Posho zote za Wabunge kufutwa!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho zote za Wabunge kufutwa!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 15, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  [h=1]Ikulu kuwafutia posho wabunge[/h]
  Mwandishi Wetu


  [​IMG]


  Rais Jakaya Kikwete, Spika Anna Makinda  Matanuzi yao sasa kutegemea mshahara
  Upembuzi wa athari wafanyika
  Siku nne tu za ‘wikiendi’ walilipwa milioni 129/-  SAKATA la nyongeza ya posho kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeingia katika sura mpya, na sasa uchunguzi wa Raia Mwema, umebaini kuwa si tu Rais Jakaya Kikwete hatasaini nyongeza hiyo mpya kama tulivyoripoti wiki iliyopita, bali posho hizo za ‘kukaa kitako’ (sitting allowance) zitatangazwa kufutwa rasmi wakati wowote.

  Vyanzo vya habari vya gazeti hili ndani ya Ikulu vimethibitisha ya kuwa Rais Kikwete amepewa ushauri wa kufuta posho hizo kutoka kwa baadhi ya watalaamu wake na uamuzi unaweza kufanyika na kutangazwa wakati wowote.
  Inaelezwa kuwa upembuzi wa kina wa athari za kufuta posho hizo kwa wabunge na hasa kujua kama zitaathiri majukumu yao umekwishakufanyika na kukamilika na taarifa zinasema kati ya waliowasilisha takwimu za ‘kihasibu’ Ikulu, ni pamoja na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila.

  “Suala lililopo mezani kwa Rais si kusaini au kutosaini waraka wa mapendekezo ya nyongeza ya posho, bali ni kufuta sitting allowance zote kwa wabunge. Huo ndio ushauri wa kitaalamu unaohusisha hesabu za wahasibu na ambao, Rais ameukubali na unatarajiwa kutangazwa karibuni.

  Raia Mwema | Ikulu kuwafutia posho wabunge

  :peace::peace::peace::peace::peace:
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ushauri unaweza kuwa mzuri sana na wenye maslahi kwa Taifa, tatizo ni nani wa kuchukua hatua. Katika awamu hii, sidhani kama hilo (la kufuta Posho) linawezekana.
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  JK ebu tuonyeshe urais wako kwenye ili suala la posho..
   
 4. S

  Smarty JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  mh.. ngoja tusubiri tuone..wangetwambia kabisa hiyo hela itapelekwa wapi ?
   
 5. L

  Luveshi Senior Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  wapeleke kwa waalimu na madaktari.
   
 6. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tukisema CDM wanaongoza nchi indirect mnakasirika na kutukana humu lakini huo ndio ukweli..
   
 7. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  sina imani na serikali inayoongozwa na chama cha walafi!
   
 8. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili haliwezekani kwa nchi hii. Jk huyu huyu ninayemfahamu?
  Kama suala dogo kama la jairo wameshindwa , itakuwa hili la wabunge ????
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Watafuta posho halafu watawapandishia mishahara kwa asilimia 1000% mambo yatakuwa even worse!

  Hii ndiyo tz bana.
   
 10. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  He has no guts! hakuna Raisi hapo, yaani jamaa sidhani kama ana uwezo wa kufanya maamuzi kama hayo, ataanza kuchekacheka tu! what a nightmare president.
   
 11. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sikujua Nape yuko CDM sikuhizi!
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Posho zikifutwa miswada inayoletwa na serikali Bungeni itapita kirahisi kama ule wa marekebisho ya katiba? bajeti za wizara muhimu kama Nishati na Madini, Maliasili na Utalii kweli zitapita?

  Sekta binafsi tumezoea lakini serikali na mashirika yake bila posho siyo tu mambo hayataenda bali kuna uwezekano hata wataalam wake kutimkia huku sekta binafsi.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Pengo: Posho za wabunge ubinafsi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 15 December 2011 21:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  AONYA BILA KATIBA MPYA UCHAGUZI MKUU 2015 UTAKUMBWA NA GHASIA, AITA USHOGA NI WENDAWAZIMU
  Geofrey Nyang'oro na Fredy Azzah
  Mwananchi

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amezungumzia mambo kadhaa ya kitaifa akisema, ongezeko la posho kwa viongozi wa umma ni ubinafsi na kuonya kama Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 utafanyika bila ya kuwako kwa Katiba Mpya, utagubikwa na ghasia.Pengo alitoa angalizo hilo jijini Dares Salaam jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.

  Posho
  Kuhusu posho, Kadinali Pengo alisema viongozi wa Serikali na umma wakiwamo wabunge, wanapaswa kuacha ubinafsi na badala yake wafanye kazi kwa kuwafikiria zaidi wananchi kuliko maslahi binafsi.

  "Sisi Wakristu tunaamani kuwa, Kristu licha ya kuwa alitumwa na Mungu Baba kuja kutukomboa wanadamu alifanyika mwili na kuzaliwa katika hali ya umaskini na ufukara ili atukomboe. Viongozi wa Serikali, dini na watumishi wa umma, inatupaswa kuiga mfano huo,"alisema Pengo.

  Aliongeza, "Nasisitiza hili kwa viongozi sababu hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya wabunge na wananchi ambao wamejiongeza posho kwa madai maisha kuwa magumu. Viongozi hatupaswi kufikiria marupurupu yetu na maslahi yetu kwanza kabla ya kuwafikiria wananchi tunaowaongoza."

  Hivi karibuni Spika wa Bunge alitangaza kwamba wabunge wameongezewa posho ya vikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku kutokana na ugumu wa maisha wakiwa Dodoma. Mbali na posho ya vikao, wabunge hupewa fedha ya kujikimu Sh80,000 na Sh50,000 ya usafiri kwa siku hivyo kuwafanya kupata Sh330,000 kwa siku.

  Pengo aliwataka viongozi wa Serikali na umma kuiga mfano wa mwokozi wao, Yesu Kristu aliyesema kuwa, licha ya kuwa na nguvu za Kimungu, alipotumwa na Mungu Baba kwenda duniani kuwakomboa wanadamu, alijishusha na kuzaliwa katika mazingira ya kimasikini na ufukara ili aweze kufanikisha kazi hiyo.

  Katiba na siasa
  Akizungumzia Katiba Mpya, Kardinali Pengo alisema ni chombo muhimu kinachotakiwa kufanya kazi kwa umakini na kuhakikisha inapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
  Pengo alionya kuwa bila Katiba Mpya, taifa linaweza kuingia matatizoni kwa kuwa katiba ndio inayoelekeza wananchi kuchagua viongozi.

  "Tukicheza na Katiba, taifa litaingia matatani. Hivi sasa watu wameshailalamikia Katiba iliyopo kuwa ni mbovu na wakati huo huo Rais anachaguliwa kwa mpangilio ulio kwenye Katiba na anaapa kulinda Katiba na kuitetea,"alisema Pengo na kuongeza:
  "Tumeshasema Katiba iliyopo kwa sasa ni mbovu, tuchukulie suala hili "very serious (kwa uzito), tukamilishe kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, vinginevyo tutaingia matatizoni".
  Akizungumzia hali ya kisiasa, alisema hadi sasa Watanzania bado wanajifunza namna ya kuishi ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa baada ya kutoka ndani ya mfumo wa chama kimoja.

  Alisema jibu la kufikia kwenye siasa bora ni, kulifanyia kazi suala la Katiba, ambayo ndio itakayoamua wananchi wanataka kutawaliwa na watu wa namna gani.
  "Kwa sasa bado tunaishi ndani ya mawazo na mtazamo wa chama kimoja cha siasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ndio sababu, mawazo ya chama ndio yanayochukuliwa kama mwongozo wa Serikali. Lakini tukiweka mkazo katika Katiba, tunapaswa kutambua tunatengeneza katiba ya nchi na si ya chama kimoja,"alisema Kardinali Pengo.

  Sherehe za miaka 50 ya uhuru
  Kuhusu sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Kardinali Pengo alipongeza hatua tuliyofikia akisema ni nzuri na kutaka furaha hiyo iendelee kubaki miongoni mwa Watanzania.

  "Desemba 9 mwaka huu tulikuwa na Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Ujumbe wangu, tuendelee na furaha hiyo, lakini suali la kujiuliza sijui ni wangapi tulifurahia sherehe hiyo? Swali hili pia hata viongozi wanapaswa kujiuliza,"alisema.

  Katika ujumbe wake huo, Pengo alisema Uhuru wa kweli hauji kwa kubahatisha bali kwa kufanyakazi.
  "Mwalimu Nyerere alisema Uhuru ni Kazi. Sisi tukasema Uhuru na Kazi. Lakini ujumbe unabaki kama ulivyo, nami leo ujumbe wangu kwa Watanzania ni kutambua bila kazi hakuna maendeleo,"alisema Kardinali Pengo.

  Suala la ushoga
  Alipoulizwa kuhusu suala la mataifa makubwa ya Uingereza na Marekeni kutaka mataifa yanayowapa misaada kuwatambua watu wanaojihusisha na ushoga, Kadinali Pengo alijibu kwa kifupi "Ushoga ni wendawazimu".

  Alisema Mungu alipoumba watu; mwanamke na mwanaume na kuwapa hisia, alitaka watu wazaliane na kuujaza ulimwengu. Akahoji "Huyo mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke wanakutana ili iwe nini?"

  Pengo alisema wanaoshiriki ushoga wanamkosea Mungu na kusisitiza, kamwe hakutakuwa na furaha kwa mtu anayekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

  Elimu
  Kuhusu matatizo yanayiokabili mfumo wa elimu hapa nchini, Pengo alisema suala hilo linapaswa kuangaliwa pande zote mbili za wananchi na Serikali.

  Alipinga njia inayotumiwa na wanafunzi kudai haki kwa maandamano na kulazimisha mambo wanayoyataka kufuatwa na watu wengine.

  "Maandamano katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliibuka kwa mara kwanza lilipoanzishwa JKT, wanafunzi katika chuo hicho waliandamana na kumpinga Mwalimu Nyerere kuwa hata kama utatulazimisha hilo tunapinga na tutakwenda huku mioyo yetu ikiwa nje ya hilo,"alisema Pengo.

  Alisema siyo jambo jema kwa mtu yeyote anayedai haki kuhamaki kwa viongozi wa nchi na kusisitiza, zipo njia sahihi za kudai haki hizo.

  "Iko namna ya kudai haki, miaka iliyopita kulikuwa na mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,vijana walikuja kwangu kuomba msaada, nikawaambia hakuna anayepingana nanyi kudai haki zenu, lakini ninachoogopa ni tendo la baadhi yenu kutumia hata nguvu kulazimisha watu wengine kufuata mnachotaka,"alisema Pengo na Kuongeza:
  "Kesho mkiwa viongozi wananchi wakikataa mnayotaka kufanyika mtalazimisha".

  Hata hivyo, alisema ni vema Serikali ikakaa chini na kuangalia madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuyafanyia kazi.Alisema kama kuna upendeleo miongoni mwa makundi yanayosoma katika vyuo hivyo, harakati za kudai haki haziwezi kunyamazishwa kwa nguvu.

  Pengo alifafanua kwamba mambo yanayoweza kuchochea vurugu katika vyuo ni kitendo cha upendeleo wa utoaji haki, ikiwamo mikopo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo.

  "Ikiwa utamnyima mikopo mtoto masikini wa mkulima na kumpatioa mkopo mtoto wa mbunge mwenye mshahara unaoridhisha kuwa ndio anayesitahili kamwe harakati hazitazuilika hata kwa kutumia silaha,"alisema.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sio Kikwete wala Ikulu............hakuna anayeweza kuzifuta posho kwenye serikali hii.

  Pinda alisema ooooh........sitaki kuona semina na warsha...........wapiiii!!!!
  wao wenyewe ndo wanafanyiwa warsha ya danganya toto na wanapewa posho ya 280k na wanachukua!!!

  hawa wanatuona sisi makenge..........na tunakuwa makenge kweli kwasababu tunawaruhusu wafanye watakacho.
   
 15. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Miti huwa na tabia ya matawi yake kuelekea upande upepo uvumapo, sasa hilo ndilo linalomsumbua Nape na wenzake..
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Unajua, Nape km mwanasiasa lazima aangalie upepo unavumia wapi ili naye asipingane nao. Hawezi kutetea posho kubwa za wabunge ilhali naye anatafuta kujijenga kisiasa.
   
 17. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kikwete bado waweza kuwa rais bora sana Africa. Simple chukua hoja za wapinzani zifanyie kazi nakwambia hata chama chako kitaimalika sana
   
 18. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  KIUCHUMI CLASSICAL, (si
  kimaadili): Kitendo cha
  wabunge kuongezewa POSHO
  ni cha KUPONGEZWA
  KABISA!!!!! kwa kuwa: 1. Posho
  ni INCENTIVE TO WORK. Hivyo
  ufanisi wa mbunge utaimarika
  ktk kutumikia wananchi, 2.
  Kitendo hiki kitashawishi
  ELITES WA NCHI HII kuhamia
  bungeni 2015!! hivyo bunge
  litaingiliwa na wataalam (who
  search for green pasture)
  watakaokuwa chachu ya
  maendeleo kupitia mipango
  na maamuzi..., 3. Posho
  ITAPUNGUZA (sio kumaliza)
  tabia ya wabunge kujihusisha
  na ubadhirifu, na biashara
  nyingine.
   
Loading...