Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 425
Last Sunday nilikuwa natoka Tabora kuja Dar kwa usafiri wa ndege ya Precision Air.
Kero ya kwanza (ambayo ni ya muda mrefu) niliipata pale kwenye security check ambapo jamaa (Tanzania Airport Authority) hawana modern equipment bali unafungua masanduku jamaa wanapekua. Kibaya zaidi kuna mdada nikaona kang'ang'ania sanduku langu sijui alikuwa anatafuta chupi......pumbavu zake!
Kero ya pili ni pale baada ya kupanda ndege, mara wakamwita abiria mmoja na kumjulisha kuwa galoni lake la asali lilikuwa inavuja kwenye mizigo hivyo waishushe au atafute mfuko wa nailoni aifunge vizuri. Abiria akawaambia poa waishushe tu, kama mfuko atoe wapi, kwenye ndege kuna duka?
Kero ya tatu ni pale ngoma ilipochelewa kuondoka na baadae wakaanza kushusha mizigo.....rubani akatutangazia eti temperature imepanda ghafla toka 25 centigrade to 31 centrigrade hivyo taking off ingeleta shida mzigo mkubwa. Hivi huwa wanajaza mizigo mpaka maximum capacity? Assume ndio ndege ingekuwa inataka kutua na mzigo mkubwa, si tungechimba mchanga hapo?
Kwanza, Security check ni kazi ya TAA na sio Precision Air. Kama TAA pale Tabora hawana vifaa vya kisasa vya kuscan hand luggage za abiria wakulaumiwa ni Wizara inayohusika na sio Precision Air. Pili, je wewe ulitaka ndege pamoja na mizigo ya watu wengi ichafuliwe na asali kutoka kwenye galoni la abiria mzembe? Ebu fikiria ndege yenu ingelivamiwa na nyuki ambao wanafuata asali uoni usalama wa abiria ungelikuwa hatarini? Tatu, kuhusu kushushwa mizigo iliyozidi. Wewe ukumbuki yalio wapata Mheshimiwa marehemu Akukweti na wenzake pale Mbeya wakati ndege iliposhindwa kupaa angani kutokana na uzito mkubwa wa mizigo? Ndugu yangu hacha kutoa lawama zisizo na msingi.
Mkuu kero ya Precision Air katika swala hili ni nini? Kwanza, Security check ni kazi ya TAA na sio Precision Air. Kama TAA pale Tabora hawana vifaa vya kisasa vya kuscan hand luggage za abiria wakulaumiwa ni Wizara inayohusika na sio Precision Air. Pili, je wewe ulitaka ndege pamoja na mizigo ya watu wengi ichafuliwe na asali kutoka kwenye galoni la abiria mzembe? Ebu fikiria ndege yenu ingelivamiwa na nyuki ambao wanafuata asali uoni usalama wa abiria ungelikuwa hatarini? Tatu, kuhusu kushushwa mizigo iliyozidi. Wewe ukumbuki yalio wapata Mheshimiwa marehemu Akukweti na wenzake pale Mbeya wakati ndege iliposhindwa kupaa angani kutokana na uzito mkubwa wa mizigo? Ndugu yangu hacha kutoa lawama zisizo na msingi.
Mkuu wewe ni rubani?Napenda nielezee kidogo kero yako ya tatu. Upakiaji wa abiria kwenye ndege una vigezo vingi hususan urefu wa kiwanja, capacity ya ndege, urefu wa kiwanja toka usawa wa bahari (sea level) na hali ya joto (Temperature).
Mara nyingi watu wanafika uwanjani wanaambiwa ndege imejaa lakini ukiingia ndani unakuta kuna viti kama 5 hivi viko wazi. Unajiuliza kulikoni?
Kawaida viwanja vilivyo karibu na bahari (sio ziwa) kama Dar Es Salaam, Mombasa n.k vinafanya ndege iwe na uwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo kuliko viwanja vilivyo juu ( toka usawa wa bahari) kama Nairobi, Jorburg, ADDIs Ababa n.k. Kwa mafano ndege aina ya B737-200 ina uwezo mdogo kuchukua abiria kutoka (take off weight) Jorburg kuliko Dar ES Salaam. Dar Es Salaam ndege hiyo hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria 116 (fullcapacity) na mizigo yao lakini kutoka Jorburg maximum passengers ni 80 tu! Kwa sababu Jorburg iko juu sana toka usawa wa bahari kuliko DAR
Pili viwanja vilivyo kwenye ukanda wa joto vina uwezo mdogo (payload penalty) wa kubeba abiria na mizigo kuliko viwanja kwenye ukanda wa baridi. Ndio maana kiwanja cha Dubai (hata kama kiko kwenye bahari) kina payload penalty wakati wa joto. Kwa hiyo utakuta safari nyingi za ndege kutua na kutoka (landing and take off) kwa Dubai zinafanyika usiku wakati hali ya joto imeshuka kidogo.
Hivyo basi kilichotokea Tabora ni kwamba wapakiaji ndege (load controllers) walipakia ndege kutokana na temperature fulani lakini mwenye kauli ya mwisho katika mambo ya weight and balance ya ndege ni rubani mkuu (captain). Akiona kuna mabadiliko ya temperature analazimika kuagiza hatua fulani kuchukuliwa ikiwemo kushusha mizigo hata abiria ikibidi.