The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 10,959
- 13,427
Kwa hesima, tumekaa ndani tena kwa adabu kuliko wafungwa.
Tumesherehekea uhuru bila uhuru kama wafungwa kwa sababu ya kumtii na kumpenda tukiogopa kumuudhi.
Tumekubali kugeuzwa wafungwa ili kuonyesha heshima na uzalendo wetu.
Tumetulia hata wale walioikuwa wamepanga kuandamana kwa kuogopa kumuudhi mama yetu kipenzi na mpendwa mwenye maono na mtenda maajabu kama ambavyo ameonyesha leo.
Tumeweza kuonyesha tulivyo taifa la amani.
Haijawahi kutokea popote duniani.
Wageni washindwe. Kwanini pesa wawahonge vijana wetu badili ya kuwapa viongozi wetu?
Wajue kazi yao ni kutoa pesa za mikopo na misaada siyo ushauri wala kutukosoa. Uliona wapi?
Pia, tuwaonye diaspora wanaopenda kuunga mkono maandamano. Kazi yao ni kubeba maboksi na kuwekeza nyumbani lakini siyo kukosoa.
Hawajui kuwa baniani mbaya kiatu chake dawa?
Mama ziiii, sorry, hoyeeeeee!