Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,393
Je niwangapi tunafurahia kuishi na ndugu zetu mijini? Swali hili lina majibu yenye kuchekesha na kushangaza pia. Ni wachache sana kati yetu ambao tunaishi na ndugu zetu hawa tukiwa na furaha nao. Wengi tunaishi nao tukiwa hatupendi. Tunajikuta tukilazimika kuishi nao kwa sababu, hatuwezi tu kukataa. Unakuta mtu anawajaza ndugu zake nyumbani kwake, halafu anaenda kuwanywea pombe ili awaambie ukweli. Kesho pombe zikiwa zimemtoka kichwani, hasemi nao, anawaogopa. Akiwa huko pembeni analalamika kuhusu hao ndugu zake. Lakini akiwa nao anaonesha kwamba, anawajali na kupenda kuishi nao.
Kwa nini?
Ni kwa sababu ya kufungwa na jamii na kushindwa kujiamini. Lakini, pia ni hofu inayotokana na kufungwa na mfumo wa familia mchangamano. Mtu anaogopa kwamba, akimfukuza au kukataa kuishi na ndugu zake, naye akija kuishiwa au kupata shida, ndugu watamkataa. Hivyo anachofanya ni sawa na kuomba mkopo kabla hajashikwa na shida. Kuna wakati wanandoa wanajifungia chumbani mwao kumjadili ndugu ambaye amengangania kuishi nyumbani kwao. wanaogopa kumwambia moja kwa moja. Kwa hiyo wanapanga njia ya kumwondoa kwa visa au visingizio vingine.
Wengi wetu tunaishi na ndugu zetu kwa mtindo kama huu. Tunajitahidi kuwatafutia visa ili waondoke majumbani mwetu. Hawa ndugu zetu nao hawaelewi kwamba, hivyo ni visa vya kuwafanya waondoke. Wao watajua fulani ana roho mbaya tu, ambayo haiwatishi au kuwasumbua wao kuishi hapo nyumbani. Na ndio hapo unajiuliza nyumba ni ya nani, ni nani anayepaswa kupanga aishi na nani na kwa sababu gani? Ni sisi wenyewe bila shaka. Kwa nini sasa tuwe wanafiki hadi kutafuta visa na sababu ili ndugu hawa waondoke majumbani mwetu? Ni kwa sababu jamii imetufunga na tumekuwa watumwa wa mtazamo fyongo wa jamii.
Nijuavyo mimi, tunapaswa kuwasaidia ndugu wengine, bila kujali kama ni ndugu zetu au hapana. Lakini kusaidia huko hakuna maana ya kulazimishwa kusaidia. Tunasaidia kwa sababu, tunaona wengine wanahitaji na wanastahili msaada wetu, sio kwa sababu jamii imetaka. Kama mtu hastahili msaada hatupaswi kumumiza kwa kumpa msaada huo. Nasema kumuumiza kwa sababu, kama mtu anakuja kuishi kwako bila shughuli wala malengo, nawe ukampa kila kitu humsaidii. Huyu unamdidimiza kwenye ujinga na ukosefu wa ufahamu kimaisha. Baada ya muda fulani, atakuwa hawezi kujisaidia au kuwasaidia wengine.
Kama ndugu amekuja kwako na unajua kwamba, anachohitaji huwezi kumpatia au hastahili, huna haja ya kumdanganya, huna haja ya kuwa mnafiki. Kama amekuja kwako na unajua hastahili kuishi nawe hapo, inabidi umwambie. Ni vizuri kumwambia kwa upendo kuhusu unachofikiri. Ni vyema akaijua hali halisi. Kama bado anangangania kuishi hapo kwako, ati kwa sababu wewe ni ndugu yake, huna budi kumnyofoa kwa nguvu. Kumbuka kwamba umwambie ukweli au hapana, atakusema tu, hata kama ukiishi naye kwa wema wa kiasi gani atakusema vibaya tu. Huo ndiyo ubinadamu wenyewe.