Pongezi Waziri Mchengerwa kwa kuahidi kushughulikia kupanda kwa madaraja ya watumishi wa umma

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
259
293
Sina maneno mengi sana ya kusema nimeona na kusikiliza clip moja hivi " Unasema kazi ya kwanza ni kushughulikia kupanda kwa madaraja ya watumishi wa umma Tanzania.

Kama ulichokisema ni dhamila yako ya dhati na Serikali ya Mhe, Rais Samia Suruhu Hassan imedhamilia kwa dhati, pokea hongera na pongezi kwa kuamua kuwapa haki na stahiki za wafanyakazi.

HONGERA mhe, Waziri hongera mhe Rais pia kwa hili.
 
Dah! Miaka sita si mchezo! Chamoto tumekiona. Watakuwa wamefanya jambo jema sana kwa sisi wafanyakazi. Hata wasipo ongeza mishahara, sawa tu! Ila siyo madaraja aisee! Ile kitu inatesa wafanyakazi mpaka basi.
 
Mh waziri ili kuongeza ufanisi naomba mawaziri wote watoe namba zao ili tuweze kuwasilisha baadhi ya kero hasa zile zilizoshindikana kutatuliwa ktk taasisi chini yao.

Huko polisi na PCCB baadhi ya maeneo bado ipo shida kubwa. Nadhani siku ya kupokea taarifa ya PCcb mh Rais aligusia pia !!
 
Shughulikia ukabila na upendeleo taasisi za umma kama vile TBS, Brela, NEMC, TRA, Latra nk

Usichekeshe members wa jukwaa hili bana huyu si ndiye Mkwe sasa uthubutu huo atautoa wapi? Sema kweli ikuweke huru kwelikweli.

Kwa Tanzania ya sasa tusidanganyane sifa ndio ziangaliwe. Kila mbusi ale kwa urefu wa kamba yake. Kama una ndugu, rafiki, kabila lako, jirani anatimiza vigezo na masharti na uko katika nafasi ya kumpendelea mpendelee tu usisite.
 
Jaman yaan nchi hii unakuta watu wote mmeanza kazi sawa kwenye HALMASHAURI za wilaya mbalimbali tanzania

Utashangaa walimu mnafanana elimu n.k lakini mwenzako unamwacha nyuma hadi madaraja mawili yeye yupo nyuma

Kuna sababu zisizo na afya huwa zinatolewaga kwenye hili utasikia unajua Afisa utumishi anakuwa hawajibiki ipasavyo au HALMASHAURI yenu ukusanyaji wa mapato upo chini

Pia, kuna swala la kujiendeleza mtu umesoma degree au hata masters mshahara upo sawa kabisa na mwenzako ambae hata bodi hamuhusu na wala hajawahi hata kujiendeleza

Haya mambo yanatakiwa yaangaliwe kwa jina sio swala la kupandisha madaraja ya bora liende yaan Ajira ya 2004 kimajadaraja unalingana na alieanza 2010 tena na elimu umejiendeleza pia.

Vyeo kwenye utumishi wa umma ni kizungumkuti sio kazi rahisi na sio kuiendea kwa papara
 
Dah! Miaka sita si mchezo! Chamoto tumekiona. Watakuwa wamefanya jambo jema sana kwa sisi wafanyakazi. Hata wasipo ongeza mishahara, sawa tu! Ila siyo madaraja aisee! Ile kitu inatesa wafanyakazi mpaka basi.
Tate Mkuu umenena vyema sana maana mtumishi wa umma anaposhidwa kupanda daraja unaathili pension yake na mafao yake ya uzeeni kiinua mgongo. Kwa kweli watu wameathilika sana na hii kitu mhe waziri asiishie hapo aangalie na mafao ya wastafu maana nao ni kilio tupu
 
Sina maneno mengi sana ya kusema nimeona na kusikiliza clip moja hivi " Unasema kazi ya kwanza ni kushughulikia kupanda kwa madaraja ya watumishi wa umma Tanzania.
Kama ulichokisema ni dhamila yako ya dhati na serikali ya Mhe, Rais Samia Suruhu Hassan imedhamilia kwa dhati, pokea HONGERA na PONGEZI kwa kuamua kuwapa haki na stahiki za wafanyakazi.
Hongera mhe, waziri hongera mhe Rais pia kwa hili.
Samia ameamua kumchagua mkwe wake/aliyemuoa mtoto wa mh.Samia kuwa waziri wa utawala bora.Kweli upendeleo hauwezi kuisha!
 
Aanze Na Hilo Kwa Kweli Aisee,Nimeteseka Sana,Hata Kukopa Nashindwa Maana Kahela Nnakolipwa Hakatoshi Hata Kuchukulia Mkopo Wa Kujenga Nyumba Na Kununua IST.
 
Mkuu Lukubuzo Mimi sina shida na hilo cha mhimu atende kazi kwa weledi na kwa haki.

Huna shida na hilo vipi?

Je ni kweli kuwa ni mkwewe?

Je akikosea huyo Waziri Rais ataweza kumkemea kwa Uhuru mtu ambaye ni Mkwewe.?

Je akimtumbua mwanae ambaye huyo bwana ni mkewe atamuelewaje Mama yake?

Vipi kuhusu mgongano wa maslahi ya Umma?

Inaleta maswali mengi, alisikika Mzee mmoja kijiweni akiuliza.

Tuchape kazi.
 
Samia ameamua kumchagua mkwe wake/aliyemuoa mtoto wa mh.Samia kuwa waziri wa utawala bora.Kweli upendeleo hauwezi kuisha!
Tanzania ngumu Sana! wajinga ni wengi mno,Cjaona kiongozi wa kuongoza Tanzania wote majizi tu, huyu naye mapeeeema keshaanza, Sasa huyo mkwe wake anajua nini kuhusu watumishi wa umma,au yupo kwa ajili ya kumjengea hi Maya via TIS.Utumishi wa umma tz ni kama mkosi fulani hawana thamani kabisa.
 
Huna shida na hilo vipi?

Je akikosea huyo Waziri Rais ataweza kumkemea kwa Uhuru mtu ambaye ni Mkwewe.?

Je akimtumbua mwanae ambaye huyo bwana ni mkewe atamuelewaje Mama yake?

Vipi kuhusu mgongano wa maslahi ya Umma?

Inaleta maswali mengi, alisikika Mzee mmoja kijiweni akiuliza.

Tuchape kazi.
[/QUOTE
Hilo nalo neno mkuu
 
Jaman yaan nchi hii unakuta watu wote mmeanza kazi sawa kwenye HALMASHAURI za wilaya mbalimbali tanzania

Utashangaa walimu mnafanana elimu n.k lakini mwenzako unamwacha nyuma hadi madaraja mawili yeye yupo nyuma

Kuna sababu zisizo na afya huwa zinatolewaga kwenye hili utasikia unajua Afisa utumishi anakuwa hawajibiki ipasavyo au HALMASHAURI yenu ukusanyaji wa mapato upo chini

Pia, kuna swala la kujiendeleza mtu umesoma degree au hata masters mshahara upo sawa kabisa na mwenzako ambae hata bodi hamuhusu na wala hajawahi hata kujiendeleza

Haya mambo yanatakiwa yaangaliwe kwa jina sio swala la kupandisha madaraja ya bora liende yaan Ajira ya 2004 kimajadaraja unalingana na alieanza 2010 tena na elimu umejiendeleza pia.

Vyeo kwenye utumishi wa umma ni kizungumkuti sio kazi rahisi na sio kuiendea kwa papara
Mkuu sana balmar uko sawa kwa 100% kwa sababu kama afisa utumishi hajafanya jambo fulani basi awajibishwe yeye bila kuathili wengine
 
Huna shida na hilo vipi?

Je ni kweli kuwa ni mkwewe?

Je akikosea huyo Waziri Rais ataweza kumkemea kwa Uhuru mtu ambaye ni Mkwewe.?

Je akimtumbua mwanae ambaye huyo bwana ni mkewe atamuelewaje Mama yake?

Vipi kuhusu mgongano wa maslahi ya Umma?

Inaleta maswali mengi, alisikika Mzee mmoja kijiweni akiuliza.

Tuchape kazi.
Na ndio changamoto anayokutana nayo sasa hivi, huyo mchengerwa anamshauri mambo ya hovyo kweli na sijui kwa nini hataki kumtoa hapo au anasubiri atakapotangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri baada ya kifo cha waziri wa ulinzi?
 
Halafu nashauri hiyo Wizara iitwe “ Wizara ya Uongozi bora na siyo Utawala bora”

Kwani baada ya kupata Uhuru kuna kutawalana tena? Au imebaki kuongozana?

Ndiyo maana tunachagua watu miongoni mwetu watuongoze na siyo watutawale.

Wakoloni tu Ndiyo walikuwa watawala maana walitumia nguvu bila sisi wenyewe kuridhia lakini baada ya Uhuru tunachaguana na kupeana ridhaa ya kuongozana kwa utaratibu tulojiwekea kupitia Katiba na sheria ndogo ndogo.
 
Back
Top Bottom