Pre Season | International Friendly Match | Ismailia SC 1-1 Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Julai 17, 2022 imecheza mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa wa kirafiki (International Friendly Match) dhidi ya Ismailia SC ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Misri ambapo mchezo huo umekwisha kwa sare ya kufungana bao moja kwa moja, bao la Simba SC likiwekwa kimiani na Nyota Augustine Okrah.

FT: Ismailia SC 1-1 Simba SC
20220717_205650.jpg
20220717_205658.jpg
 
Hii game ilikuwa ya kimya kimya.

Ila angefungwa mtu basi tusingejua kabisa kuwa leo mechi ya kirafiki ilichezeka.
 
Hii game ilikuwa ya kimya kimya.

Ila angefungwa mtu basi tusingejua kabisa kuwa leo mechi ya kirafiki ilichezeka.
Wewe ndo usingejua, lakini Wanamsimbazi na Wadau wangejua kwasababu ratiba ilishatoka kabla ya mchezo huu kuwa Simba SC atakuwa na Mechi ya Kirafiki na Ismailia SC
 
Sasa msako dhidi ya kikosi cha pili cha Ismaily SC...?

Mtani mbona unachekesha sasa
Yaani safari hii Simba SC ni mwendo wa ngiri tu meno nje, hapo ni kucheki tu mitambo.

Wale wazee wanu walioachwa na timu zao mbona wana kesi ya kujibu yaani..!
 
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Julai 17, 2022 imecheza mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa wa kirafiki (International Friendly Match) dhidi ya Ismailia SC ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Misri ambapo mchezo huo umekwisha kwa sare ya kufungana bao moja kwa moja, bao la Simba SC likiwekwa kimiani na Nyota Augustine Okrah.

FT: Ismailia SC 1-1 Simba SCView attachment 2294533View attachment 2294534
Ni mechi nzuri ya kirafiki na ibaki hivyo ni ya kirafiki,ni mazoezi tu, timu zote mbili hazikucheza kwenye kiwango cha kimashindano, ismaily imecheza jana mechi ya ligi yao,na simba ni timu mpya na kocha mpya.

Hivyo isichukuliwe kiukuuuubwa.
 
Usichukuliwe kiukubwa kwasababu gani..! Kwani hii si Pre Season..!
 
Ubaya Wa Mechi Hizi Unaweza Kuta Aliyefunga Goli Ni Bocco Lakini Sifa Anapewa Mwingine ilimradi Tu , Au Inaweza Kuwa Mtu Kapigwa Tatu Bila ila Ndo Ivo Tena Kwakuwa Watu Hawajaona Ni Mwendo Wa Kupigwa Kamba Tu Mitandaoni, Kwanini Wasitangaze Kabla Kama Watacheza Mechi?
 
Baada ya kufika Misri katika mji wa Ismailia ambao wameaweka Kambi, ratiba ilishatoka kwa Simba kuwa kutakuwa na game dhidi Ismailia SC.

Ingia Simba App ina kila kitu, mpaka goal la Augustine Okrah

Mbona mnasumbuka na mambo ambayo yapo wazi sana.

Kwahivyo hii sare nayo hamjapenda.
 
Back
Top Bottom