Prepaid Legal Services | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prepaid Legal Services

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by payuka, Oct 20, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa wana JF wote,

  Hili ni wazo ambalo nimekuwa nikilifikiria kwa muda mrefu sasa licha ya kwamba professional yangu sio sheria ( in short mi sio lawyer).

  Kwa mtazamo wangu, nchi yetu imefikia mahala ambapo inahitajika law firms and lawyers waangalie namna ya ku-introduce huduma hii ndani ya soko ya tanzania kutokana na ukweli ufuatao:

  1. Watu wengi wamepoteza haki zao pale wanapopatwa na matatizo ambayo yanahitaji msaada wa kisheria kutokana na gharama kubwa ambazo wanasheria wanatoza; mfano: kwenye ubakaji, kubambikiziwa kesi, ukatili wa kijinsia, utapeli unaotokana na bogus contracts n.k
  2. Watu wenye fedha au nyadhifa kubwa serikalini wameweza kutumia pesa pamoja na nguvu zao kuwafanyia maskini wanyonge vile wanavyotaka; mfano mzuri ni Mh. Andrew Chenge, Marehemu Ditopile, Mh. Zombe just kuwataja wachache
  Mimi nafikiria na ninaomba kama kuna mtu ambaye anaweza aka-initiate hiki kitu ambacho operating model yake ni similar na microinsurance policies zainavyo-operate atakuwa kasaidia watanzania wengi mno.

  Kinachotakiwa na ku-design packages mbalimbali ambazo watu watakuwa wana-contribute pesa ndogondogo! na endapo litatokea la kutokea lawyers wanakuwa standby kuanza kazi ya utetezi ( lakini wa Haki).

  Angalizo:
  1. kwa nature ya nchi yetu, elimu ndo swala la msingi before and after introduction of any service/product in the market
  2. Nina shaka na willingness ya watu kwenye contribution, licha ya kwamba unaweza ukatumia njia mbadala kama vile mtu ku-send SMS ambayo atakatwa kiasi fulani cha pesa na wakati huohuo ana-pata points kadhaa za kuingizwa kwenye bahati nasibu ( ndo watanzania wanapenda jamani)
  Kama kunamtu yeyote yuko interested: mcahngo wangu utakuwa ni kwenye kusaidia kuandaa operating model, pamoja na kufanya brainstorming ili kutouch angle mbalimbali.

  Nawakilisha!
   
 2. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu, ubarikiwe. Hii topic nilikua nawaza lakini sikujua namna ya kuiframe ili wakuu watoe michango yao. Bepari mmoja alisema "Kutajirika unahitaji vitu viwili, Muhasibu Mwerevu na Mwanasheria" (by Andrews Carnegie). Nadhani humu wengi wetu hatuna uwezo wa kuwapa kazi hawa jamaa. LAKINI, tunaweza kuwatumia kwa mambo maalum wakati inapobidi. Nahapo ndipo tutapata wenzetu wengi.

  Mimi kawaida ni muhasibu, sijui kama ni mwerevu lakini ntasaidia kufanikisha lengo hili ikiwa mtiririko wa Prepaid Legal utapa michango ya kutosha. Tafadhalini wafanyakazi, wajasirimali, wafanya biashara, wawekezaji, na wanafunzi. This is the real deal if done correctly. Tutadhibiti over charging by using free market tools.

  Naomba tuungane. Itapunguza Wizi, dhuluma, na utapeli. Hivi ndio vitu vinavyoharibu nchi yetu.
  Kwa wale vijana wamjini, itasaidia hata wakivunjiwa vibanda vyao vya kutafutia riziki bila kupewa taarifa. Serikali haiwezi kutufanyia hili, imekwisha ruhusu Free market. Soko Rukhsa!

  Ukweli husemwa, wabongo wanajua kubonga, inapokuja kwenye sheria.
   
 3. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu, nashukuru kwa mchango wako...ninaamini Wadau watajitokeza ili kutoa michango yao namna ya kusaidia hii kitu iwe implemented ndani ya nchi yetu ili kusaidia wale walionyimwa/ wanaonyimwa haki zao kisheria.
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Niishafikiriaga sana hili jambo! Watu wengi sana wamepoteza na wanaendelea kupoteza haki zao na ni kwa sababu ya wachache walio na power au ktk position zao au kifedha, yaani inasikitisha sana kiasi cha kwamba mpaka walala hoi wengi wamekuwa waki give up haki zao ambazo unaona waziwazi wanaonewa lakini wameshakata tamaa na kukubali kuonewa. it is sick!
   
 5. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
Loading...