Pride Comes Before the Fall: CHADEMA inabidi wajipange upya

daaaah kwani watu mnatumia kiungo gani kufikiri chadema na ccm nani mwenye pride(ego)?
 
Sijakuelewa una maana gani kwamba hamna kiongozi aliyejitokeza kumtetea TAL, viongozi wote wanaogopa kukamatwa, hawatadhubutu kuja hadharani kuonesha support kwa TAL.

Ila hamna kesi ya kumtia hatiani. Wanasheria wengi tu na Civil Society na Mataifa mengi yapo Nyuma yake. Vivyo hivyo kwa Mikutano ya Mkoani hali ni hiyo hiyo, watu wanaogopa kupigwa Mabomu ya Machozi na Maudhi menginne. Sio kwamba CDM imepoteza umaarufu.

Tofauti na Mawazo yako. Vitisho vya vikipungua watu watafurika Mikutano sio ya CDM tu bali na Vyama vinginne vya upinzani.
 
Mbowe alipotoka rumande alikaa na Samia wakakubaliana mazungumzo yatakayo wapeleka kwenye maridhiano. Mazungumzo hayo yalifanikisha yafuatayo:
1. Viongozi waliokuwa wakimbizi waliweza kurudi nchini na kuendelea na shughuli za siasa. Baadhi yao ndio sasa wanaongoza CDM. Inawezekana bila mazungumzo ya maridhiano wangekuwa bado wakimbizi hivyo ingekuwa vigumu kushiriki katika uchaguzi.
2. Zuio la mikutano ya hadhara na mingine ya kisiasa likaondolewa. Lingekuwa bado lipo, hii mikutano ya NRNE isingefanikiwa.
3. Wanachama wa Chadema waliokuwa ndani waliachiwa na kesi zao kufutwa. Hali hii imeongeza imani kwa CDM kuwa inapigania wanachama wake.
Kitu kingine ni kuwa CDM iliweza kukubali kupokea ruzuku yao ambayo iliwawezesha kununua jengo lao la Makao Makuu na kukipunguzia mzigo wa gharama za uendeshaji.
Naam, waliendelea kufanyiwa dhulma lakini walikuwa katika nafasi nzuri ya kukabiliana nazo kwa sababu kwa kiasi kikubwa CDM ilikuwa imeungana.
Uongozi mpya umesema wazi kuwa strategy ya Mbowe haina tija na kinachohitajika ni approach ambayo ni more confrontational. Approach ambayo ni ya ninja ninja. Na hakuna kubembelezans. Ams uko nasi au wewe ni adui yetu. Mafanikio ya approach hiyo mpaka sasa ni:
1. Kumekuwa na muitiko mkubwa kutoka kwa wananchi kuhusiana na wito wao wa NRNE.
2. Wanachama na watu wengine wa kawaida wameonyesha moyo wa kuchangia mfuko wa chama.
3. Dunia nzima imetambua uwepo wa CDM.

Lakini pamoja na hayo mafanikio, yafuatayo yametokea:
1. CDM imeondolewa katika orodha ya vyama vitakavyo shiriki uchaguzi mwaka huu. Kuna uwezekano mdogo sana wa hali hii kubadilika.
2. Mfuasi mkubwa ambae sasa ni mwanachama alishikwa na kuwekwa ndani. Alifutiwa kesi bila presha yeyote kutoka kwa wananchi.
3. Mwenyekiti wa CHADEMA yuko rumande. Ukiondoa juhudi zinazofanywa nje ya nchi na taasisi chache nchini, hamna presha kubwa kutoka kwa wananchi ya kutaka aachiwe.
4. Mwanachama maarufu wa CDM amepotea katika mazingira ya ajabu. Nako pia tunasikia vitisho tu jukwaani na mitandaoni lakini hatuoni presha kubwa ikifanyika on the ground za kuhakikisha yeye na wengine waliopotea kabla wanapatikana. Presha hizo ni maandamano, sit ins, hunger strikes,
5. Chadema imegawanyika, na baadhi ya waliokuwa viongozi na wanachama waandamizi wamejitoa kwenye chama. Matokeo ya hatua hii ajenda kubwa ya chama sasa inaonekana ni kukabiliana na wale wanaodai kuwa ni wasaliti. Matusi, uongo, ghiliba n.k. vimetumika kuwachafua watu ambao wamekitumikia chama chao kwa miaka mingi sana.
6. Uteuzi wa watendaji wakuu wa chama na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu umebatilishwa na Mamlaka husika.

Kutokana na yote haya, nawashauri CDM isiendelee kukaza shingo. Ni wakati wa kuwasikiliza viongozi wao wa zamani ili wakinusuru chama chao. Wanahitaji busara za mtu kama Mbowe.

Najua kuwa itawauma sana lakini uongozi makini unahitaji flexibility ya kuweza kugeuza position of weakness kuwa strength. Lakini nahisi kwa kiasi kikubwa pride yao itawazuia kufanya hivyo.

Amandla...
 
Pumba tupu
 
Acha maduka yaondoke chama kibaki safi.
Kuhusu uchaguzi sio kipaumbele chetu kwa wakati huu ambao kura haziheshimiwi.
Wasimamizi wa uchaguzi kugeuka wapiga kura ili kuisaidia ccm.
Bila mageuzi ya kweli katika mfumo wa uchaguzi, kupiga kura ni ujinga na uwendawazimu
 
Kama ndivyo Lisu alivyo kwa nini chama kilimpatia nafasi ya kugombea urais?
 
Umeandika pumba na siwezi kupoteza muda kuzijibu
Lakini ukazijibu kwa kuandika pumba. Mimi niko tofauti na wewe. Nikiona michango yako haina tija kwangu nakuweka kwenye 'ignore list'. Kwa kufanya hivyo silikoni tena. Ukiona sikujibu ujue kuwa uko kwenye hiyo list.

Amandla...
 
Kama ndivyo Lisu alivyo kwa nini chama kilimpatia nafasi ya kugombea urais?
Hilo swali linapaswa kujibiwa na CDM wenyewe. Labda kwa sababu Lissu ni charismatic sana ana mvuto mkubwa na anaweza kujenga hoja ikaeleweka kirahisi. Aidha, ana ujasiri wa kusema yale ambayo watu wengi wanaogopa kusema.

Wengi tuliamini kuwa hiyo ndio haiba yake hata nje ya majukwaa. Mimi naamini kuwa pamoja na mapungufu yake, kama patakuwa na uchaguzi wa haki na uwazi anaweza kushinda. Lakini akishinda atakuwa autocratic na atalipa kisasi kwa wote ambao anaamini walimkosea.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…