Ponda havumiliki

Ponda havumiliki

Hizo ni propaganda ulizopangiwa uziseme na makanisa. SHEIKH PONDA ni msomi wa dini ya kiislamu. Uislam hauruhusu kuuawa nafsi ya mtu yeyote pasi na makosa. Na kisha Waislam wameamrishwa kuishi kwa wema na watu wote yaani Mayahudi na Manaswara. Wewe ulimsikia wapi akisema kauli hiyo?

Mnaomtetea Ponda wote akili zenu zimebunguliwa na mdudu aitwaye UDINI. Ponda hastahili hata kuitwa sheikh. Huyo ni baladhuli mkubwa anayeivuruga amani ya nchi hii. Hakuna haja ya kumpa masikio yetu mtu anayetolea dukuduku lake misikitini. Hata kama nia yake ni njema bado kwa njia anayotumia inaleta mashaka. Ponda hana tofauti na makaburu wa afrika kusini waliotumia rangi kueneza ubaguzi, huyu Ponda anatumia udini. IGP mwema tuma vijana wako wakamate mbaguzi huyu. Ni bora mtu mmoja akafa walio wengi wakaishi kwa amani, badala ya mtu mmoja kuachwa akisambaza sumu ya ubaguzi wa kidini kama Ponda.
 
wewe muelewe ponda hapa kwa maelezo ya ukweli kuhusu huyu mtu

Muda si mrefu nimetoka kuongea na shuhuda mmoja aliyekuwepo Morogoro. Ni kweli kuwa Sheikh PONDA amejeruhiwa vibaya kwa RISASI. Huu ni mwendelezo wa matukio ya kuwawinda viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari na wanaharakati ambao serikali inaamini ni watu hatari.
Hivi karibuni, taarifa za ndani za serikali zimekuwa zikimuonesha Sheikh Ponda kama mtu hatari kwa usalama wa taifa, huu ni upuuzi na ujinga mkuu ambao utatupeleka pabaya.
Ikiwa kuna mtu ni hatari sana kwa taifa, na serikali ina ushahidi, kwa nini isimfungulie mashtaka mtu huyo na ipeleke ushahidi huo mahakamani ili mahakama ipime na kuamua au la!
Serikali inayotumia approach (mbinu) ya kushambulia, kujeruhi kwa nia ya kuwaua watu wenye msimamo tofauti na serikali hiyo, hii inakuwa serikali hatari, ya kijinga, dhaifu na iliyoshindwa kuongoza, serikali ya namna hii is more dangerous to the peace of the nation than the dangerous persons themselves (serikali ya namna hii ni serikali hatari mno kwa amani ya taifa kuliko watu inaowadhania kuwa hatari.
Mimi nachojua, Sheikh Ponda ni mwanaharakati wa kiislamu anayebeba matumaini, hoja na visheni ya waislamu walio wengi. Kwa upande mwingine serikali ya CCM inamuona Sheikh PONDA kama mtu hatari kwa sababu hoja na visheni zake vikifanikiwa vitawatoa waislamu chini ya BAKWATA ambayo inatumiwa na serikali ya CCM kama nyenzo ya kuwadhibiti waislamu katika masuala yao ya msingi na hata baadhi ya haki zao muhimu za kiimani.
Serikali yoyote ya kipuuzi na iliyokufa a failed state haifikiri namna ya kutafakari hoja zinazokinzana na serikali na kuzitafutia ufumbuzi mezani. Hufikiri kutumia nguvu, kuwatisha watoa hoja husika na hata kuwaua pale nafasi inapopatikana, ilimradi udhibiti sensorship uendelee.
Serikali mfu kama ya CCM huwasha kiberiti yenyewe na baadaye huhaha kuzima moto ikiwalaumu watu wengine kwa matatizo yaliyoanzishwa na serikali yenyewe.
Ikiwa viongozi tutachekelea unyama huu na kuacha fulani atambuliwe kama mtu hatari sana ATI kwa sababu tu yeye ni dini fulani, ni kweli mhusika atashughulikiwa ipasavyo, atateswa tutachekelea, ataumizwa tutasheherekea na atauawa tutapiga nderemo na vifijo.
Serikali mfu haitaishia hapo, ikimaliza kumshughulikia yeye kwa dini yake itahamia kwako, itakuita mtu hatari sana kwa sababu ya chama chako, kwa sababu ya uanaharakati wako, kwa sababu ya uandishi wako na kwa sababu ya msimamo na mtizamo wako ambao unapingana na serikali. Nani atabaki salama?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, ukinywa damu ya mtu, utaendelea kunywa tu. Nami nasema, tukichekelea na kukubali propaganda za CCM kuwa Sheikh Ponda ni mtu hatari sana, akishamalizwa watahamia kwetu(kwangu na kwako), mimi na wewe tutapewa uhatari na tutasakwa kwa mtutu wa bunduki tuuawe haraka ili taifa libaki kuwa salama.
Serikali ya CCM iache mbinu hizi ambazo tulishazijua. Serikali ikatatue tatizo la msingi la MZOZO WA MIONGO KADHAA KATI YAKE NA WAISLAMU. CCM iwaache waislamu watafute uongozi wao huru kabisa, wanaouamini. Kufikiri ATI maoni ya waislamu yataendelea kusimamiwa, kuratibiwa na kuongozwa na BAKWATA ni kupoteza muda na kijidanganya. Mbona sisi wakristu tuna taasisi zetu muhimu na imara za kidini na tunaziamini? Kwa nini serikali ya CCM inaendelea kuwashika waislamu na kuwadhibiti kwa kuitumia taasisi ambayo waislamu hawaiamini?
Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, pamekuwa na marais wawili ambao ni waumini wa dini ya kiislamu, Mzee Mwinyi na sasa Mhe. Kikwete, hawa ni waislamu kabisa, ina maana hawajui malalamiko ya waislamu ya miaka nenda rudi? Kama Kikwete na wenzie walichoshwa na mauaji yaliyokuwa yanaendelea Zanzibar na wakaamua kuwaacha wazanzibari waamue hatima yao na Leo imeundwa SUK. Kina Kikwete haohao wanashindwaje kusema matatizo ya waislamu sasa basi na wakawaachia waislamu huru waamue hatima yao, wawe na vyombo wanavyoviamini visimamie maslahi yao. Mwinyi na sasa Kikwete siyo waislamu? CCM ina maslahi gani BAKWATA?
Mtizamo wangu pia ni kwamba, waislamu wanaweza kuwa wanamalizana wao kwa wao bila kujua.
Pale Marekani kulikuwa na tatizo la msingi kwa wamarekani wengi wa kipato cha chini, huduma za afya zilikuwa kuzungumkuti. Sehemu kubwa ya waathirika wa jambo hili walikuwa wamarekani weusi. Marais wote wazungu waliopita hawakuwahi kufikiri kulitatua, alipopata nafasi Obama akalibainisha Suala la afya kwa wamarekani wa kipato cha chini kama tatizo la msingi linalohitaji utatuzi wa haraka.
Obama akatengeneza muswada wa bima ya afya, akapambana hadi ukawa sheria, Leo wamarekani wa kipato cha chini ambao wengi ni weusi wanafaidika na mpango huo. Obama alipigwa vijembe kuwa analeta muswada wa kuwapendelea watu weusi lakini aliwapuuza wapinzani wake, alijua anafanya jambo ambalo litaondoa mgawanyiko na ukosefu wa haki muhimu ambalo lingeisumbua Marekani ya baadaye.
Hapa kwetu tuna marais wanaonea haya dini zao na wanashindwa kutatua matatizo ya msingi ya kundi ambalo wameliishi na kuonja adha ya kero zao. Kuwaacha waislamu wajichagulie vyombo huru vya kujiongoza ni kuongeza na kupanua wigo wa demokrasia na uhuru muhimu kwa watanzania wote, hili halitakuwa na faida kwa waislamu peke yao, lina faida kwa nchi nzima. Ni bora rais uitwe mdini kwa kuondoa udhibiti wa chama chako kwa taasisi ya kidini na kuiacha huru kuliko kuacha mifarakano na malalamiko ya kundi linalodhaniwa linaonewa kwa miongo kadhaa yaendelee.
Mimi nadhani waislamu wana matatizo ya msingi kati yao, panahitajika viongozi imara wanaoliona hilo. Ikiwa yataachwa au kushughulikiwa kwa mtindo huu wa kuvizia na kupiga RISASI wale wanaotetea maslahi halisi ya waislamu, hayatakwisha.
Ikiwa atauawa Ponda mmoja eti kwa sababu anadhaniwa kuwa mtu hatari, in the next morning watazaliwa Ponda wengine hatari zaidi wapatao 1000. Uhuru wa Dokta hauzimwi kwa RISASI.
Sote bila kujali itikadi zetu za kidini, kisiasa na kimtizamo, TULAANI KWA NGUVU UNYAMA ALIOFANYIWA SHEIKH PONDA.
Julius Mtatiro,
+255717536759.
Maoni haya ni yangu binafsi, yasihusishwe na chama changu wala nafasi yangu ya uongozi ndani ya chama.well said mkuu
 
Huko zanji kafanya mihazara ya uchochezi sili kali ikamuacha moro tena aaaaaaaaah sasa yatosha akamatwe mara moja


Kukamatwa? Sikia, Gaidi hana haki hivyo huyu inabidi anyongwe tu au afungwe maisha. Si bure kuna anachojivunia tu. Siku zote serikali inasema wachochezi wa siasa/amani wasivumiliwe na wachukuliwe hatua, why Ponda asinyongwe ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine? Yeye anataka sharia, basi aende kwao uarabuni.
 
kuna watu wanambwandambwanda tu we baada ya kuchangia mada unaingza ukafiri au ndo mawazo yako yalipokomea apo ukiona uko kidini zaid waachie uwanja wenye hoja za msingi waweke co unakuza izi tu bila hoja!! we anavumilika au havumilika shusha na evidence kaa pembeni.

Mkuu kuna watu nilikuwa nawakubali sana humu JF, ila kupitia uzi huu, lol nimewashusha.... Kumbe wanaongozwa na hisia zao na wala si uhalisia wa mambo? Jamani, itikadi zetu za dini zisitufanye wajinga! Imani yako kwa nini iwe kero kwa wengine?
 
Kafiri mkubwa wee, Tena unyamaze wala tusikuone tena hapa !! Kwenda ukafie na ukafiri wako hukoo!
Kweli kwenye msafara wa mamba na kenge wamo... I think, in future, kuna haja ya members wote tuwe verified users.. Hii itawafanya watu wafuate signature ya Invisible ya kwamba... Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!.... Kuna watu wanafanya kinyume cha hiyo signature... kama bwana life is Short


 
Kweli kwenye msafara wa mamba na kenge wamo... I think, in future, kuna haja ya members wote tuwe verified users.. Hii itawafanya watu wafuate signature ya Invisible ya kwamba... Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!.... Kuna watu wanafanya kinyume cha hiyo signature... kama bwana life is Short


My dear N. good morning, I am a respected person. Na ujio wangu ulikwa mwema kuliko member yyt.hapa.
Lakini malezi yenu na tabia zenu ndo zilizo nifikisha kuwapa ukweli na kuwa fundisha yakuwa " ukitukana UTATUKANWA"
ukijiheshimu utaheshimika. usiwe one sided, Tafdahli sana angalia BOTH sides. What you are talking is't TRUE at all.
Good luck and blessings.
 
Ponda anasema: " watu wote wasio waislamu ni makafiri, na makafiri lazima wauawe ili dola ya kiislamu isimame, na ukiua kafiri unapata dhawabu"



Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

kwa statement hii bila kumung'unya maneno Ponda havumiliki hizo kauli hapo zinaonyesha wazi UGAIDI.
 
My dear N. good morning, I am a respected person. Na ujio wangu ulikwa mwema kuliko member yyt.hapa.
Lakini malezi yenu na tabia zenu ndo zilizo nifikisha kuwapa ukweli na kuwa fundisha yakuwa " ukitukana UTATUKANWA"
ukijiheshimu utaheshimika. usiwe one sided, Tafdahli sana angalia BOTH sides. What you are talking is't TRUE at all.
Good luck and blessings.
Thank you for understanding... But despite this, mi nadhani, hata kama kuna mtu alishawahi kukutukana, you need to be you, na usiongozwe na matukio... Kwamba huyu kafanya kile basi nawe ufanye hiki, mbaya kuna mengine yanaharibu kabisa perception ya watu juu yako... UNAJUWA, KWA HIZI KEYBOARDS, THE ONLY WAY YA KUWEZA KUJUA TABIA YA MTU NI THROUGH POSTS ZAKE..
 
Huko zanji kafanya mihazara ya uchochezi sili kali ikamuacha moro tena aaaaaaaaah sasa yatosha akamatwe mara moja
Yaani we jamaa boya kabisa, hivi unajua maana ya Uchochezi, hebu ielezee jamii ya wana JF huo uchochezi ni wa nani na nini na kwanini? Usiropoke usilolijua
 
Thank you for understanding... But despite this, mi nadhani, hata kama kuna mtu alishawahi kukutukana, you need to be you, na usiongozwe na matukio... Kwamba huyu kafanya kile basi nawe ufanye hiki, mbaya kuna mengine yanaharibu kabisa perception ya watu juu yako... UNAJUWA, KWA HIZI KEYBOARDS, THE ONLY WAY YA KUWEZA KUJUA TABIA YA MTU NI THROUGH POSTS ZAKE..
With whole Respect to humankinds, Tunaweza hitalafiana kimawazo na kiiamni lakini heshima na utu unakuwepo pale pale bila kubadilika kwa mawanaadamu mwenzio. So mkuu everyone likes his mother na IMANI ya mtu ni kama mama yake.....
inapokuja kugeneralize ubaya kwa kuattack mama (imani)... hapo hakuna cha kusimamisha yaani madness ndiyo huReact.
konsikwes zake zawa unpredict.
Take care and good luck.
 
Hakika wengi hawamjui sheikh ponda zaidi ya kusikiliza propaganda chafu zinazoenezwa juu yake ila serikali ina haki ya kutambua wakimpoteza ponda leo watazaliwa kina ponda 100,000 kwa mwaka hadi watakapokuja tambua na kuwaacha waislamu wajisimamie wenyewe kama zilivyo dini nyingine.
Kwa hiyo PONDA ndio msimamizi wa WAISLAMU..!?
 
...si jamaa wamemchapa risasi, naona jamaa walilenga moyo wameukosa,duuh snipers noma sana...
Ushukuru hao snipers wako wamekosea shabaha maana wangetimiza lengo moto ambao ungewashwa mpaka sasa hata huo muda ulioutumia kubonyeza keyboard au kamchina kako usingeupata. Fahamu kuwa kuna waislamu zaidi ya 3/4 nchini wanaomkubari na kumuunga mkono Ponda idadi ambayo ni kubwa kuliko wapiga kura waliomuweka JK madarakani au kura zota za JK na Slaa. Usidhani kuwa hayo mabomu ya machozi yanayobebwa na vibaraka FFU yanaweza kukuhakikishia amani kama watu watakuwa fade up na kuamua "kama mbwai na iwe mbwai" kumbuka sakata la Mwembe chai vituo vingi vya polisi maeneo ya Manzese, Mburahati, Tandale na Kiduka vilivamiwa na polisi walikula chochoro. Sipendezwi na tabia ya Ponda kuvunja sharia kila siku tena kwa makusudi lakini kauli za kishabiki kama zako zitaliangamiza taifa, polisi wanapaswa watumie busara kushughulika na waalifu sio kukurupuka tu kisa Pinda kawaruhusu.
 
Great thinkers hawana majibu ya dizaini hii....

ila greater thikers wanatakiwa watoe majibu ya dizaini gani, mtu hasumbuki na -------- ndo maana ukajibiwa kulingana na upuuzi wako, hilo nalo linahitaji mtu aende shule, hivi unaweza kuniambia how can u be so'sure kama kote uliposema ameleta uchochezi? Kwa propaganda za media au? Umeshawahi kupata nakala ya cd ambayo anayoshtumiwa kaleta kauli ya uchochezi? Maana sehemu zote alizofanya mihadhara cd zake zipo? For ur information Na hata huko morogoro hakuongea cha sana zaid ya kuwaambia waislamu waliohudhuria pale kuwa sku hiyo yeye si mzungumzaji bali siku inayofuata ataongea msikit wa aljabar kwa hiyo waumin wajitokeze, haya kauli ya chochezi hapo ipo wapi? Unatakiwa uvarify kabla ya kupost vitu
 
Huko Tanzania Ponda ndiye kasoma sana DINI kuliko Late Sheikh Yahaya Khussein au anaelimu ya chuo kikuu ktk SIASA NA JAMII
 
Ponda anasema: " watu wote wasio waislamu ni makafiri, na makafiri lazima wauawe ili dola ya kiislamu isimame, na ukiua kafiri unapata dhawabu"



Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Ua kafiri ukapate mabikira akhera
 
Serikali imeyataka yenyewe kwanini ilimtengenezea mashtaka laini? NAshindwa kuamini iwapo kweli serikali ina dhamira ya dhati kuleta utulivu nchin.i really question the wisdon and rationale behind this.
 
Walah kwa matusi haya utaiona Firdaus inshallah
MHE.MKUU WANGU WEWE ULIKUJA NA FAUL GAME UKAINGIA KWA KIBURI NA UZUSHI... NAMI SIKUCHELEWA KUKUPA DOZI. NITASHUKURU UKIKUBALI APPOLOGY ZANGU KWAKO NA NINAOMBA SAMAHNI WOTE NI WAUNGWANA "sintofahamu imetupelkesha pabaya.... Allah ni mwingi wa rehema.GOOD LUCK
 
Back
Top Bottom