tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania ambaye ni mwanachama wa ACT Wazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa wito wa umoja na ushirikiano kwa Watanzania wote katika kupinga kile alichokiita sheria kandamizi.
Akizungumza na Wilberforce Ngoto katika kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, Sheikh Ponda ameeleza kuwa mshikamano unahitajika kupinga sheria zinazokandamiza haki za watu akidai kuwa hata wale wanaokandamiza haki za watu wanatumia vifungu ‘vibovu’ vilivyoko kwenye sheria.
Soma pia: ACT Wazalendo yamtambulisha Sheikh Ponda Issa Ponda, leo Juni 5, 2025, asema Sheria ina mifumo kandamizi
"Hizo sheria ni sheria mbovu ambazo zipo kwenye mfumo wetu wa sheria na ni lazima tupambane kuziondoa hizo sharia, kama hatutapambana kuziondoa hizo sheria ni tatizo kubwa kwasababu hata wao wanatudhulumu na kutukandamiza kwa mujibu wa sheria", amesema Ponda.
Aidha ameeleza kuwa watakaoingia bungeni ni vyema washinikize mabadiliko ya sheria ili kuondoa sheria ambazo zinaonekana kuwa adui wa haki za binadamu na Watanzania wote kwa ujumla