Jethro
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 2,219
- 371
Mgao wa umeme hapa Arusha umekuwa kero na janga kubwa la kiuchumi kwa wajasiriamali wadogo haswa baada ya mgao kuwa wa masaa zaidi ya 16 kwa siku ya masaa 24 ktk baadhi ya maeneo tu. TANESCO Arusha imekuwa ikitoa mgao kwa baadhi ya maeneo tu huku maeneo mengine kama ya Uzunguni, Mjini katikati, Unga LTD, Njiro, Moshono wakiwa hawana mgao hata siku moja. Maeneo ambayo yamekuwa ni waathirika wakubwa wa mgao ni maeneo ya pembezoni ambayo ni Ngaramtoni, Baadhi ya sehemu za Sakina, Kata yote ya kimandolu, Kwa mrefu, Tengeru, Usa river, KIA hadi Mererani. Maeneo hayo yameathirika vibaya na mgao wa kila siku huku maeneo mengine yakiishi ulimwengu mwingine kabisa hali ambayo imewagawa wakazi wa Arusha kati makundi ya walio nacho na wasiokuwa nacho. Licha ya kuwepo mgao wa kila siku tangu November 2010, wananchi wamechukizwa zaidi na mgao wa wiki hii Jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 7 usiku na Jumapili kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 Asubuhi ya jumatatu. Chuki dhidi ya Serikali inaongezeka na wananchi wanaona wanachokozwa na serikali na ufa kati ya wananchi na serikali inaongezeka siku hadi siku . Shughuli za uzalishaji zimeshuka kwani hamna mtu anaweza tena kufanya shughuli kama kuchoma grills, salon,saw mills,Mill machine, kufuga kuku, kazi za kutengeneza vifaa vya electronics n.k. Hii imepelekea watu kupoteza ajira na kubaki Kijiweni.
Kilio cha Wananchi ni kuwa TANESCO wafanye huu mgao fairly ili kufanya makali yapungue haya maeneo yaliyozoeleka na badala yake siku na masaa ya mgao angalau yapungue ili watu waweze kufanya shughuli za uzalishaji.
Tunatoa na tunazidi kutoa kilio chetu kwa TANESCO wajue kwamba sisi tunaopata mgao tunaumia sana na kwa serikali ijue kwamba watu wamechoka na itafika mahali wananchi wataitaka serikali iseme wazi kama sehemu hizi za mgao ni Tanzania au ziko Somalia.
Tunajua TANESCO Arusha ikitumia busara mgao huu ukafanyika fairly ungeweza kupunguzwa hadi kufanyika mara 2-3 kwa wiki kama wakazi wa Uzunguni, Mjini katikati, Unga LTD, Njiro, Moshono, Monduli na maeneo mengine ambayo umeme haukatwi kabisa.
Meneja wa TANESCO Arusha na Mkurugenzi wa TANESCO Mr. Wiliam Mhando please hili suala liangalieni hili kwani ni kero mno mno.
Wajua Wana JF,
Tatizo kubwa hapa sijui hawa Tanesco wanajua kazi yao kweli au ndio tayari si ha sa imeingia huko, Sijui inaingia akilini kweli kukata umeme every day hawa Tanesco wanaingiza faida kanai au walisha pata faidi sasa ni time ya kuwanyanyasa Wananchi? Strategic Plan zao ziko wapi, Mbaya zaidi hawa ku fnaya PA kuhusu swala la umeme na hata kama wangefanya PA still % fulani wangepisha maelezo na serikali kuhusu Mgao maana ni mgao wa kimya kimya huku nyuma tulfanyiwa PA( Publica Announcement) kuwa ni mgao wa One Month sasa duuuuh imekuwa ni zaidi nahi tatizo kwa mji wa Arusha hata nilipo kuwa huko lilikuwepo sishangai huo mji wameufanya wa Kijanja janja hivi na umekumbatiwa na wakubwa na pale watu wa kipato cha chini ndio kabisaaa watabaki kunyanyasika tuu gap iko kubwa sana kwa wenye nazo na wasio nazo mji hauko kwa City Planining kabisa sinawashangaa kila kukicha wanatashindwa kuupa JIJI kani uko shaghala baghala mfumo wa ujenzi wa makazi ni mbovu kupita maelezo kukuza kwa mji ni mwendo wa kinyonga watu waote wanataka kukaa hapo mjini huduma za maji kwenda huko njie ya mji kama Kisongo, Ngaramtoni Njiro Chini hazifanyiki na mbaya zaidi Usalama wa Raia ndio mbovu kabisaa wizii wa kuvunja mijumba ya raina na uvamizi wa kutumia silaha ndio umekidhiri sasa kweli mji utakuwa na maendeleo kweli? na umeme ndio huo tena.
Mr. Mhando nadhani mwatakiwa kuachana na si hasa mfanye kazi kuna madhambi mengi isikute mwayaficha na mwawafiv=chia hao wakubwa huku mwawanyanyasa wananchi walipa kodi kuto pata haki zao.
Tanesco Strategy Planning yenu tokea uhuru ina phases 2 kuanzia 1960' upto now its 50 years ambayo iko 25/25years sasa sijui ipi plan mwaitekeleza mkisema tena kuna plan ya 25years huko mbele inamaana huku nyuma hamkufanya kitu. Which means wakati wa mwl.JK nyerere uongozi wake ulikuwa bora zaidi katika zama izo ambayo Technology ilikuwa haijazagaaa kama kipindi hiki ambacho Technologia ipo nasi ila utawala wenu ni uozo mtu yani ni upuuuzi mtu na pamoja na elimu yenu hamjui mfanyalo mpaka sasa na ukweli ni kwamba even iyo 25yrs plan ni fake which means nothing will be done.
Mbaya zaidi Communication btn Customer service wenu na Technician ni zero kabisa unamuliza mtu wa tanesco kwa simu jamani umeme unarudi muda gani yeye anakupa mlolongo wa maelezo mengi na yote ni uongo mtupu ati kuna nguzo imekatia Hapo Korogwe ndio maana umeme hapa arusha hakuna wakati Moshi hakuna tatizo ivi ni ujinga gani huu alafu anakuambia umeme sidhani kama utarudi mapema kwani mafundi bado wanashugulikia within 5min mara umeme huo umerudi sasa huyu mtu wa customer support kanijibu nini? na hii hali iko mikoani kote sio uongo