kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,104
Nimetafakari kwa kina zaidi juu ya nguvu iliyopo ktk ubaya(nimejikita kutafsiri dhana ya ubaya kwa kadri jamii zetu zinavyoamini) nikaona dhahiri kuwa kwa kiasi kikubwa ubaya una nguvu zaidi ya wema hasa ukizingatia juu ya haya.
1. Mtu anaweza akafanya mema mengi machoni pa watu lakini baya moja likafuta mema yote aliyofanya na hatimae mtu anahesabika kuwa mbaya.
2. Yanayotafsiriwa kama ni ubaya katika jamii ndio yanashawishi zaidi kuliko mema, mfano mtu anashawishika kufnya ngono,kulewa n.k lakini masuala kama kusaidia wagonjwa na wahitaji huwa inahitajika nguvu ya ziada kushawishi watu wafanye.
3. Ni rahisi zaidi kwa muasherati kujulikana katika jamii kuliko yule anayependa kuisaidia watu.
4. Habari mbaya husambaa haraka mithili ya moto katika nyasi kavu lakini habari njema huchechemea kwa mguu mmoja.
5. Wakati mwingine watu wanajua kitu fulani ni kibaya na madhara yake yanafahamika lakini wanafanya tu.
6. Ni rahisi zaidi kwa watu kutoka nje wakashuhudie mzinzi alivyokamatwa kuliko kutoka nje kumsikilza mhubiri anayehubiri.
7. Maovu husisimua yaan yanatengeneza attention kubwa zaidi ya mema, mfano mdada akikatiza kapiga kimini ataamsha hamasa ya watu wengi kuliko yule aliyevaa kwa staha.
8. Kasi ya mabaya inaongezeka kila uchao zaidi ya wema
Sasa suala la kujiuliza ni nini siri ya hii nguvu iliyopo katika mambo tunayoyaita ni mabaya? Iwapo ubaya unafungamanishwa na shetani na wema ni wa mungu ambaye anaaminika kwa wengi ndiye mwenye nguvu zaidi.
Je, kwanini wema uzidiwe na ubaya? Naomba michango yenu wadau juu ya Hilo.