kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 753
Habari zenu wana jf.
Nimeshindwa zuia hisia zangu juu ya hii jinsia ya kike na umuhimu wake hapa duniani nikaona nije nitiririke huku ili kama kuna wenzangu wenye hisia kama zangu juu ya kiumbe huyu basi tufarijiane kwa kutambua nafasi muhimu ya mama.
Mama ni kiumbe jinsia ya kike ambacho kinaweza kuwa binadamu au viumbe vingingine kwani hata kifaranga nae mama yake kuku jinsia ya kike(tetea), ingawa tumezoea sana kulitumia kwa binadamu na hata mimi nipo upande huu wa binadamu na_declare interest.
Ukuu wa mama nauona ndio unabeba maisha yako yote, mama anakubeba tumboni mwake, anakuzaa kwa tabu na mateso makubwa na mda mwingine anapasuliwa tumbo lake, anakunyonyesha, kukusafisha kila aina ya uchafu, pia anahakikisha umekula na kushiba muda wote (yupo teyari wewe ule yeye akae na njaa). Ukiumwa mwanae yeye nae atakosa raha na muda mwingine unaweza sema nae ni mgonjwa. Ukifurahi nae hufurahi sana tena zaidi yako, lakini mwanae ukifanikiwa nae huhisi kafanikiwa zaidi ingawa baadhi yetu tumekuwa tukiwatupa mama zetu! Rudi kwa mama mwambie mama ahsante kwa kunifikisha hapa.
ONYO na KATAZO, usithubutu kumdharau mama kwa namna yoyote ile mama ndie kiumbe mkuu duniani aliyebeba baraka zako hapa duniani. Usimtukane mama wala kumdhihaki,hasa kwa wale vijana wenye kujawa na maneno ya viungo vya akina mama midomoni mwao mda mwingine wakitumia kama tusi na mda mwingine kupeana sifa...acheni hiyo tabia lakini wengi wenye kutamka hivo hata maisha yao huwa ni ya shida sana kwa upande mwingine inawezekana ikawa ni moja ya pigo kwao kwa kumdhihaki mama kupitia kiungo chake.
Mama nakupenda sana, ahsante kwa kunifikisha hapa nilipo nitakuheshimu daima.
=============
Kalenga kidamali