Kwanza,unajuaje kuwa hiki kitu ni chema,na hiki ni kibaya?
Kitu kinachowaongoza kutenganisha ubaya na wema ni kipi?
Na kwanini,Mungu anahusishwa na mema na shetani anahusishwa na ubaya?
Na tunauhakika gani kuwa Mungu yupo?au shetani yupo?
Ndugu
Einstein....labda tu nijaribu kudadavua swali/maswali yako,kama ifuatavyo nikianaza na ni nini hasa kinachokufanya kutambua ubaya na wema...jibu hapa ni simple kabisa....mwanadamu ana kiungo kimoja hatari sana..ambacho ni "UBONGO".katika organ hii ndipo hasa huo ulimwengu wa ROHO unapo cheza ngoma zake.Hapo ndipo mapambano hasa yana-take place.
Kiungo hiki(UBONGO) ndicho kinacho channel na kukuruhusu wewe ku-control "FREEWILL"(UHURU WA KUJIAMULIA).Hii FREEWILL ni sawa na daftari tupu,ambapo ni wewe sasa kuandika kwa uzuri au kulichafua.....utakapo andika kwa uzuri,ndipo unakuta MEMA yakitawala maisha ya mtu...ukiandika kwa ubaya...ndipo utakuta UBAYA ukiyatawala maisha ya mtu.
Hivyo uchambuzi wa hoja ya mleta mada bado narudia tena una-base sana katika kumakinika na kujua hasa nini maana ya ULIMWENGU WA ROHO......Mimi naamini yakuwa sisi tumeumbwa(tume-kuwa programmed katika kutenda mema).Ndio maana kama unabisha we jaribu kutembea kinyumenyume badala ya kimbelembele uone kama hata ww mwenye hutajishanaaa....mfano huu unamaanisha ya kuwa MUUMBAJI WETU amekusudia kuuishia WEMA.
Katika kujaribu kulijibu swali la pili...niseme tu MUNGU anahusishwa na WEMA kwa sababu ndie muumbaji wetu...na ametuumba vyema kabisa,bila fikra ovu..kama unabisha tizama sana ukuaji wa mtoto....ambapo jinsi utakavyo mlea katika kufuata WEMA ndivyo atakavyo kulia...hii ina maana uovu,mabaya,chuku,wivu,....yoote haya mtu hufunza au hujifunza na si kwamba anazaliwa akiwa na hivi vitu......Upendo,kwa mfano ni kitu ambacho tunazaliwa nacho naturally...hii ikichukulia mfano upendo wa mtoto kwa mama tangu akiwa mdogo kabisa na kadhalika.
Swali lako la tatu,pia nalijibu kama ifuatavyo...mimi binafsi yangu naamini kuwa MUNGU yupo..kwa sababu chache zifuatazo miongoni mwa nyingi...moja tizama jinsi ulimwengu ama DUNIA yetu ilivyo umbwa..huwezi hata kidogo kuniambia ni BIG BANG THING..kila ukionacho juu ya uso wa DUNIA si kwa bahati mbaya...kila kitu kinakitegemea kingine katika mpangilio mzuri kabisa...chukulia swala la unyeshaji wa mvua.....MUWAKO WA JUA....BAHARI KUWA HEATED....EVAPORATION.....CONDENSATION...PRECIPITATION(MVUA)...Je uratibu huu ni BIG BANG THING which happened and started just from nowhere...ndio ulipelekea coordination ya hizi taratibu.HAPANA...hii ni dhahiri ya kuwa yuko MUWEZA,MASTER-PLANNER aliye coordinate na ambaye ana-supervise haya yote.
Kwa uchache ndugu yangu Einstein na wadau wote katika uzi huu....hivi ndivyo binasfi yangu ninge jaribu kujibu maswali yaliyo ulizwa hapo juu.
Karibuni kwa michango na maoni zaidi.
Ahsanteni.