Posho Bungeni: Zitto, Lema katika vita ya maneno

Status
Not open for further replies.
"....UZALENDO SI UMASIKINI, Wabunge wanapaswa kulipwa vizuri ili waweze kupigania maslahi ya watumishi wengine na kuwa2mikia wananchi...." Mimi hoja yangu ni kuwa pia UZALENDO huohuo SI UTAJIRI! Anayefanya kazi na ale ila asiyefanya kazi asile isipokuwa wale wote wasioweza kufanya kazi kwa7bu ya hitilafu ya na uwezo wa miili yao. Ijadiliwe ikifaa ipitishwe posho 7bu huwezi kukubali/kupinga bila 7bu za msingi. Wabunge watoe 7bu za msingi sana kudai posho . Af pia, kama swala ni wakiongezewa posho ndipo na watumishi wengine waongezewe basi sheria itungwe kuwa wabunge wakipandishiwa posho tu basi na watumishi nao mishahara yao ipandishwe.
 
Wabunge wetu wameshindwa kutekeleza majukumu yao hivo kuwepo na ukomo wa kiti cha ubunge majimboni la sivyo wanasiasa wetu watachukulia ni sehemu ya kujipatia maslahi mazuri
 
Wanakula nyama zilizooza mnadani,wanakuja kusinzia bungeni,mama akitoa hoja utasikia ndiooo/siyooo halaf wanataka mshahara upande. Majambazi hao kama kinana anavyomaliza tembo wetu
 
Hakuna haja ya kuongezewa posho,waliridhike na wanachokipata kisha wakawatumikie wananachi walalahoi,

Hongera kwa hao walioacha kuchukua hizo posho,atleast wameonesha kwa vitendo
 
Lema anapambana kumalizia jumba lake la kifahari Njiro pesa za M4C zote zimeishia huko.
 
Lema badala ya kutetea wana Arusha, anatetea aongezewe posho, kweli CHADEMA hawaaminiki, Nilimsikia pia akiomba barabara ya kwenda VETA (njiro Arusha) ambako ndiko anakoishi , ijengwe, maana haipitiki kirahisi.

Kwani hyo barabara ikijengwa atapita mwenyewe au ataweka geti na kuifunga? Kua na akili hata kidogo. Yote hayo ni athari za mwenge kweli upigwe marufuku.
 
Lema anapambana kumalizia jumba lake la kifahari Njiro pesa za M4C zote zimeishia huko.
Kwa mbaaaaali nimeanza kuielewa picha ya Kihindi ya Lema, na kwa hili Chdm mmejiporomosha sana kwa Wananchi mtaniambia kwny uchaguz 2015. BORA MNGEKAA KIMYA MPAKA UCHAGUZ UPITE THEN NDO MNGEIBUA HIYO HOJA. *mmechemsha*
 
Suala la posho kufutwa lilikuwa hoja ya CDM, lakini lengo ilikuwa posho kufutwa kwa wabunge wote, siyo kwa mtu moja moja. Zitto kutopokea posho peke yake bado haijalipunguzia taifa mzigo mkubwa wa kuwakomboa maskini wa nchi hii. Hata hivyo tunaambiwa Zitto anaingiziwa mabilioni kwenye akaunti zake kupitia moja ya mabenki huko majuu, hivyo suala la posho kwake ni kama vijisenti tu.

Ningemkubali Zitto angelishawishi bunge kusitisha posho, siyo yeye kususia posho.

Kwa hili akili ya Zitto imemtosha mwenyewe

Hizo manufactured stories ni bora mkawa makini nazo zingine zinatengenezwa makusudi ili kukwamisha vita dhidi ya jambo flani,Hiyo ni manufactured story ili ionekane kuwa Zitto anaingiza fedha nyingi kupitia njia nyingine ndio maana anakataa posho siku ya siku tutajikuta tukiunasa huu mtego na kuanza kuzipuuza hoja za posho za Zitto then hawa jamaa wa Upinzani wanao-protest ajenda za Zitto aidha wata-join na wa CCM kujiongezea posho au it's just an on-going political wars!
 
Lema anapewa kiburi na Mbowe kisa wote wanatoka sehemu moja Machame.

Zitto, na nyie tafuteni mtu mwingine awe M/Kiti sio lazima chama kiongozwe na WACHAGA tu.

Watawaburuza mpaka mchoke.
 
Kama mnaona ubunge haulipi rudieni kazi zenu za zamani.
 
Suala la posho kufutwa lilikuwa hoja ya CDM, lakini lengo ilikuwa posho kufutwa kwa wabunge wote, siyo kwa mtu moja moja. Zitto kutopokea posho peke yake bado haijalipunguzia taifa mzigo mkubwa wa kuwakomboa maskini wa nchi hii. Hata hivyo tunaambiwa Zitto anaingiziwa mabilioni kwenye akaunti zake kupitia moja ya mabenki huko majuu, hivyo suala la posho kwake ni kama vijisenti tu.

Ningemkubali Zitto angelishawishi bunge kusitisha posho, siyo yeye kususia posho.

Kwa hili akili ya Zitto imemtosha mwenyewe

Unajua kuna wakati lazima tusimame sasa na kusema yatosha na kuzipinga akili za ki.pu.mba.vu kama hizi,

Ni kweli ile hoja ya kupinga posho iliibuliwa na chadema kama unavosema,lakini kwa kuwa mle ndan ya bunge wengi wape autoamatically zilipopigwa kura za ndio CCM na wabunge wao wakashinda na lile suala likagota

Sasa kama lengo la harakati zile zilikuwa ni kupinga kwa wabunge wote na ikashindikana zitto na wengine wowote wale wakiamua kuendela kususia wanakosa gani?

Na kama hao wabunge wengine wa upinzani hiyo nia kama ilikua inatoka moyoni wameona shida gani kuendelea kwa umoja wao kuisusia posho ile na ikibid hata kuliomba bunge waipeleke kwenye shughuli zingine kama kusaidia wagonjwa
mahospitalin?au kusaidia walemavu na watoto yatima??kwanin wanaendelea kuchukua??

Unakuja sasa na story za kuambiwa ushahid uko wapi??kama ndan ya chama mnaanza kuwachafua viongoz na kujenga chuki na matabaka,vipi pale chama kitapochukua hatamu ya uongoz itakuaje??

Wewe hata usipomkubali zitto we nani??
Who knows you??U-JF GOLD MEMBER AU KITU GANI??AKILI ZA KIPIMBI NA UBAGUZ PELEKA KWA JAMAA ZAKO HUKO HUKO
 
Lema anapewa kiburi na Mbowe kisa wote wanatoka sehemu moja Machame.

Zitto, na nyie tafuteni mtu mwingine awe M/Kiti sio lazima chama kiongozwe na WACHAGA tu.

Watawaburuza mpaka mchoke.

Mtasubiri sana kuona hayo yakitokea. Mbowe Lema Dr slaa Mnyika wataendelea kuongoza hiki chama wakisaidiana na majembe kama kina Lissu Marando Baregu Safari Kitila mkumbo lakin sio huyo mnaempigia upatu.
 
Kwenye hili la posho ninamuunga mkono Zitto Kabwe, after all wabunge wanatakiwa kupigania kupandishiwa mshahara ambao unakatwa kodi na sio kupandishiwa posho ambazo ni wizi wa mchana...

Lakini hili la posho ni jambo dogo, kubwa ni lile la KAWAMBWA NA MULUGO KUBAKA MFUMO WA ELIMU NCHINI. Hilo ndio suala linahitaji mjadala kama kweli kuna mtu anaipenda Tanzania ijayo
 
Hakuna haja ya kuongezewa posho,waliridhike na wanachokipata kisha wakawatumikie wananachi walalahoi,

Hongera kwa hao walioacha kuchukua hizo posho,atleast wameonesha kwa vitendo
Wengine tumeshawashtukia. Sasa hivi wezi wanataka kujitambulisha kama makamanda wa kutukomboa wakati ukweli ni tofauti kabisa. Zitto komaa na hawa wajinga wote bila kuangalia ni wa CDM au chama gani.
 
kwanza lema anataka kuongezewa hela anafanya nini kwa watanzania hasa jimboni kwake zaidi ya mandamano na kupigana hovyo.
 
Suala la posho kufutwa lilikuwa hoja ya CDM, lakini lengo ilikuwa posho kufutwa kwa wabunge wote, siyo kwa mtu moja moja. Zitto kutopokea posho peke yake bado haijalipunguzia taifa mzigo mkubwa wa kuwakomboa maskini wa nchi hii. Hata hivyo tunaambiwa Zitto anaingiziwa mabilioni kwenye akaunti zake kupitia moja ya mabenki huko majuu, hivyo suala la posho kwake ni kama vijisenti tu.

Ningemkubali Zitto angelishawishi bunge kusitisha posho, siyo yeye kususia posho.

Kwa hili akili ya Zitto imemtosha mwenyewe

Mkuu wangu Mungi na wewe umejivua heshima yako kwa kutete upuuzi? Nimeumia sana kusikia kamanda nliyekua namuamini akiungana na wataka posho. Kama wakombozi wenyewe ndo hawa watetea posho kuna haja gani ya watu kupoteza maisha yao wakitaka mabadiliko? Kwa hiyo unataka na yeye aendelee kupokea kama wengine wanavyofanya hujui kua wanagawana jasho letu? Kamanda Lema amenidhalilisha sana kutetea posho au msimamo wa chama umebadilika kuhusiana na hili? na kama umebadilika kuna haja ya kutujulisha ili tujue cha kufanya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom