Even if t z their official language but not all passengers are capable to speak dat stupid language,,Wat I know,they need clients as other business done no matter language U speak...
Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
Labda umedandia huu uzi katikati. Hujaelewa kinachozungumzwa!
Kwa manufaa yako ni hivi:- Kisheria, anaye ruhusiwa kukaa kiti kwenye emergency exit row ni lazima akidhi vigezo fulani..... ni vingi tu siwezi kuvirudia vyote, lakini moja wapo ni kuweza kuelewa lugha ya kiingereza.
Hii ni kwa sababu ikitokea dharura, atachukua majukumu ya mhudumu. Lugha rasmi ambayo kamanda anawapa amri wahudumu kwenye dharura ni Kiingereza...
Ndio sheria! Pia anarekodiwa kwenye vifaa ili isaidie upelelezi baadae.
Pili huyu mheshimiwa imeelezwa na abiria aliyekuwemo kuwa alikuwa amelewa chakari na kuleta ubishi wa kipiuzi. Hadi abiria wenzake walimzomea kwa ujinga alio onesha.
Hizo ndio facts....
Pia mimi sio kinda wa kunufaika na elimu ya kubabaisha ambayo naona umeipata wewe. Kuwa na elimu ni kuweza kujua kiwango cha uwezo na ujuaji wako. Waache wataalam wa fani zao watimize kazi zao.
Mdada kafanya kazi yake, na Captain akakubaliana nae, heshimu hilo kwanza
mkuu, tatizo si unajua hostess wetu, inawezekana kabisa hawamjui, wanaona 'haka kasee labda ndio mara ya kwanza, wanaona isiwe shida'..
Sasa precision inakoelekea ni kubaya zaidi, kutoka kweye kuchelewesha ndege/safari hadi, "kunyanyasa" wateja kama walivyofanya!
Sio hairusiwi, panasuhusiwa kukaa pale unless wewe utakuwa hujawahi panda hiki chomboNimjuavyo Dr Lwaitama Ni msomi na mtu alielimika iweje aende akakae hapo na anajua hairuhusiwi?
Karibu kwa kasuku
hapa naona unafiki tu.mbona lwaitama hajawahi kukataa vyuo vikuu visifundishwe kwa kiingereza?mbona hapa tanzania lugha ya taifa ni kiswahili lakini lugha ya kufundishia vyuoni na sekondari ni kiingereza?kwa nini hajawahi kupinga hilo?lwaitama ni mnafiki tu katika hilo jambo.hivi anafikiri ndege ni kama gari?inapotokea dharura mkiwa juu ndio muanze kutafuta nani anajua nini?kwanini maandalizi yasiwe tangu chini?pw wako sahihi kabisa na rubani yuko sahihi kabisa,kwanza lwaitama ashitakiwa,amehatarisha usalama wa anga.ikiwezekana apigwe hata ban katika usafiri wa anga.
acha mihemko, tumia busara kidogo tu. hivi kuhoji kitu ni kufanya fujo? maana hilo ndilo alilotuhumiwa. mbona hao wahudumu hawajaripoti polisi kuwa amekataa kutumia kiswahili? nahisi huo sio unafiki!
kuhusu lugha ya kufundishia, aliwahi kusema angetamani afundishwe kwa kihaya maana hicho anafahamu vizuri sana. Dr. Lwaitama ni miongoni mwa wasomi wachache wanaounga mkono elimu itolewe kwa kiswahili kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu hadi ya juu.
kumbuka ule ni usafiri na sio taasisi ya elimu
hahahahaaaaa kwikwikwi!wewe ndo uache ukichwa maji,mleta mada ameeleza kinaga ubaga.hapo ni pfisini kwa mtu,mwenye ofisi ndie anaetoa utaratibu wa ofisi yake,halafu yeye analeta mzaha,kwanini asichukuliwe hatua?maelezo anayopewa ni kwa ajili ya usalama,sio wake tu bali wa kila aliyeko ndani ya ndege yeye alichokuwa anataka ni nini?cheap popularity?lugha ya anga ni kiingereza,usafiri wa anga hatukuuanzisha sisi,waliouanzisha ndio walioweka utaratibu huo na lazima ufuatwe yeye ni nani anayeleta masihara na kazi za watu?hayo ndo matatizo ya kujifanya mjuaji sana mwishowe unaonekana bwe*ge tu.kwa hiyo yeye alitaka kwa kuwa ni lwaitama ndo wabadili utaratibu wao wa kazi?wewe na yeye kwendeni zenu kule
Hahaa mzee mtata huyuuuu
Hapa, Fast jet wanakujaje tena hapa!?