Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,751
Hali ya shirika la ndege la Precission la Tanzania inaelezwa kuwa 'mbaya' huku shirika la ndege la Kenya(KQ) likihusishwa na matatizo ya sasa ya shirika hilo.
Tayari Precission imeanza kufunga baadhi ya ofisi zake zilizopo nje ya nchi huku ikirudisha baadhi ya ndege zake aina ya Boing ilizokodi kwa ajili ya kuongeza maeneo inakofanyia safari zake.
Raia Mwema limeambiwa kwamba kuna hofu ya ukweli kwamba shirika hilo linaweza kutangaza kupunguza wafanyakazi wake wakati wowote kuanzia Leo.
Miji ambayo tayari Precision imefunga shughuli zake ni Lusaka Lubumbashi na Kinshasa.
Uongozi mbovu wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Alfonce Kioko, raia wa Kenya na kutofanya vizuri kwa shirika hilo wakati wa zoezi lake la kutaka kuuza hisa kwenye soko la Hisa la Dar es salaam ni mambo mawili makubwa yaliyochangia hali ya Precision kwa sasa.
Raia Mwema limepewa tuhuma mbalimbali za kifisadi kumhusu Kioko lakini inazihifadhi kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi badae.
Kioko alikuwa ni Pendekezo la KQ kuongoza Precision ingawa utendaji wake ulionyesha matatizo tangu awali, mwanzilishi na mwenyekiti wa Precision, Michael Shirima alikuwa akimkingia kifua.
Shirima ndiye mwenye hisa nyingi 35% huku KQ ikiwa na 34%.
Wadadisi katika sekta ya Anga nchini wanadai kwamba matatizo haya ya Precision yana mkono wa KQ ambayo inataka kutawala eneo la Afrika mashariki.
Sababu zilizotolewa ni mosi Kioko alikuwa Chaguo lao, Pili kushindwa kwa Precision kupata faida kwenye IPO kulichangiwa na kutopata wateja wengi Kenya na tatu ni hatua ya KQ kuanzisha safari za shirika hilo kati ya Nairobi na Kilimanjaro katika kipindi hiki cha matatizo ya Precision.
Wakati wa IPO, Precision ilitaraji Wakenya na Watanzania wengi wangeshiriki, cha ajabu Mamlaka za Kenya zikachelewesha uuzwaji wa hisa Kenya na waliporuhusu ikawa imechelewa.

na bado
watanzania tutalala wee.....tukiamka kila kitu tumewaachia wageni hasa wakenya
inaelekea woote tumesahau jinsi ile jumuiya ya kwanza ya afrika mashariki ilivyovunjika 1977
elimu elimu elimu ni muhimu sana
Hii precision ni kampuni binafsi......lakini kuhusu hujuma za nchi jirani za kwa biashara za Tanzania, hapo ndio tunaona kuwa na TISS inayowajibika kwa maslahi ya nchi badala ya watu..... precosion ina semekana ni yakina mramba, TISS mko wapi? tena iliwahi kupewa Government Guarantee na kuweza kukopa ulaya......haya kuna suala la General Tyre Ltd, ni yale yale, sasa waweztu TISS wanafanya nini?
Huu ni uongo na upuuzi wa watanzania kila wanapokuwa na matatizo wanajaribu kuwasingizia watu wengine. Mwandishi wa Raia Mwema umekaa ofisini kwa Dar unaandika habari za kimajungu majungu. Hata huko Kenya KQ ina hali mbaya ya kifedha kwa sasa, inakuwaje iiue Precision Air ambako wana hisa na ijiue yenyewe?? Acheni hizo tabia zenu, Lazy but knows it all atitude haitawasaidia waandishi wa habari wa Tanzania.
Mimi Ulukolokwitanga ni mteja wa PW kwa miaka mitano sasa, at least kila mwezi nawachangia hawa jamaa. Kwa maoni yangu kama abiria PW hii ya Sauda Rajabu imechoka sana ukilinganisha na ile ya Alfonse Kioko. Hii ya saizi haina hata ratiba ya ndege, kila siku kuna zaidi ya nusu ya ndege za PW zinachelewa kuondoka. Yes hata wakati wa Kioko kulikuwa na delays, lakini sasa ni mara 25 zaidi. Enzi za Kioko wafanyakazi walikuwa nidhamu na heshima kwa wateja, saizi hakuna nidhamu tena. Huyu mama ameondoa hadi BIA kwenye ndege na huku bei ya ticket ikipaa mara dufu, enzi za Kioko tulikuwa tunapata hadi offa ya bei, kwa sasa imebaki historia. Yes huenda jamaa alikuwa na mapungufu kama binadamu lakini sio kwa vile ni Mkenya, hili andiko ni la kibaguzi lenye lengo la kuficha udhaifu wa huyu dada wa Kiswahili kwa kisingizio cha matatizo nimeyakuta, kama matatizo umeyakuta so what? We si ndio CEO, tatua hayo matatizo kwa skills zako sio kupita magazetini kusema matatizo kayaleta mtangulizi wangu. Huu upuuzi watanzania tusiukubali kabisa, mtu kaomba kazi akijua kuna changamoto, anashindwa kuzitatua anasingizia mtangulizi wake, bull shit. Kama umeshindwa kazi Sauda achia ngazi.
kaka mbona unakua mkali una hisa nini?
Nimeongea na mtu wa precision aliniambia kuna baadhi ya strategic decisons ambazo zilikua wrong ndio zimewafikisha hapa.Kwa hiyo kinachofanyika sasa ni kuwithdraw baadhi ya routes ambazo zinaligharimu shirika ,then kubaki na ATR's ambazo ni cost effective kwa muda,then baadae hali itakapotulia ndio warejeshe na boeing.Mimi kwa mtizamo wangu , huu ulikua ni mpango kabambe wa kuhamisha fedha zetu, kwenda nje,na hivyo kuanzisha shirika jingine.Kwa hasara aliyosababisha Kioko haiwezekani kueleweka katika hali ya kawaida.
unles hilo shirika lilikua linaendeshwa kifamilia zaidi kwa kuaminiana kama ndugu.