Presha kupanda

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Habari wana jamvii.....nina shemeji yangu alianza kuongea vitu visivyoeleweka (maluweluwe) ijumaa iliyopita na kulamimika kuwa ana uchovu sana.

Dada yangu (mkewe) alihisi ni gea tu yakukwepa maswali maana alikuwa akimdai pesa ambayo alihaidiwa na huyo mumewe.Hali ya mume iliendelea hivyo ndipo alipomtilia mashaka siku ya jumapili na kumpeleka hospital aga khan.

Alipimwa presha ikaonekana ipo juu 223/118 ikabidi wamlaze na kuendelea na vipimo vingine kama full blood pic,xray ya moyo na ct scan kwa ajili ya kichwa coz alianza kupoteza kumbukumbu na kuongea maluweluwe.

Kipimo cha kichwa kilionesha ameshawahi pata stroke ya ubongo(dada halijui hilo)na kuna stroke nyingine mpya ambayo wanasema ndiyo imemfanya awe hivyo na hawezi rudi katika hali ya kawaida.

Wadau tusaidieni mawazo maana madaktar wametukatisha tamaa....
[MENTION=12367]MziziMkavu, DRMo, @DrRiwa, The Boss, Mimi49 na wengineo wote
 
Last edited by a moderator:
Habari wana jamvii.....nina shemeji yangu alianza kuongea vitu visivyoeleweka (maluweluwe) ijumaa iliyopita na kulamimika kuwa ana uchovu sana.

Dada yangu (mkewe) alihisi ni gea tu yakukwepa maswali maana alikuwa akimdai pesa ambayo alihaidiwa na huyo mumewe.Hali ya mume iliendelea hivyo ndipo alipomtilia mashaka siku ya jumapili na kumpeleka hospital aga khan.

Alipimwa presha ikaonekana ipo juu 223/118 ikabidi wamlaze na kuendelea na vipimo vingine kama full blood pic,xray ya moyo na ct scan kwa ajili ya kichwa coz alianza kupoteza kumbukumbu na kuongea maluweluwe.

Kipimo cha kichwa kilionesha ameshawahi pata stroke ya ubongo(dada halijui hilo)na kuna stroke nyingine mpya ambayo wanasema ndiyo imemfanya awe hivyo na hawezi rudi katika hali ya kawaida.

Wadau tusaidieni mawazo maana madaktar wametukatisha tamaa....
MziziMkavu, DRMo, @DrRiwa, The Boss, Mimi49 na wengineo wote

miss strong!

Upo uwezekano mkubwa akawa na tatizo la figo pia!

kwa kawaida pressure ikipanda sana huwa 'inachoma' figo kwa haraka sana na kusababisha 'stroke' iinayo-pelekea kupoteza kumbu kumbu, kukiambata na kipindi cha kushi tuka shituka sana kwa mgongwa!

Jaribuni kumpima figo zake kama zinafanya kazi vizuri, kazeni buti kweli kweli ugonjwa wa kisuna ndo kwaanzaa unapiga hodi jipangeni kuukabiliana nao!
 
Habari wana jamvii.....nina shemeji yangu alianza kuongea vitu visivyoeleweka (maluweluwe) ijumaa iliyopita na kulamimika kuwa ana uchovu sana.

Dada yangu (mkewe) alihisi ni gea tu yakukwepa maswali maana alikuwa akimdai pesa ambayo alihaidiwa na huyo mumewe.Hali ya mume iliendelea hivyo ndipo alipomtilia mashaka siku ya jumapili na kumpeleka hospital aga khan.

Alipimwa presha ikaonekana ipo juu 223/118 ikabidi wamlaze na kuendelea na vipimo vingine kama full blood pic,xray ya moyo na ct scan kwa ajili ya kichwa coz alianza kupoteza kumbukumbu na kuongea maluweluwe.

Kipimo cha kichwa kilionesha ameshawahi pata stroke ya ubongo(dada halijui hilo)na kuna stroke nyingine mpya ambayo wanasema ndiyo imemfanya awe hivyo na hawezi rudi katika hali ya kawaida.

Wadau tusaidieni mawazo maana madaktar wametukatisha tamaa....
MziziMkavu, DRMo, @DrRiwa, The Boss, Mimi49 na wengineo wote
Pole sana kama ana Ugonjwa wa Maradhi ya Prewsha ya kupanda Dawa ninakupa hii hapa awe anakula kila siku Punje 2 za kitunguu Saumu kila siku asubuhi anapoamka kabla ya kula kitu na mchana ale tena hizo punje 2 za kitunguu saumu na usiku ale tena atapona hayo maradhi ya Presha ya kupanda .

La Kama ana Maradhi ya Kiharusi asile hicho Kitunguu Saumu. Hebu soma hapa chini kuhusu hayo Maradhi ya Kiharusi.


Maradhi ya kiharusi (stroke)


Maana ya Kiharusi



webmd_rm_illustration_of_stroke_causes_.jpg


What Is a Stroke?


Stroke is a medical emergency and a leading cause of death in the U.S. It occurs when a blood vessel in the brain bursts or, more commonly, when a blockage develops. Without treatment, cells in the brain quickly begin to die. The result can be serious disability or death. If a loved one is having stroke symptoms, seek emergency medical attention without delay.





getty_rm_illustration_of_stroke.jpg


Stroke Symptoms


Signs of a stroke may include:



  • Sudden numbness or weakness of the body, especially on one side.
  • Sudden vision changes in one or both eyes, or difficulty swallowing.
  • Sudden, severe headache with unknown cause.
  • Sudden problems with dizziness, walking, or balance.
  • Sudden confusion, difficulty speaking or understanding others.


Call 911 immediately if you notice any of these symptoms.





phototake_rm_photo_of_brain_damage_from_stroke.jpg


Stroke: Time = Brain Damage


Every second counts when seeking treatment for a stroke. When deprived of oxygen, brain cells begin dying within minutes. There are clot-busting drugs that can curb brain damage, but they have


to be used within three hours of the initial stroke symptoms. Once brain tissue has died, the body parts controlled by that area won't work properly. This is why stroke is a top cause of long-term disability.


MARADHI YA KIHARUSI:


Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo na hivyo kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.


Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo na ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24. Muda wa masaa 24 umechukuliwa ili kutofautisha kiharusi na kiharusi cha kukosa oksijeni katika ubongo (ischemia) ambacho hutokea na kudumu kwa muda mfupi yaani (transient ischemic attack).


Kwa kawaida dalili za TIA hupotea na mtu kurudia hali yake ya kawaida ndani ya masaa 24.


Aina za kiharusi



Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea (visababishi vyake). Aina hizo ni



1. Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)


Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.



Aina hii ya kiharusi husababishwa na nini?


Aina hii ya kiharusi husababishwa na


Damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis) au

Kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism)


Kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla kwa mfano shock.

Vena thrombosis


2. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya Ubongo (Haemorrhagic Stroke)


Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu ubongoni (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.


Visababishi vya Kiharusi (kwa ujumla)


Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika


mishipa (thrombosis) hiyo. Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza


kuathirika na tatizo hili ni pamoja na arteri za common carotid na interior carotid arteries, na arteri za vertebral. Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo.


Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgojwa wa sickle cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha Kiharusi.


Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis) huweza


kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.


Upungufu wa usafirishaji damu mwilini (systemic hypoperfusion) - Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa


sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha (Ischaemic Heart Diseases) au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje (pericardial effusion) au kupungua kwa damu mwilini,


kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa. Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.


Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo (Intracerebral hemorrhage).


Dalili za kiharusi



Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa.


Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa ( Cerebellum) itaadhirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake, kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.


Iwapo sehemu ya ubongo wa kati (cerebral cortex) itakuwa imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea,kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, kushindwa kuona vizuri, kuwa


na ukosefu wa kumbukumbu, kuwa na mvurugiko wa mpangilio wakw wa kufikiri, kuchanganyikiwa, na kubadilika kwa mwendo wa harakati za hiari.


Iwapo mgonjwa ataadhirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na


kuona; kulegea kwa misuli ya macho (ptosis); kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande); kupungua uwezo wa


kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja; kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti; mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda.


Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na hisia mtetemo.


Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida


hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.



Vipimo


Mionzi

CT-scan

MRI

PET

SPECT

Vipimo vingine ni;



ECG, ECHOCARDIOGRAM huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo


Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi


Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba.

Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu

Vihatarishi vya kiharusi


Vitu vinavyoweza kumuweka mtu katika hatari ya kupata kiharusi ni pamoja na


Shinikizo la damu lisilothibitiwa

Kisukari

Uvutaji sigara

Unywaji pombe kupita kiasi

Kutofanya mazoezi kabisa

Fetma (obesity)

Kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu

Atrial fibrillation

Matibabu


Matibabu ya kiharusi hutegemea pia aina na visababishi vyake .


1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke)


Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.


2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke)


Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Angalizo: ni hatari kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu


iliyoganda au za kuzuia kuganda maana uhatarisha maisha ya mgonjwa badal ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.


Huduma na Matunzo kwa mgonjwa wa Kiharusi


Mojawapo ya mambo muhimu ya kufanya kwa mgonjwa aliyepata kiharusi ni kumuongoza na kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Hapa uhitaji ushirikiano wa wauguzi,


wataalamu wa viungo, wataalamu wa ushauri wa kazi na daktari. Kuna umuhimu pia wa kuwaelimisha ndugu kuhusu hali ya mgonjwa ili waweze kumsaidia katika matunzo yake nyumbani na kwenye jamii inayomzunguka.


Matarajio (prognosis)


Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao na kuajiriwa. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja.


Ulemavu wa kimwili ni pamoja na


Ulegevu wa misuli

Kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika

Kujikojolea

Kutoona vizuri

Kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku

Vichomi

Vidonda shinikizo

Kukosa hamu ya chakula.

Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama


Mgonjwa kuwa na wasiwasi

Hofu ya mashambulizi, na

Unyongovu.

Jinsi ya kuzuia kiharusi


Zuia au tibu shinikizo la damu

Dhibiti kisukari

Fanya mazoezi

Acha kuvuta sigara

Punguza uzito

Acha kunywa pombe kupita kiasi

Tumia Junior Aspirin

Kula chakula kisichokuwa na mengi na kisicho na chumvi nyingi.

Tumia dawa za kupunguza mafuta mwilini (statins)kwa mfano Simvastatin.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom