Pongezi kwa Mkandarasi barabara Moro-Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi kwa Mkandarasi barabara Moro-Iringa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir echa, Jul 23, 2011.

 1. s

  sir echa Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa moyo safi kabisa napenda kumpongeza/kuwapongeza wakandarasi walioetengeneza na wanaomalizia barabara hiyo,nilikuwa nina muda kidogo sijapita njia hiyo leo ndo nimepita,ki ukweli sikuamini macho yangu jinsi barabara ilivyotulia hasa kipande cha kutoka mikumi hadi iringa kuna maeneo yalikuwa kero kupitiliza kiasi ambacho hata magari kupishana ilikuwa patashika,lakini leo nimepita magari yanapishana vizuri kabisa.

  Tahadhari:
  Wasimamizi na wakaguzi tunaomba wathibitishe ubora wa barabara hizo isijekuwa ni bomu ambalo litalipuka miaka michache ijayo,na wenye magari ya mizigo tunaomba wapitishe uzito ambao unastahili na kuzingatia matumizi bora ya barabara.
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  wamechemka kwenye Matuta... kwenye kila kitongoji wameqweka Matuta khaaaaa...
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Amri ya TANROAD
   
 4. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,583
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu ile road kwa sasa naikubali viwango vyake naona vimetulia.Me nilikuwa napita hata wakati wanaitengeneza kwa kweli ilikuwa tofauti na zile za Igunga-Nzega (za Wachina)!Hii viwango vyake ni kama vya ile ya Nzega-Tinde-Shy mpaka mpakani mwa Shy na Mza.Wale wa-South Africa waliisuka haswa.
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kumbe ndo maana inachinja wa2 daily.
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kuna majamaa wanavunja lami nzuri ya zamani ndani ya hifadhi ya mikumi, na kuweka lami yao fake. Kwa kweli ukiona tu utashtuka.
   
 7. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shukrani kwa niaba ya wenzangu lakini acha niwe mkweli,barabara inavutia ila subirini pot-holes za kutosha after 2 or 3 yrs.Tunajiandaa pia na kipande cha iringa-mafinga(km 69.8) kwa kiwango cha lami.Kwa hii ya mafinga angalau itakuwa bora kwa sababu jiwe litakalotumika ni zuri zaidi kuliko lile lililotumika kuanzia iringa-kitonga gorge-iyovi(km 159).
   
 8. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hahaha nimepita juzi,wanaojenga wamejipanga vifaa vya kutosha,nimependa hata mimi,wanastahili kupewa pongezi,ila wakazane.
   
 9. m

  mbweta JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Balabala imetulia ile mbaya cjuh kwa upande wa ubora.
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hapo pekundu !!!!

  Sehemu waliyoniburudisha ni jinsi walivyopanua pale Ruaha Mbuyuni/Ilula na Check point, wameweka maegesho ya muda kwa magari makubwa na madogo kando ya barabara kiasi kwamba wanaopita moja kwa moja hawapati shida kama zamani.

  Kutoka Ipogoro kwenda Iringa mjini wameweka fly over ili magari yapite juu na waenda kwa miguu wapite chini. Na wamama wabeba nyululu sasa wanavuka barabara kwa raha zao. Matuta yamezidi pale mlimani kuelekea Iringa mjini.
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Ile kambi yao imejengwa vizuri sana pale njiani,sijui wakishamaliza ujenzi tutaifanyia nini?
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu ni iyovi kuja iringa town sio mikumi!
  Jamaa wako vizuri na hata gharama zao ziko juu bse kwa km moja wanatumia atleast a billion wakati mchina wa iringa to mtera anatumia 700mil/km
  Big up sana twangoja mkeka wa iringa to mafinga
  Nb:hawa jamaa ndo walijenga chalinze to moro huwa hawabahatishi JV aarself interbeton
  Na kuna package wanajenga kule sumbwanga.
  I wish wangepewa nchi nzima
  n
   
 13. C

  Calist Senior Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pale hakuna ubabaishaji, imejengwa kwa viwango vya kimatafa nawahakikishieni itadumu kwa muda mrefu sana.
   
 14. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watawapa wamama walio pembeni,wanaopika chakula pale!
   
 15. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wamejitahidi lakini wamejenga tangu nipo third year(2007/08) hadi sasa nimeshamaliza internship. Ngoja tusubiri itakaa miaka mingapi.
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Duh Big Up sana km barabara ipo Poa.
   
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeiona hasa ukarabati unaenda kwa kasi zaidi maeneo ya milima ya Kitonga
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ila mpaka sasa washaingia hasara ya. Zaidi ya 1.5billion kwa wizi wa mafuta,cement,guardrails,roada signs kufanywa scaper etc
  Dr G jamaa walianza ujenzi 2009 na sasa wako ukingoni wanahamia ya kwenda mafinga
   
 19. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Boss si kweli mi naenda iringa kila likizo maeneo ya iyovi muda mrefu sana magari yanapishana tangu muda niliotoa hapo na uhakika, labda kama makandarasi wanabadilika
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kijana nina vijana wanafanya pale kama consultant cowi as of today bado km kam 3 kumalizia na wanacomission in two month time.
  Ili wahamie hii ya mafinga i
   
Loading...