wife ambao wote mtakuwa mnarudi mmechoka mbaya. Hamtokuwa na muda mzuri wa kujua maendeleo ya watoto wenu na mambo mengine. Ukiwa na house girl/boy mapepe, kama kawa he/she will capitalize the situation kwa kugeuza nyumbani kwako sehemu ya kuangalizia picha chafu na ujinga mwengine kama wanenu ni wadogo bado!!
Labda wadau Mkiniconvince vizuri, naweza kununua plot mitaa hiyo!!
We need fly overs in Dar especially at Ubungo, tazara, mwenge, moroco etc to ease road traffic!