Power shedding is back | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Power shedding is back

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 8, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Power shedding is back

  2008-10-08 13:30:10
  By Guardian Reporter

  The Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) has announced fresh load shedding countrywide following yesterday`s collapse of a big transformer at its Ubungo plant in Dar es Salaam.

  In a message signed by Tanesco communication manager Badra Masoud yesterday, the company said it had also been forced to re-introduce power shedding after another Aggreko gas turbine in the city developed mechanical problems.

  With the two equipment out of order, Tanesco said, the national grid had suffered a shortage of 40MW from the defective transformer and 20MW from the Aggreko turbine.

  A rationing schedule issued by Tanesco shows that power will be disconnected in the city from 9am to 6pm on Mondays, Wednesdays and Fridays.

  On Tuesdays, Thursdays and Saturdays, power will be disconnected in Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Mbeya, Tanga, Dodoma and Morogoro regions.

  SOURCE: Guardian
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Tanzaniaaa, Tanzaniaaa
  Nakupenda kwa moyo woteeeeee!!
  Nchi yangu Tanzaniaaa, jina lako ni tamu sanaaa!!
  Nilalapo nakuota weweee, niamkapo ni heri mama weee!!!
  Tanzaniaaa, Tanzaniaaa.
  Nakupenda kwa moyo woteeeeeeeeeeeee!!!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Je, Fisadi RA na kampuni yake ya kifisadi Richmond/Dowans kupata mkataba mpya toka serikalini?

  Mgawo wa umeme waanza upya

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  ZIKIWA zimepita wiki mbili tangu Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), lisitishe mgawo wa umeme, shirika hilo jana limetangaza kuanza tena kutoa umeme wa mgawo kwa nchi nzima.

  Katika mgawo huo, Mkoa wa Dar es Salaam, utapata mgawo mara nne kuanzia Jumatatu.

  Ofisa Mawasiliano wa Shirika hilo, Badra Masoud, alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema Tanesco imelazimika kuurejesha tena mgawo wa umeme baada ya transfoma moja kubwa ya kuzalisha umeme katika kituo chake cha gesi cha Ubungo kuharibika, sambamba na kuharibika kwa jenereta kubwa la kuzalisha umeme katika kituo cha Aggreko.

  Alisema kuharibika kwa transfoma hiyo ya mtambo wa gesi wa Ubungo, kuna sababisha upungufu wa megawati 40 katika mtambo huo, unaozalisha megawati 100.

  Alisema pia kuharibika kwa jenereta ya Aggreko, kuna sababisha kuwepo kwa upungufu wa megawati 20 ambapo kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha megawati 40.

  "Kutokana na sababu hizo mbili, kumekuwapo na upungufu wa megawati 60 na hivyo kulilazimu shirika hilo kugawa kiasi kidogo cha megawati zinazobaki katika gridi ya taifa," ilisema taarifa hiyo.

  Aidha, alisema mashine mbili za Songas zenye uwezo wa kuzalisha megawati 70, nazo bado ziko katika matengenezo kutokana na wahusika wa Kampuni ya GE ya Marekani kwa kushirikiana na Songas kuagiza injini mbili, moja kutoka Marekani na nyingine Uholanzi.

  Kwa mujibu wa ratiba ya mgawo huo iliyotolewa katika taarifa hiyo, Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Jumatatu utapata umeme wa mgawo kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

  Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Mbeya, Tanga, Dodoma na Morogoro, itakuwa na mgawo siku ya Jumanne kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

  Dar es Salaam, tena itakuwa na mgawo siku ya Jumatano kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni wakati mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Mbeya, Tanga, Dodoma na Morogoro, itapata mgawo mwingine wa umeme siku ya Alhamisi kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

  "Dar es Salaam itapata umeme mwingine wa mgawo Ijumaa, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni na Jumamosi itakuwa zamu ya mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Mbeya, Tanga, Dodoma na Morogoro, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni," alisema.

  Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jumapili itakuwa tena zamu ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

  "Tanesco inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wa mgawo huo uliojitokeza," ilisema taarifa hiyo.

  Wiki mbili zilizopita Tanesco ilitangaza kumalizika kwa mgawo wa umeme baada ya mafundi kutoka Marekani kufanikiwa kutengeneza mtambo mmoja wa umeme unaozalisha megawati 40, uliokuwa umeharibika ghafla.

  TANESCO iliwahakikishia wananchi kwamba hakutakuwa na mgawo tena wa umeme, labda kwa dharura ndogo ndogo ambazo shirika litatangaza endapo zikitokea.

  Juzi, Rais Kikwete akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano wa kwanza wa majadiliano kati ya serikali na wafanyabiashara wakubwa, uliofanyika jijini Dar es Salaam, alisema serikali imejipanga kuhakikisha tatizo la kukosekana kwa umeme wa uhakika halitokei tena na litabaki kuwa historia.

  Rais aliyasema hayo baada ya baadhi ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha wasiwasi juu ya hali ya upatikanaji wa umeme usio wa uhakika nchini na kuitaka serikali kuliangalia vizuri suala hilo, kwani ni moja ya mambo yanayokwamisha shughuli zao.
   
 4. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Tafadhali usiendelee kuimba

  unanifanya nizidi kusikia uchungu na kulia mbele za watu. ooooh tanzania weeee, unakwenda wapi tanzania? me nadhani kwa watu wenye pesa na uwezo wa kuwekeza katika sekta ya umeme wafanye hivyo. tanesco wanaringa zaidi hata kuamua wanavyoamua bila kufikiria hasara tunayopata watu tunaotegemea umeme ili tupate riziki ya kila siku kwa sababu wanajua hatuna la kuwafanya, tutake tusitake tutawavumilia tu maovu yao yote na kuendlea kutumia huduma zao mbozu zisizo na utaratibu .

  Iwapo kungekuwa na makampuni zaidi ya mawili ya umeme (kama vile simu voda ikikuzingua unaweka line ya tigo, zain wakukukera unaweka zantel), hali isingekuwa hivi, makampuni yangekuwa yanafanya kazi kwa ufanis zaidi na kutoa huduma bora ili wasiwapoteze wateja, lakini kutegemea haka ka kampuni ka kipuuzi ka tanesco ni sawa na kuendelea kukubali kuishi na mume/mke ambaye hana uwezo wa kuzaa kamwe na wewe ukitegemea siku moja kupata mtoto, no way
   
 5. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sijui rais wa nchi yetu akiwa na marais wenzie huwa yuko proud na nini!!! Hata hao wawekezaji wanaowatafuta, kweli wanatuelewa! Mtu anakuja kuona mazingira ya biashara na first impression ni kuwa nchi haina umeme!

  Hivi hizo safari za rais nje kweli hazitoshi kununua mashine za umeme! Pole sana Tanzania
   
Loading...