Pongezi kwa JMK

wililo

Member
Apr 25, 2015
78
27
Ni kweli kila kiongozi anazama zake, ila nachelea kumpongeza mh.JMK katika uongozi wake amejitahidi kuendana na mahitaji ya watanzania. Mfano alianzisha vyuo vikuu na kutoa kipaumbele kozi za sayansi na walimu ili kuziba pengo la uhitaji la wataalamu, japo watu wanalaumu mpango huo. Baada ya kuona upungufu wa walimu wa sayansi shule za kata akanzisha stashahada ya sayansi kwa ajili ya sekondari miaka mitatu, na hilo nalo watu wameona ni baya wakati huo hawaji na mbadala. Alijitahidi kutumia diplomasia kutatua migogoro mbalimbali kitaifa na kimataifa.

NB. mabadiliko tunayapenda ila lazima yaendane na mahitaji ya taifa na kwa kuzingatia vipaumbele. mfano shule za misingi darasa moja lina wanafunzi 500 unaleta madawati bila kuongeza walimu na vyumba vya madarasa.
 
Back
Top Bottom