Aisee sijawahi ona mtu anayejifanya anajua kumbe hajui chochote kama wewe duh. Yaani umeandika ujinga mtupu hadi nimetikisa kichwa. Ushauri tu, anza kujifunza programming from scratch, alafu soma concepts mbalimbali za operating systems, anza kujua how memory works na imetengenezwaje, networking, cpu, kuna mambo kibao ya kusoma hapo utakutana nayo, jipanue akili kwanza alafu urudi miaka ya mbele ukiwa umeiva utaona ulichoandika hapa ni total rubbish.
Kwanza kuna tofauti kubwa sana kati ya encryption na hashing, encryption algorithms zinachofanya ni kuchukua data flani, zinabadilisha hiyo data isiweze kutambulika kwa kutumia key flani, na kwa kutumia the same key unaweza decrypt kurecover data yako in original form. Zipo encryption algorithms kibao sitoingia in details zinafanyeje kazi unaweza jisomea mwenyewe, popular ni kama RSA inayotumika kuficha data yako isionekane wakati inapita kwenda na kutoka kwenye server.
Hashing algorithms zenyewe zinavyofanya kazi ni unachukua data flani alafu inaproduce hash, hata kama una seed huwezi kupata original data kutoka kwenye hash hiyo isingekua hashing tena tungeiita tu encryption algorithm. Hizi zinatumika sehemu ambazo huna haja ya kua na the original data, mfano kwenye kutunza password za wateja kwenye database badala ya kutunza password ya mtu in clear text, unaichukua unaihash alafu unatunza hash, mteja akihitaji kulogin unachukua password yake unajaribu kuproduce hash ili uone kama ni same hash then unajua password ni sahihi, ili hata mtu akifanikiwa kuhack database akiona password hazitomsaidia kulogin coz hawezi pata the original password hata afanyeje.
Sasa turudi kwenye mambo uliyoandika wewe, in short umekosea kila kitu ulichoandika.
MD5 sio encryption algorithm, MD5 ni hashing algorithm, huwezi chukua md5 hash ukapata the original information, na MD5 siku hizi haitumiki sana kwa sababu ina flaw moja kubwa, ni rahisi kutumia information tofauti na zika-collide kuproduce the same hash, sifa ya hashing function nzuri ni kuproduce unique hashes kwa kila input unayoweka.
Gzip sio encryption algorithm pia, Gzip ni compression algorithm, inachofanya ni kuchukua data yako ikacompress into smaller size, haihitaji password wala nini, mtu yeyote anaweza ku-unzip na kupata original data, so sio encryption pia coz haihitaji key.
Sasa kama umeshindwa kujua vitu simple namna hii ambavyo ni commonly used kila siku, mfano gzip inatumika kwenye browser zote unazotumia, website nyingi karibia zote siku hizi zinatumia gzip kucompress data, kama hujui kitu simple namna hiyo kuna haja yoyote ya mtu kuamini unachokiandika? hujui unachokiandika umecopy na kupaste ulivyoelewa kumbe ulivyoelewa ni uongo mtupu.
Algorithm converter ndo kiumbe gani hicho? we jamaa unakuja na vitu ambavyo havipo, hakuna kitu kinaitwa algorithm converter, naomba usiweke post nyingine tena kuhusu haya mambo aisee, nenda kasome miaka 5 rudi tena ukiwa umeelimika. Kama una post nyingine za hivi naomba ufute zote usipotoshe watu.
Na hiyo code uliyoandika kutokua detected na antivirus sio accomplishment, hiyo code sio virus, toka lini code ya kuhash data ikawa virus seriously?