Porojo za hiza tambwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Porojo za hiza tambwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mfianchi, Sep 19, 2010.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Jana nilikuwa mitaa ya Sinza Kumekucha,nilikuwa napita nikakuta wana CCM wako kwenye Kampeni,na mgeni wa heshima alikuwa Hiza Tambwe,kwa hakika nilishangaa kuona vijana wengi wahuni wasichana kwa wavulana wenye umri mdogo wakiwa wamelewa chakari na wakishangilia utumbo aliokuwa anutoa Hiza Tambwe.

  Kilichonisikitisha ni pale mheshimiwa huyo alipokuwa akiongopa ,kwanza alisema barabara ya kwanza nchini kujengwa ni ile ya Njombe -Songea na akaendelea kusema kuwa Kikwete katika miaka 5 kajenga shule nyingi za sekondari kuliko raisi yeyote ,mambo aliyoyafanya eti Kikwete katika miaka 5 wengine wameshindwa kuyafanya katika miaka 45,na wale "wahuni ''wakawa wanashangilia na mwisho akamalizia kusema watu wa Sinza tahadharini na jamaa anayechumbia uzeeni eti atakuja wapora wake zenu.

  Hakika sasa nimeamini maneno ya Jenerali Ulimwengu kuwa CCM imejaa viongozi wahuni ambao kazi yao kupiga porojo na hao ndio washauri wa Mzee Msekwa.

  Hakika mikutano ya kutangaza sera sasa imegeuzwa kilabu za pombe na mahala pa kufanya ukahba waziwazi ,kwa macho yangu jana niliona misururu ya akina dada na akina kaka wa chama tawala wakiingia na kutoka kwenye guest zilizokuwa karibu na uwanja huo wa mkutano wa hadhara ,hakika hata watu wazima walifadhaika kwa jinsi watoto wao walivyokuwa wanafanya vituko ni kama vile ni machokaraa hawana soni hata punje
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ccm watajibeba mwaka huu
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hatuibezi CCM bali tunapambana nayo majukwaani.
  Mbinu zote zimeisha na sasa wanafanya marejeo ya propaganda. Kipindi cha kudanganyana kimepita.
  Tunajenga tanzania ya wenetu na wajukuu zao iwe njema na si ya kimaskini kama ccm wanavyoijenga.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ikifika wakati chama tawala kinataka kutoweka huanza na vituko vya nuni firauni...tumeona hivyo kwa UNIP ya Zambia, KANU ya Kenya, MCP ya Kamuzu Banda n.k naona na CCM wanakwenda staili hiyo hiyo, hawana mda tena ni kama wanafungasha virago tu kama si mwaka huu mwakani...ila itafika tu kwanini ukolini ufe wakati ulikuwa na roho ngumu CCM ibaki?
   
Loading...