the glassroof
JF-Expert Member
- Apr 25, 2017
- 279
- 422
Ni mara tatu sasa mfululizo nakumbwa na matatizo ya umeme tena mida mibovu.
Kwa mara ya kwanza, tatizo lilipotokea sikujua nianzie wapi bahati nzuri nikapekuwa majina kwenye phone book yangu nikakuta jina moja la mtumishi wa TANESCO.
Nikampigia nakumuelezea tatizo langu, kwa kuwa ilikuwa mida mibovu akashauri niwapigie emergency mara moja.
Akili yangu ikanituma bora nipotezee tu, emergency na wabongo wapi na wapi. Na nikikumbuka TANESCO niliyokuwa naifahamu mmi, kuwapata mpaka utambikie.
Ila nikajisemea tena ngoja nijaribu.
Ile kupiga tu, napokelewa na mdada fulani akajitambulisha vizuri kabisa. Nikaeleza shida yangu mpaka mwisho bila kikwazo chochote.
Alichofanya yeye, ni kuniuliza mtaa ninaoishi na namba ya simu. Mwisho akasema, subiri muda si mrefu emergency watafika hapo kukusaidia na ilikuwa mishare kama ya 2 hivi usiku.
Mungu si athumani, by saa 3:30 usiku hivi simu ikaita, kucheki namba mpya nikapokea. Kijana mmoja kajitambulisha na kusema simama barabarani gari ya TANESCO itafika hapo hivi punde.
Mara paaaap! Vijana kweli hawa shusha ngazi panda rekebisha mambo safi kabisa bila kudai chochote. Wakanipa kijikaratasi fulani wao wanaita TB nadhani, ili asubuhi yake nifike ofisini kukamilisha suala langu.
Kesho yake huyo mjengoni, huduma safi kabisa, mpaka nikasema kulikoni ofisi hizi. Anyway, chap chap huduma nikapewa nikaenda zangu.
Baada ya siku kadhaa, Mita yangu ikapata hitilafu tena mida mibovu, nikapiga emergency, muda si muda hawa hapa wakatua. Ile kuchek Mita kumbe imeungua wakaahidi kesho watakuja kunibadilishia, bila hiana kesho yake mapemaaa! timu hiyo home wakabadili Mita bila longo longo na mpaka sasa nakula good time tu.
Haya yakiwa yanatendeka majirani nao wanashangaa kulikoni huyu jamaa anahudumiwa fasta kiasi hiki au wale wale. Kumbe wala, mie pangu pakavu sijui hili wala lile katika fani hiyo.
Siku ya siku mmoja wapo wa majirani zangu akapata shida, akaja kwangu nakuomba niwapigie. Kwa kujiamini kabisa nikavuta waya na bila kupoteza muda kama kawaida yao TANESCO wakafika na kutatua tatizo la jirani ambaye ni mfanyabiashara anaetegemea umeme asilimia ili mambo yake yaende.
Kutokana na experience hiyo waungwana nisiwachoshe, TANESCO Dodoma, kusema ukweli mmetisha kinoma noma. Taasisi zingine za serikali zijifunze kwa hawa jamaa.
Ni hayo tu. Big up sana na Mungu awabariki.
Sent using Jamii Forums mobile app