Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,533
Ni miezi 15 tangu awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli na kaulimbiu za HapaKaziTu na Utumbuaji zilipoingia madarakani na kuongoza Taifa.
Pamoja na shauku kubwa ya wananchi na Taifa zima kuona kasi yenye umakini na hasa suala la HapaKaziTu na Utumbuaji, uhalisia unaoonekana ni kukwama kwa unyoofu wa kimatendo wa kaulimbiu hizo (fluidity and sound execution).
Je ni kitu gani kimetokea na kusababisha kuporomoka kwa ufanisi wa kaulimbiu hizo ambazo zaweza simama pekee bila kuhusishwa na matokeo ya siasa na kauli za Kiki?
Je Rais Magufuli alikuwa amejiandaa kivipi kuanza kutimiza na kutoa matokeo chanya ya HapaKaziTu na Utumbuaji?
Kinachoonekana sasa hivi ukikipima kwa umakini ni fahari ya macho na vipodozi: iwe ni vyeti feki,utumbuaji, kubana matumizi, kubana Usiasa au hata ukuswanyaji wa mapato.
Kama Taifa tumeendelea kushangulia matukio na kauli zinazozungumzia vitu ambavyo ni sawa na viini macho, lakini uhalisia wa hali ya Mtanzania bado uko pale pale: Masikini, Mjinga na mwenye Maradhi.
Je ni wapi Rais Magufuli na kaulimbiu zake amekosea? je Ilani ya CCM na kujitutumua kwa kudai sasa ni CCM mpya na hata"matokeo" ya mabadiliko ndani ya chama na hata serikali (utumbuaji) kumesaidia kunyoosha kwa udhati, uhakika na umakini mfumo mbovu wa kiutawala,sera na hata kuonyesha kuwa HapaKaziTu si kauli ya kuombea kura bali kuna mfumo unaoeleweka katika kila ngazi ya jamii nzima kuwa tunakuwa na umahiri wa uzalishaji kutumia juhudi na maarifa?
Tunapoangalia Utumbuaji na hata ujio wenye kauli za "kushughulikia" au "kuwaonyoosha" Watanzania, je jamii yetu kiuhalisia na ukweli wa dhamiri, nafsi na hata matendo imebadilika na "kujirudi" au jamii nayo imebaini utamu wa kauli na lugha tamu kwa kujifanya ikiwa wanyenyekevu, watimiziaji na hata waoga wa Kutumbuliwa na HapaKaziTu?
Je Rais Magufuli na serikali yake, imeweza kuwa kinara wa matendo kufanya mambo kwa uadilifu, kufuata kanuni na sheria au nayo imetumia udhaifu wa kisheria, kikanuni na kikatiba kujifanyia mambo na kuyahalalisha kuwa ni sehemu ya utimizaji wa ahadi ya Tanzania mpya yenye kujitegemea, ongezeko la uzalishaji na pato la Taifa na lenye uadilifu?
Je Rais Magufuli amefanikiwa kuuza fikra zake kwa wateuliwa wake na wao wakawa wabunifu endelevu (progressive thinkers) katika kila sekta zao kujenga mifumo imara ya utendaji, uzalishaji na matokeo halisi na si kukimbilia vipaza sauti kubwekakauli mbiu hizo?
Sina haja ya kutoa mifano kujenga hoja yangu ili malumbano na majadiliano yaendelee, lakini kwa nafsi na nadhiri iliyo safi(clear conscious) bila kuleta ushabiki wa upingaji au pongezi,ni kitu gani Rais Magufulina Serikali yake(hata ndaniyaChama) inabidi kufanya kubadilisha hali namuonekano hasiunaojijenga kwa wananchi kwa vipengele vifuatavyo:
Uchumi
Uzalishaji Mali
Elimu
Afya
Huduma za Jamii
Demokrasia
Uwazi na Uwajibikaji
Utawala Bora
Haki za Binadamu
Wikiendi njma!