Posho Bungeni: Zitto, Lema katika vita ya maneno

Status
Not open for further replies.

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
16,927
13,011
Zitto juu ya Posho;


"Enyi Watanzania, wabunge wenu wanataka posho ziongezwe na mishahara. Mbunge mmoja wa upinzani kanisemea mbovu huko Dodoma kwenye kikao cha wabunge eti mimi ni kikwazo kwa wao kuongezewa posho. Kasema nikiwa Arusha nakaa chumba cha dola 600 kwa siku. Hivi Hoteli gani Arusha ina chumba dola 600 kwa siku? Albert Msando naomba msaada nikija Arusha unionyeshe hiyo hotel japo nione chumba cha dola 600 kinafafanaje...."
Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.

Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.

Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.

Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
"Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema".

Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.

"Mimi sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011," aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.

Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.

"Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee," alisema Zitto.

Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine wa umma.

"Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine," alisema Lema na kuongeza:

"Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600".

Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.

"Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili, ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,"alisema Lema.

Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.

"Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000 ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata Sh10,000,"alisema Lema.


Source: Mwananchi
Aisee nimeikumbuka hii habari ya 2011

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kusaini na kuchukua posho ya kikao cha Baraza la Madiwani mwishoni mwa wiki, lakini akatetea uamuzi huo akisema alikwenda kuzima njama za kufukuzana.


Lema na madiwani wenzake watatu wa Chadema, walishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha, kinyume cha msimamo wao wa kutohudhuria vikao hivyo.

Mapema mwaka jana, Lema na madiwani wote wa Chadema wa Jiji la Arusha waliweka msimamo wa kutomtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo na kutohudhuria vikao vyote vya Baraza la Madiwani kwa madai kuwa Meya huyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na kuhudhuria vikao ni kumtambua.

Lakini Ijumaa iliyopita, Lema na madiwani Isaya Doita (Ngarenaro), Crispin Tarimo (Sekei) na Sabina Francis (Viti Maalumu), walihudhuria kikao hicho na kupokea posho kwa malipo ya kuhudhuria kikao.

Lema alikiri alisaini posho hiyo yeye na wenzake na kudai kulikuwa na njama za kutaka kuwafukuza madiwani wa Chadema kwa kukosa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila ya kuwa na taarifa yoyote na kwa mujibu wa sheria na kanuni wangetimuliwa.

Alisema kwa kufanya hivyo siyo kama wamebadilisha msimamo wao wa kutomtambua Meya Lyimo na Naibu wake, Estomii Mallah, isipokuwa ilibidi wafanye hivyo kutegua mtego wao wa madai ya kufukuzwa madiwani.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Chang'a alisema madiwani wa Chadema walipewa posho baada ya kuhudhuria kikao hicho na wala hakukuwa na njama za kutaka kuwafukuza kama alivyodai Lema.

Source: Habari Leo
Nakumbuka Zitto Kabwe alipohusisha na rushwa kwenye kupitisha bajeti ya wizara ya Nishati na madini.

"Kwa kuwa ‘my conscious is clear', (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza:

"Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'."

Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!
 
Hawana lolote wanazodoana kwa sababu msingi wa chama chao CHADEMA niwa kilaghai. Most of them are scam profiteers.

Hivi unategemea nini kama kiongozi wa upinzani ni von politician kwa maana kuwa uliudanganya umma kuwa ameachana na "anasa" zitokanazo na kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani na mpaka akarudisha gari ya KUB ili serikali ipige mnada, halafu baadaye kinyemela akarudi serikali na kuwaomba wasilipige mnada.
 
Wabunge wetu wanapalipwa milioni saba na ushee na eti hizo ni kidogo sana! Waliwatukana sana walimu na madaktari walipogoma kuwa mishahara yao ni midogo! Kazi kwelikweli!
 
Jamani mimi bado nina mawazo sana ya jinsi Elimu yetu inavyo bakwa na kutendewa vibaya na wanasiasa.
 
kama atakuwa ni shibuda basi zitto asipoteze muda kulumbana naye maana alishaweka wazi msimamo wake juu ya posho za wabunge
 
Zitto juu ya Posho;


"Enyi Watanzania, wabunge wenu wanataka posho ziongezwe na mishahara. Mbunge mmoja wa upinzani kanisemea mbovu huko Dodoma kwenye kikao cha wabunge eti mimi ni kikwazo kwa wao kuongezewa posho. Kasema nikiwa Arusha nakaa chumba cha dola 600 kwa siku. Hivi Hoteli gani Arusha ina chumba dola 600 kwa siku? Albert Msando naomba msaada nikija Arusha unionyeshe hiyo hotel japo nione chumba cha dola 600 kinafafanaje...."

CCM itaadhibiwa pindi itapopandisha mishahara yao ya mamilioni kuwa mamilioni zaidi kwa wabunge huku wastaafu wakishindwa kumudu maisha yao kwa shs 50,000 kwa mwezi. Wajue walivumilia mengi ktk kuujenga uchumi wa nchi hii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom