Posho Bungeni: Zitto, Lema katika vita ya maneno

Status
Not open for further replies.
Mbona gazeti la Mwananchi limemtaja ni Godbless Lema(mbunge wa Arusha)naumia kuona Mamluki kama Lema anajiona yeye ndo CHADEMA,wakati amekalibishwa tu----sisi Watanzania tunataka Upinzani wa kweli sio wa kilaghai
Bravo Zitto kwa kusimamia unachoamini
 
Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.

Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.

Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.

Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
"Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema".

Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

"Mimi sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011," aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.

Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.

"Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee," alisema Zitto.

Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine wa umma.

"Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine," alisema Lema na kuongeza:

"Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600".

Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.

"Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili, ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,"alisema Lema.

Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.

"Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000 ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata Sh10,000,"alisema Lema.

Source: Mwananchi
 
Hawana lolote wanazodoana kwa sababu msingi wa chama chao CHADEMA niwa kilaghai. Most of them are scam profiteers.

Hivi unategemea nini kama kiongozi wa upinzani ni von politician kwa maana kuwa uliudanganya umma kuwa ameachana na "anasa" zitokanazo na kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani na mpaka akarudisha gari ya KUB ili serikali ipige mnada, halafu baadaye kinyemela akarudi serikali na kuwaomba wasilipige mnada.

Usipindishe mantiki, je ni halali wabunge kudai maslahi manono ya zaidi ya milioni 12 kwa mwezi huku watumishi wengine kama waalimu wakiambulia shilingi 200,000 kwa mwezi? Wakulima ndiyo usiseme wanavuja jasho bila msaada wa serikali huku wakilipa ushuru mbalimbali wa mazao, pembejeo kujinunulia na kulipa VAT kila wakinunua mahitaji yao ya kila siku. Serikali gani inafanya hayo, ni ya CCM. Na ninyi watu wa Lumumba kila kukicha ni kupiga porojo ya CDM huku wabunge wakijiongezea marupurupu kimyakimya!
 
na wewe mbunge mtarajiwa 2015 una maoni gani? Mshahara wa milioni 11 na kiinua mgongo cha 72 million haviwatoshi wabunge maccm na hivyo wanastahili kuongezewa badala ya kuongeza mishahara ya walimu, madaktari, manesi na wafanyakazi wengine serikalini ambao mishahara yao bado ni ya kiwango cha chini sana?


acha utoto, godbless lema ndio aliyetamka hayo maneno. Chadema hakuna mkombozi zaidi ya zitto.
 
Hii ndiyo akili za wabunge wa chadema maneno mengi mantiki hakuna mtu kama lema yule si mzima anaweza kuongea kitu ambacho hata hakijui ili mradi tu asikike.
 
Suala la posho kufutwa lilikuwa hoja ya CDM, lakini lengo ilikuwa posho kufutwa kwa wabunge wote, siyo kwa mtu moja moja. Zitto kutopokea posho peke yake bado haijalipunguzia taifa mzigo mkubwa wa kuwakomboa maskini wa nchi hii. Hata hivyo tunaambiwa Zitto anaingiziwa mabilioni kwenye akaunti zake kupitia moja ya mabenki huko majuu, hivyo suala la posho kwake ni kama vijisenti tu.

Ningemkubali Zitto angelishawishi bunge kusitisha posho, siyo yeye kususia posho.

Kwa hili akili ya Zitto imemtosha mwenyewe
 
Acha kuonyesha upumbavu wako wewe!!! Hivi hujawasikia wabunge wa ukoo wa panya wanaodai mishahara haiwatoshi? Hukumsikia bi kiroboto juzi wewe!? Unaishi nchi ipi!?

acha utoto, godbless lema ndio aliyetamka hayo maneno. Chadema hakuna mkombozi zaidi ya zitto.
 
Pigeni hela majembe riziki huja kwa mafungu na wajinga ndio waliwao na mlichaguliwa ili mkale na huku mtaani wanalijua hlo wanalalamika kisela tu watanyamaza!! C mnawajua wabongo maneno tu
 
Kiukweli kutoka moyoni nampongeza Zitto kwa kuendelea kukataa kuchukua Posho,wengine wasanii tu,kila siku wanajijali wao tu,tungekuwa na Zitto 20 naamin mishahara ya Anasa kwa Wabunge,mawaziri,na Viongozi waandamizi yangeondoka Tanzania.
Wengi wapo bungeni kupigania Maslai yao,sio Mwananchi wa kawaida
Bravo Zitto
 
Well... but sio sawa ku judge wabunge wote nchi hii kwa kigezo kimoja...
 
siku mkumuelwa zitto sijui mtaficha wapi nyuso zenu,
na mtaanza kuwaelewa wabunge mmoja mmoja haa na bado watalilia posho mpka mtakoma
 
ABRACADABRA NIMEZICHOKA KWANINI CHADEMA HAWAKAI KTK ONE PLATFORM KTK UTENDAJI WAO NA KTK SUALA LA KIMAAMUZI

-->NOW ON THE WAY ---> CCM, but let think twice!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom