Pongezi kwa Jimbo la Geita, dunia imewasikia

MCHAPAKAZZ

Member
Mar 29, 2016
31
18
Mmempata Askofu mwenye elimu,busara na jasiri. Kwa mfumo uliopo msingefanikiwa kumpata Askofu Kassala lakini kwa kupambana na kusimamia taratibu za msingi mwisho mmefanikiwa kumpata yule anayewafaa.

Baada ya jimbo kuwa wazi march 2014 mchakato ulianza kufanyika wa kawaida,ambapo majina yalipendekezwa miongoni mwa wanajimbo na yakapelekwa kwenye ngazi inayohusika ambapo Askofu Kassala(padri kipindi icho) naye jina lake lilikuepo.

Majina yaliporudi(yaliyopitishwa) jina la Kassala lilikuepo ila likakatwa na kuwekwa majina mengine ya watu ambao hawakupendekezwa hapo ndipo shida ilipoonza na kusababisha mchakato kuwa mrefu nakufanya jimbo kuwa wazi hadi April2016 tangu March 2014. Pongezi kwa wanajimbo wa Geita,mapadri na aliyekuwa msimamizi wa jimbo hilo kwa kuruhusu busara itawale katika maamuzi.

Mfano huu mzuri wa Geita uigwe na wanajimbo wa majimbo mengine katika kutetea maslahi ya kanisa tusisite kusimama kidete kupinga maslahi ya watu fulani, mfano huu uigwe na Jimbo la Mbulu katika kuj ikwamua katika hali inayoendelea na kukwamisha mchakato halali...Hongereni Jimbo la Geita
 
Hakika Geita wamepta Askofu bora, kwa kipindi kifupi nilicho mfahamu Padri Kasala wakati huo now Askofu hapa Arusha nilijifunza mengi kwake, ni mtu mwenye busara, mnyeyekevu wa hali ya juu, mwenye maono ya mbali hasa kwa vijana, anae hubiri kulingana na wakati, nilisikitika sana alipo ondolewa Arusha na kupelekwa Mtwara. Hongereni na mjitahidi kumuombea Mungu ili kazi yake ifanyike bila makwazo.
 
image.jpeg

"Siasa" za Kanisa Katoliki na Vatican ni za aina yake..."Vurugu" ni nyingi lakini zinaenda kwa usiri sana sana sana,ama hakika mchakato wa kumpata huyu ndugu ulikuwa mgumu sana.

Anaenda kukamata moja kati ya Majimbo magumu kuyaongoza,Ni imani yangu kuwa mwenyezi Mungu,Mwingi wa rehema na huruma atamuongoza,alichokianzisha ndani yake akitimize,si kwa manufaa yake,bali manufaa ya kanisa na familia ya Mungu kote duniani.

Jamaa kwa umri wa kikanisa bado kijana sana...Miaka 15 ya Upadre kapata nafasi ya Uaskofu..When the Vatican Speaks,Others Respond

Ora et Labora
 
Hii mada ni ngumu kuchangia! Japo nina swali dogo: msimamizi wa jimbo alikuwa nani?
 
Msimamizi wa jimbo alikuwa anaitwa Renatusi Nkwande alikuwa Makamu Askofu wa Jimbo la Mwanza
 
View attachment 343423

"Siasa" za Kanisa Katoliki na Vatican ni za aina yake..."Vurugu" ni nyingi lakini zinaenda kwa usiri sana sana sana,ama hakika mchakato wa kumpata huyu ndugu ulikuwa mgumu sana.

Anaenda kukamata moja kati ya Majimbo magumu kuyaongoza,Ni imani yangu kuwa mwenyezi Mungu,Mwingi wa rehema na huruma atamuongoza,alichokianzisha ndani yake akitimize,si kwa manufaa yake,bali manufaa ya kanisa na familia ya Mungu kote duniani.

Jamaa kwa umri wa kikanisa bado kijana sana...Miaka 15 ya Upadre kapata nafasi ya Uaskofu..When the Vatican Speaks,Others Respond

Ora et Labora
Fafanua kidogo mkuu,mchakato ulikuwa mgumu namna gani?
 
Jimbo la Geita nadhani litakuwa jimbo la kwanza kuongozwa na askofu mwenye umri mdogo kuliko wote pia itakuwa historia kwa wazazi wa Askofu Kasala kushuhudia mtoto wao akipata daraja la upadri na daraja la uaskofu mahali pale pale ni jambo la kumshukuru Mungu
 
Ni bahati nzuri umeanza na neno "nadhani",kwa sababu katika historia ya Maaskofu wa kizazi hiki kipya,Askofu Nyaisonga aliyekuwa Dodoma kabla ya kupelekwa Mpanda ndio alikuwa mmoja wa Maaskofu vijana akiwa na umri mdogo tu.Wazazi wake wakiishudia Upadre na Uaskofu wake

Tarcicius Ngalalekumtwa akiwa kama Askofu Mwandamizi Jimbo la S'wanga aliteuliwa akiwa kijana wa miaka 40 tu,wakati Mhashamu Askofu Timanywa ndio alipata kwanza akiwa na umri mdogo lakini pia akiwa na miaka michache ya upadre

Historia haimpi nafasi hiyo Mhashamu Askofu Flavian,japo anaingia kwenye kundi la waliopata wakiwa bado vijana kwa umri wa kikanisa...Tumsifu Yesu Kristo ndugu Muangila
 
Naomba nisaidiwe pia. Je ni kweli kuna kikao cha jimbo kinachopendekeza mapadre kuwa maaskofu jimbo linapokuwa wazi? Roma locuta Causa finita.
Ndio mkuu kapiki
Kuna kikao maalumu na cha siri kubwa ambacho hukaa na kupendekeza.Wapo wengi waliokatwa majina na wenzao kwa sbb mbalimbali,pia ni ukweli kuwa kuna waumini pia chini ya kiapo hupewa formu ya kujaza na kumeulezea mtarajiwa wa uaskofu,hii hupewa wale wanaonekana kumfahamu sana na wanatakiwa kujaza bila kupendelea
 
View attachment 343423

"Siasa" za Kanisa Katoliki na Vatican ni za aina yake..."Vurugu" ni nyingi lakini zinaenda kwa usiri sana sana sana,ama hakika mchakato wa kumpata huyu ndugu ulikuwa mgumu sana.

Anaenda kukamata moja kati ya Majimbo magumu kuyaongoza,Ni imani yangu kuwa mwenyezi Mungu,Mwingi wa rehema na huruma atamuongoza,alichokianzisha ndani yake akitimize,si kwa manufaa yake,bali manufaa ya kanisa na familia ya Mungu kote duniani.

Jamaa kwa umri wa kikanisa bado kijana sana...Miaka 15 ya Upadre kapata nafasi ya Uaskofu..When the Vatican Speaks,Others Respond

Ora et Labora
Roma locuta causa finita.
 
Back
Top Bottom