Pride ndiyo mkombozi wa wajasiriamali wadogo

HAZOLE

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,551
708
Jamani nimesoma brochures za pride na jinsi wanavyotoa mikopo yao nikaona ni safi sana.
Wanaanza kukopesha tsh.200,000/= unalipa tsh.11,000/= kila wiki kwa wiki 25 (11,000 *25=275,000/=). Ukimaliza deni unakopeshwa laki tano (14,500/= kwa wiki kwa wiki 25 marejesho) ukimaliza unakopeshwa 1 million, 2 million and so forth......up to ten million.
Si lazima urejeshe kwa wiki 25, waweza rejesha hata 2 weeks tangu ukopeshwe na unahamia next level........
Nadhani hii itasaidia wa tz wengi wanaotaka kuanza na small loans with soft terms and conditions maana dhamana yao ni kutambulishwa na watu watano ambao tayari wamekopa hapo
guys mpooooo?????
 
hiyo Riba mbona haina ukombozi wowote.Si bora utafute saccos yeyote ukope maana hiyo riba ni kubwa sana.
 
kibongobongo huwa tunaangalia kiasi gani tunarudisha na sio riba kiasi gani ndo maana watz wengi wanakimbilia huko mkuu...
 
La msingi - popot unapokopa uwe unakopa kwa ajili ya biashara itakayokuwezesha kulipa kikamilifu na kubaki na ziada. vinginevyo usikope.
 
Jamani nimesoma brochures za pride na jinsi wanavyotoa mikopo yao nikaona ni safi sana.
Wanaanza kukopesha tsh.200,000/= unalipa tsh.11,000/= kila wiki kwa wiki 25 (11,000 *25=275,000/=). Ukimaliza deni unakopeshwa laki tano (14,500/= kwa wiki kwa wiki 25 marejesho) ukimaliza unakopeshwa 1 million, 2 million and so forth......up to ten million.
Si lazima urejeshe kwa wiki 25, waweza rejesha hata 2 weeks tangu ukopeshwe na unahamia next level........
Nadhani hii itasaidia wa tz wengi wanaotaka kuanza na small loans with soft terms and conditions maana dhamana yao ni kutambulishwa na watu watano ambao tayari wamekopa hapo
guys mpooooo?????

Ndugu hao watu watano utawapata wapi? Na wengi hawakubali mtu wasie mjua kufanya naye ushirika. Kazi ya kutafuta watu watano ni ngumu sana hasa kwa Watz wa kawaida.
 
Wengi wetu tunanunua samani za kichina ili tuwakoge majirani na wageni sebuleni. Hapo ndipo huwa kilio na kusaga meno. Elimu zaidi inahitajika kwa wadau!
 
kwa maoni yangu siyo tu kununua bidhaa za kichina lakini watz tuliowengi elimu ya ujasiriamali hatunayo wala hatutaki kukiri hilo na kuondoa kasoro hizo mfano Wanawake wengi japo si wote wanachukua mikopo midogomidogo hiyo bila kuwa na mipango iliyoandaliwa kwa kina na ambayo imezingatia kiwango cha hasara na faida ya utekelezaji wa mradi husika in financial implecations (Project Appraisal). Nawashauri wale wote wanaokopa wahahakikishe wanakopa kwa malengo yaliyothabiti. Watanzania pia tuache ulimbukeni wa kununua bidhaa kutoka nje na kudhoofisha uchumi wa nchi yetu maana tunasaidia kujenga uchumi wa wenzetu na sisi kubaki hoehae. je huu si ushamba kuwa bidhaa za nje ni bora zaidi kuliko za watanzania, eg club za michezo za nje ni bora zaidi, meza maofisini zinazotoka nje ni bora kuliko zetu. huu ni ushamba wa kiuchumi. tuondokane na ukoloni mamboleo watanzania. ni maoni yangu changieni wadau
 
wengi wetu tunanunua samani za kichina ili tuwakoge majirani na wageni sebuleni. Hapo ndipo huwa kilio na kusaga meno. Elimu zaidi inahitajika kwa wadau!

mkuu hapo umenena, watu hukopa ili kuwafurahisha ndugu, jamaa na marafiki.ndo zao watu wanakopa
- kununua sofa za kichina
- flat screen
- meza ya vyombo na ya nguo
- frdge na kazalika
na hivi vyote ni ili kuwafurahisha ndugu jamaa marafiki na majirani
 
na harusi mkuu..... yaani hapa bongo,harusi/kitchen party/arobaini/jando etc zinathaminiwa kuliko mambo muhimu kama kusomesha, kusave nk..... we need a change
 
kibongobongo huwa tunaangalia kiasi gani tunarudisha na sio riba kiasi gani ndo maana watz wengi wanakimbilia huko mkuu...
kijana umezungumza from experience viewpoint...ndomaana hata DECI ilikamata wa tz wengi
 
fikiria kabla ya kutenda.
Angalia mchanganuo ufuatao;
200000/25=8000/=
11000-8000=3000/=
3000/8000*100=37.5%
8000*25*37.5%=75000/=
11000*25=275000/=

jamani hapa riba ni zaidi ya 37.5% kwa wiki huu ni zaidi yawizi wa macho.

yaani kopa 8000=kwa wiki halafu lipa 11000/= kwa wiki.
 
kijana hauogi lakini unamahesabu sana.
From that description, naona wanaiba sana hawa PRIDE. duh ukombozi hamna hapo, jamani kweli africa for africa!!!
 
Pride inahusishwa na idd simba,ndo haohao wanaoiba pesa za walalahoi na kuwakopesha tena,hhahahahaaa,
 
Ukishidwa kulipa wanachukua kila kitu hata unga wa ugali wa watoto, walimshusha mama mmoja na mtoto mchanga kitandani wakamlaza sakafuni wakachukua kitanda, hawana huruma wala utu, mama alichukua mkopo baba akachukua akatambaa na hela zote.
 
Back
Top Bottom