Huenda watu hapo juu (ukiondoa mleta mada) hawaielewi Postgraduate Diploma, na nimesema hivyo kutokana na post zilizowekwa hapo juu. Ili mtu usome Postgraduate Diploma, lazima uwe graduate. Kama watu hapo juu mngekuwa na uelewa wa matumizi ya prefix na suffix, bila shaka hata neno 'post' lingetosha kuvuta attention kwamba 'postgraduate' ni nini!
Tukirudi kwenye swali, mleta mada anahoji 'utendaji', na sio 'qualification'. Kwa kweli ili upate jibu sahihi, inabidi ufanywe utafiti (research), vinginevyo labda upokee majibu ya mtu mmoja mmoja tu ambayo katika research ni sawa na dodoso (questionnaire) moja moja tu. Kwangu mimi, tofauti ya ufanisi wa mtu katika kazi kati ya graduand wa fani husika na postgraduand wa fani husika lakini aliyetokea katika fani tofauti, inaweza ikawepo au isiwepo kutegemea na hiyo fani. Mfano mzuri ni Uhandisi (Engineering), kwa chuo kilicho makini hakiwezi kupokea mtu mwenye degree au advance diploma ya fani tofauti na Engineering asome Postgraduate Diploma ya Engineering kwani wanajua utendaji wa huyu wa postgraduate utakuwa low ukilinganisha na mtu aliyetoka nayo taratibu kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa nne/tatu. The same to field za Health. Lakini fani za Biashara, utendaji na ufanisi unaweza usitofautiane kabisa hususan katika management, ila katika mambo ya kiufundi kama Audit, huenda mtu mwenye degree akawa mzuri zaidi.
Kwa ufupi utendaji wa kifanisi unategemea fani yenyewe