ashy da don
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 615
- 671
Wakuu habari za jioni humu ndani.
Najua wengi wetu ikiwemo mimi tunawachukia sana askari polisi kutokana na vitendo vyao vya unyanyasaji kwa raia.
Kwa hili nililoshuhudia hapa kituo cha stesheni ningeomba nichukue fursa hii kuwapongeza sana askari hawa. Takribani ni mwezi sasa nimeukuta utaratibu ambapo polisi husimamisha madaladala yote yanayotoka Mbagala rangi tatu, na Temeke na kuwaamuru wanafunzi wapande kwanza kwa utaratibu maalumu wa kupanga mstari na kila gari kuchukua wanafunzi takribani watano..
Utaratibu huu umenifurahisha sana kwani nikikumbuka enzi hizo nasoma Benjamin Mkapa tulikua tunasumbuliwa sana na makonda hadi kufikia hatua ya kuleta uadui kati yetu na wao.
Nachukua fursa hii Kuwapongeza jeshi letu hili la polisi na kuomba rai kwa vituo vingine kuiga mtindo huu kama polisi hawa..