CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Ndugu hawa wamegeuka popo kudandia kila tawi. Katika mapendekezo yao kuhami uchumi wanapendekeza mambo mengine hata mwanafunzi wa economics au development studies wa mwaka wa kwanza ataona haiwezekani. Nipitie mapendekezo mawili ili kuonyesha walivyopotoka:
1. Wanapendekeza kila kaya isiyo na mfanyakazi sekta rasmi ilipwe 300,000/= kwa mwezi. Kwanza hawaelezi hii figure ya 300,000/= wameikokotoa vipi! Kawaida ukitaka kupata figure hii unatakiwa ufanye household/cost of living analysis. Hii TBS hufanya kila mwaka kwa kutumia wataalamu wa statistics. ACT wao wametoa kichwani kwa mtu! Nadhani upotofu mwingine ni kuiga wazungu. Wanadhani nchi za Ulaya zinagawa fedha kiholela. Tanzania haijaweka total lockdown kwa raia wake. Yaani Serikali haijazuia raia kuendesha shughuli zao za kiuchumi. Ulaya Serikali zimezuia ndio maana zinalipa fidia. Sio sadaka! Serikali zinatathmini hasara ya kila mtu mmoja mmoja na inamlipa fidia stahiki. Haitoi kiwango kinachofanana Kwa raia woote. Meneja atalipwa fidia yake mesenja atalipwa yake! Sio kulipa wooote 300,000 kama wanavyopendekeza ACT! Hivi hata ambaye akiwa huru kabisa hazalishi hata 1000 kutokana na uzembe umlipe?
2. ACT wanapendekeza Serikali itumie mifuko ya hifadhi ya jamii kulipia hizi gharama. Kwanza ACT wanaonyesha uelewa zero kuhusu mkataba wa ILO kuhusu Social Protection Funds. Mkataba huu unatamka wazi mfuko wa hifadhi sio mali ya serikali! Ni mali ya wanaochangia.Wanaochangia ndio wenye mamlaka ya kuamua mfuko utumikaje. ACT bado wako zama za ujima. Hata Ulaya Serikali hazithubutu kumega mifuko hii bila wahusika kukubali. Niwape kisa cha AU?
Miaka mitano iliyopita AFRICAN UNION (AU) waliandaa kitu kinaitwa AFRICAN MINING VISION (AMS). Ndani ya mpango huu walipendekeza mifuko ya jamii itumike kufadhili sekta ya madini! Sisi wenye uelewa tulipinga AU!
Tukawakumbusha ILO Convention na tukawaonyesha upotofu. Vipi hela ya mfanyakazi au mwanamfuko itumike kufadhili shughuli za kampuni kama De Beers, Barrick, Ashanti Goldmine? Masikini wafadhili mabilionea?
Tuliwapa notisi AU kuwa ikiwa wataendelea na mpango wao wa kuhujumu mifuko ya kijamii tutaitaka mahakama ya Afrika ya haki za binadamu kuingilia Kati. Walituelewa! Sio kwamba nchi zilikuwa na nia mbaya bali aliyepewa zabuni kuandaa hiyo vision alikuwa na conflict of interest! Na tungeionyesha mahakamani. Alikuwa mwajiriwa wa makampuni makubwa ya madini duniani. Alitaka kucheza cheusi chekundu Addis Ababa! Akakuta wajanja tupo!
Mawazo haya ambayo na ACT bado wanayo ni ile dhana potofu kuwa mifuko ya hifadhi jamii ni mali ya serikali.
Rafiki na mdogo wangu Ado Shaibu kabla ya kukurupuka na haya matangazo ya korona na uchumi hebu jaribuni kuwasiliana na wataalamu wawashauri. Tanzania ina utajiri wa wataalam utumieni.
TUSITISHANE