MTAZAMO
Platinum Member
- Feb 8, 2011
- 20,209
- 35,852
Rais Kabila ameingia kwenye mgogoro na Kanisa Katoliki baada ya kuvunja makubaliano ya kutoongeza muhula mwingine kama katiba inavyosema.
Kanisa Katoliki liliamua kuitisha maandamano ya amani kushinikiza takwa hili la kikatiba kuheshimiwa na Rais Kabila amejibu kwa vitendo hatua hiyo kwa kutuma vikosi vya jeshi na Polisi kuvamia makanisa, kukamata mapadre na viongozi wa hayo maandamano, mbaya zaidi mabomu na risasi kutumika kukatisha maisha ya baadhi ya waamini.
Maandamano ya wiki iliyopita yameungwa mkono na Wakristo wa madhehebu mengine na jumuiya za Kiislamu kwa mujibu wa ripoti ya BBC na vyombo vingine vya habari
Nini nafasi ya Kanisa,
Kanisa ndio lililosimamia makubaliano ya kuhakikisha uchaguzi unaitishwa kabla ya 2017. Hivyo kuvunjwa kwa makubaliano hayo ni jambo ambalo lilitegemewa kuleta mzozo dhidi ya Kanisa Katoliki.
Juhudi za maaskofu kumuasa Kabila kuheshimu Katiba zimegonga mwamba na kutokana na udhaifu wa upinzani, Kanisa halikuwa na jinsi zaidi ya kutimiza jukumu lake la kiroho na kimwili dhidi ya ukiukwaji huu wa katiba kwa kuitisha maandamano ya amani.
Kwa mujibu wa news24 hisia kubwa zilitawala kwenye misa pale majina ya watu sita waliokufa kwenye maandamano yalipotajwa kwa marudio mara tatu. Askofu msaidizi Donatien Bafuidinsoni akisema " tumepoteza kaka na dada zetu, tumepata mashujaa, mashujaa wa kweli. Wamemwaga damu zao pamoja na wengine kwaajili ya mabadiliko ya utawala, uhakika wa demokrasia"
Kabila afanye nini,
Tayari ameharibu taswira yake kwa jinsi anavyopambana na waamini wenye misalaba na biblia huku kukiwa na taarifa za vifo.
Pres. Kabila hataweza kuitawala DRC ikatawalika zaidi ya kuzidi kukaribisha uasi utaomweka pabaya zaidi.
Aitishe uchaguzi ambao utasimamiwa na jumuiya za kimataifa. Aombe hifadhi ya kisiasa hadi Rais atakayechaguliwa atakapoweka hali ya usalama sawa.
Hatua yoyote atayochukua kupambana na Kanisa kuanzia sasa itamuweka pabaya mno yeye na familia yake binafsi maana wakongo wanazidi kuungana kinyume chake. Udhibiti wa nchi kwa kutegemea majeshi ya kigeni haujawahi kufanikiwa kama wananchi na jeshi la nchi lipo kinyume chako ( tayari kuna taarifa ya baadhi ya makamanda kuanza kuasi)
Rais Kabila chukua hatua mapema kabla mambo hayajafikia "beyond repair". Kubali majadiliano ya kitaifa na kuitisha uchaguzi kabla "maadui" wengi zaidi kuanza kutumia fursa hiyo kukumaliza.