Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,101
- 128,716
Wanabodi
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe.
Huu ni wito kwa wana tasnia ya habari, "Moja shika sii kumi nenda rudi " and "if you can't get what you want, then just take what you get", kumaanisha, ukikosa kile ulichokitaka, pokea kile ulichopatiwa, hata kama sio kile ulichokitaka, wakati ukiendelea kutafuta kile unachokitaka.
Kilio kikubwa cha media ya Tanzania, ni kutoheshimika na kutothaminiwa kama fani nyingine muhimu za wanasheria, madaktari, wahasibu, nah ii fani mpya ya kisasa ya machawa, kwenye mikutano muhimu, machawa wanapangiwa viti vya mbele, waandishi tunatupwa nje!.
Lakini sasa baada ya kuundwa kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa habari, heshima imeanza anza, tutoe ushirikiano wote kwa utekelezaji wa sheria hii mpya, lakini pia tuisaidie kuishauri bodi hii, ili kuizuia, badala ya kuwa neema kwa waandishi, ikageuka ni neema kwa waandishi wakubwa tuu, lakini ni mwiba kwa waandishi chipukizi.
Ibara ya 5: Kwenye majukumu ya Director of Information Services, ameonyeshwa atasajili print media pekee, lakini sio broadcast media, hili ni tatizo!, siku zote tunataka waandishi wa habari na watangazaji tuwe kitu kimoja, tuunganishe vyombo vya habari vyote nchini Tanzania chini ya mwamvuli mmoja. Mpaka sasa vyombo vya habari vya print ndio viko chini ya wizara ya habari, nah ii sheria mpya ya habari, halafu vyombo vya habari vya utangazaji, TV, Redio na Online, viko chini ya wizara ya mawasiliano, na sheria ya utangazaji chini ya TCRA.
Bodi ya Ithbati imekuja na lile hitaji la mwandishi wa habari lazima awe na vyeti vya kitaaluma kwa kiwango cha Diploma, hivyo ndivyo sheria mpya ya habari inataka mwandishi wa habari lazima awe na angalau diploma ya habari. Hitaji hili ni neema kwa waandishi wa habari wa magazeti, na mwiba kwa watangazaji na online media.
Kwanza mimi kama mwandishi wa habari mkongwe, naunga mkono hoja hii kwa asilimia 100% kwa 100% ili kujenga heshima ya tasnia ya habari as a professional, kama walivyo wanasheria, madaktari, mainjinia na professional nyingine zote.
Lakini uandishi wa habari na utangazaji, zaidi ya taaluma, pia ni kipaji, lakini pamoja na kipaji, ili mtu awe mwandishi au mtangazaji lazima apite shule ya habari kupigwa angalau msasa tuu wa certificate. Nilipoajiriwa RTD, unapimwa kipaji tuu, halafu mafunzo ya kazi unayapatia kazini, kupitia mafunzo kazi kwa kozi ya Radio Induction Course.
JAB imewaweka waandishi wote wa habari kwenye tenga moja la diploma!. Hii sio sawa, hata baharini na kwenye maziwa, kuna samaki wakubwa papa na nyangumi, kuna samaki wa kati, sato, sangala na kambale, na kuna samaki wadogo dagaa!, wote ni samaki, kuwawaeka samaki wote kwenye tenga moja kubwa la nyangumi, papa, sato sangala na dagaa, sio kuwatendea haki dagaa, watatafunwa wote na samaki wakubwa!.
JAB imeanza kuwakaba dagaa wasio na diploma na kuwazuia kuwa waandishi wakati wana vipaji na hawana vyeti! Nashauri tuwagawe waandishi kwenye makundi makundi ya accredited expert profession journalist lazima wawe na shahada ya Chuo Kikuu, masters na PH.D au zaidi waitwe ma ekpati wa uandishi ili kujenga heshima kama tasnia ya sheria.
Kwenye tasnia ya sheria , japo kuna certificate, diploma na degree, mtu huwezi kuwa advocate hadi kwanza uwe na degree, kisha uende Law School ndipo usajiliwe na mahakama kuu kama wakili. Hata uwe na diploma mia, hata uwe na Ph.D ya sheria, kama huna LL.B huwezi kuwa wakili. Kama kwa wanasheria hili limewezekana kwa nini kwa waandishi lisiwezekane?
Waandishi wa kawaida wa diploma, ndio iwe ngazi ya professional journalist, kama kinachofanywa sasa na JAB. Lakini kuwe na kundi la media contributors, hawa ni waandishi wenye fani nyingine ambao wanaandika na hawa diploma ya habari, watambuliwe!. CNN, BBC, VOA wanawatumia ma expert wa fani nyingine kutoa expert opinion. Tuwaruhusu.
Kuna wenye certificates wasajiliwa kama assistant journalists lakini sio professional journalist. Na waandishi wengine wote wenye vipaji lakini hawana vyeti, wasajiliwe kama trainee journalists, milango ya kujiendeleza ifunguliwe, wajiendeleze na sio kuwafungia na kuwatimua newsrooms.
JAB ni fursa ya kuijengea heshima tasnia ya habari kama taaluma yenye kuheshimika kama taaluma ya sheria, na wanahabari tuwe kama ilivyo kwa wanasheria, ili mtu awe wakili, lazima kwanza apate shahada ya sheria, LL.B, wale wengine wote wenye certificates au diploma za sheria, ni ma para legal na sio mawakili. Hivyo Waandishi pia wagawanywe makundi, professional accredited journalist ili kuwa Accredited Journalist lazima kwanza uwe na a university degree ya journalism or related field.
Kwa mujibu wa sheria hii, kama nilivyosema mwanzo, hii ni ile Newspaper Act ya 1976 iliyoboreshwa, hiyo bodi ya Ithibati isiwe rigid kusajili waandishi wa habari wa diploma tuu.
Sheria hii mpya ya Habari ni ile ile Newspaper Act ya 1976, iliyoboreshwa ambayo ina deal na print tuu, broadcast iko wizara nyingine, mamlaka nyingine chini ya TCRA, kule unajisajili kwa TZS 1.M, kisha unapeleka unlimited number ya waandishi wa social media ambao hawana cheti chochote!.
Bodi ya Ithibati iangalie fani ya utangazaji ni vipaji na sio vyeti, kuwataka watangazaji wote wawe na diploma ni kuwaonea bure!. Baharini papa na nyangumi , sato na sangala ni samaki, lakini hata dagaa pia ni samaki na ana haki ya kuishi sio tuu kuliwa na samaki wakubwa!. Hawa hawa dagaa wa uandishi wasio na diploma, ndio vipaji vinavyoendesha redio zote na mitandao ya kijamii, tusiwafungie kufisha vipaji vyao, tuwawekee dirisha dogo la usajili.
Hongera JAB kwa mwanzo mzuri, mna kazi kubwa mbele yenu.
Mungu ibariki JAB
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu uandishi wa habari

- Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!
- Siku ya Uhuru wa Habari: Hakuna Uhuru wa Habari bila Uhuru wa Kiuchumi wa Waandishi wa Habari
- Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa
- Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.
- Vyombo Vya Rasmi vya Habari vya TZ, Havitimizi wajibu Wake, Njaa, Ukata, Ujinga!. Waandishi, Wamiliki Watakiwa Kujiongeza- Jicho Letu Star TV
- Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa Habari, News Analysis-Jicho Letu