Postmaster General: Posta mmepoteza mzigo wangu na hamtaki kunilipa, tafadhali nitendeeni haki

DPN

Member
Sep 28, 2020
31
68
KWA POSTMASTER GENERAL, TPC.

Tarehe 13/3/2020 nilituma mzigo kwa njia ya posta kutoka Magu, MWANZA kwenda Mbinga, RUVUMA; ambapo nilihudumiwa na REGINA SEDEDE ambaye alinipa Invoice Namba M-7203-03200066751 ya shilingi 11,900/= (Elfu kumi na moja na mia tisa tu) ambazo nililipa taslimu na mzigo wangu ukapewa Register namba RD037111148TZ tayari kwa kusafirishwa.

Mzigo huo ulikuwa na vitu vyenye thamani ya shilingi 140,000/=; ukijumlisha na gharama kusafirishia mzigo huo nilizolipa posta shilingi 11,900/=, thamani ya mzigo huo inafikia shilingi 151,900/=

Nilimtumia namba ya Register niliyopewa posta mtu niliyemtumia mzigo (kama nilivyoshauriwa na mfanyakazi aliyenihudumia posta); na nilianza kuwasiliana na niliyemtumia mzigo huo wiki moja baada ya kutuma mzigo, ili afuatilie mzigo huo Posta Mbinga, lakini mpaka leo mzigo huo haujamfikia.

Baada ya kufuatilia kwa Posta Masta Magu, jibu alilonipa ni kuwa, tracking system inaonyesha mzigo ulipokelewa Posta Dar-es-salaam kutoka Posta Mwanza tangu tarehe 17/3/2020; na siku hiyohiyo 17/3/2020 mzigo ukatumwa kwenda Posta Songea kwa gari la posta; lakini system hiyo haionyeshi chochote baada ya mzigo kutoka posta Dar-es-Salaam

Nimeendelea kufuatilia mzigo huo Posta Magu, na nimekuwa nikishauriwa kuwasiliana na niliyemtumia mzigo; lakini naye jibu lake kutoka Posta Mbinga limekuwa ni hilohilo kwamba mzigo haujafika Posta Mbinga.

Leo ni zaidi ya miezi tisa tangu nitume mzigo huo (tarehe 13/3/2020) lakini mpaka leo haujanfikia niliyemtumia.

Nimeshaandika barua na kupiga simu mara nyingi kwa Posta Masta Magu na Mwanza nikifuatilia mzigo huo, lakini hakuna jibu la maana ninalopewa ambalo linaleta ufumbuzi wa hicho kilichotokea; wanachofanya mabosi hao ni kupotezea mpaka nichoke kufuatilia hatimae ninyamaze, maisha yaendelee wakati nimepoteza

Hiyo siyo sawa, wala siyo haki, maana hamko hapo kwa ajili ya kunyang'anya mali za watu ndani ya shirika hilo la umma huku mkilipwa mishahara; mnasababisha madhila kwa watu na hata kuharibu maisha yao!!

POSTMASTER GENERAL, nina kila sababu ya kuamini kwamba mzigo huo umeibiwa na watumishi wa shirika unaloliongoza; na kama ndivyo, nina kila sababu ya kuamini kwamba mizigo mingi ya wateja inaibwa na watumishi wako wasiokuwa waaminifu, na wewe umeshindwa kukomesha tabia hiyo mbaya ambayo inalichafua shirika.

Kwa vile umeshindwa kufikisha mzigo huo kwa niliyemtumia, basi fanya utaratibu upasao ili unifidie mzigo wangu; niko tayari kutoa uthibitisho wa madai yangu ili unifidie.

Asante; wako katika ujenzi wa Taifa.
DPN
 
Ivi watalaam,chombo hiki kinasimamiwa na nani,mfano jamaa ana malalamiko yake,mahali gani anaweza kwenda kushtaki?
Mfano; Vyombo vya mawasiliano na habari,wasimamizi ni tcra,mteja akiona ameonewa basi malalamiko yake atapeleka tcra na kuhudumia au kukutanishwa na mlalamikiwa wake.

Je kwa kesi ya member huyu,anafaa akalalamike wapi ili asaidiwe.?
 
Achaneni na makampuni ya CCM, mbona Kuna courier companies kibao mjini, na wako cheap, faster and reliable
Bujibuji, siyo kila pahala kuna hizo private courier companies; na kama zipo siyo kila mtu ana uwezo wa kuzimudu.
Lakini kwa nini wateja tutwishwe wajibu kwa uzembe wa watu wa shirika la posta?
Shirika lipo kwa ajili ya kutoa huduma kama hizo; lina uongozi kuanzia wizara ya uchukuzi, lina bodi ya wakurugenzi, lina CEO, mameneja wa mikoa mpaka wilaya. Ni taasisi rasmi inayotambulika kitaifa mpaka kimataifa; na tuna haki ya kuitumia.
Tatizo la shirika ni kutokujitambua kwa baadhi ya watendaji na watumishi, kitu kinachopelekea madudu kama haya kutokea.
Bujibuji, wahukumu posta kwa kutokutimiza wajibu wao; usituhukumu sisi wateja kwa kutumia posta.
 
Tatizo taasisi nyingi za serikali uwa wafanyakazi wana hulka ya kuona wanakusaidia hata kama huduma umelipia. Na kukiwa na tatizo hawaonyeshi kujali kivyovyote wanaona shida ni yako upambane na hali yako.
Umeongea kwa hisia sana
 
Hivi Posta ya bongo nayo wanatoa Tracking number kama majuu?
 
Hivi Posta ya bongo nayo wanatoa Tracking number kama majuu?
Tracking system wanayo na inafanya kazi. Siku za mwanzo nilipokuwa nikifuatilia suala hilo posta Magu, niliwahi kuona taarifa za huo mzigo wangu za kutoka Magu kwenda Mwanza (kwa gari), Mwanza kwenda Dar-es-salaam (kwa ndege), na kutoka Dar-es-salaam kwenda Songea (kwa gari la posta); na kila sehemu mzigo unapoondoka kuna taarifa kadhaa muhimu zinazosomeka kwenye system, vikiwemo jina la mhudumu anayefungasha mzigo kwenye kifurushi kinachoondoka na mzigo husika, anamkabidhi nani na saa ngapi.

Niliona hata jina la mhudumu aliyefungasha mzigo wangu kwenye kifurushi kilichokwenda Songea na gari la posta. Taarifa iliishia hapo kwenye tracking system.

Ninaamini aidha mzigo wangu ulipotelea kwenye gari la posta baada ya kifurushi kufunguliwa, ama ulipotelea posta Songea; na ili kuficha madudu yao hayo, wahusika huko posta Songea wakaamua kutoku-update tracking system.

OK; hata kama hao wahusika wa posta Songea waliamua kutoku-update tracking system, kwa nini watu wa posta Dar-es-salaam mzigo ulipopita ukitokea Mwanza wasimfuatilie mtu wa posta Songea?

Na hata kama watu wa posta Dar-es-salaam hawakumfuatilia mtu wa posta Songea, kwa nini Tracking System Administrator posta HQ asifuatilie taarifa za huo mzigo ambao kwenye tracking system ulikuwa bado una-hang?

Inawezekana haya mambo yanapangwa na wahusika ndani ya posta!! Ila nawaambia, kila kubwa ina kubwa yake.
 
Back
Top Bottom